Kwa wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali 2019

Thefuture1

Member
Nov 20, 2019
15
22
Habari wanajamii, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Kwa kuanza niwape hongera wahitimu wa kada mbalimbali kwa kuzingatia changamoto za ajira zinazoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla vijana mliohitimu masomo ni wakati sasa wa kuanza safari ya ajira hivyo basi ni vizuri mkapeleka taarifa zenu TaESA kwani wanaweza kuwasaidia kutafuta internship na ajira kwa baadhi ya kada.

Nawatakieni mafanikio wote kwa ujumla wenu.
 
Baadhi ya kada kama zipi? Serikalini unaweza pata kupitia TaESA
 
Umetoa wazo zuri sana. Sitarajii mtu akauliza TaESA ni nini na wako wapi, ikiwa unatumia smart phone.

Mimi naongezea jambo! Tieni Akili zenu mimba ya biashara yaani uwe na wazo lako ambalo hata ukishinda biko basi unapeleka kuihudumia mimba yako.

Wasalaaam.
 
Hivi ni vizuri kwenda moja kwa moja katika ofisi zao au kuwatumia email?..nlishatuma cv yangu kupitia format waliyotoa hivi majuzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom