Hili jambo nimekua nikilifikiria kwa miaka mingi bila majibu.Hata wewe hapo ulipo jaribu kuangalia katika familia au ukoo wenu. Unaweza kuta katika ukoo au familia ndugu yenu mwenye roho mbaya ndiye mwenye uwezo kifedha kuliko nyie wenye moyo wa kutoa. Katika jamii tunazoishi yaani wale watu wenye huruma na moyo wa kujitolea kwenye matatizo ya wenzao huwa na maisha magumu au ya kawaida sana.
Labda ungetegemea kwa kadiri mtu anavyosaidia wenzake ndo na yeye mambo yake yanyooke lakini inakua tofauti.Wapo watu wengi waliofirisika kwa kusaidia ndugu au marafiki mwisho wa siku wakajikuta wameishiwa kabisa. Mbaya zaidi wale waliosaidiwa huanza kuwacheka na kuwakejeli. Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.
Upande wa pili ukiangalia watu wenye roho mbaya na wabinafsi huwa wanafanikiwa sana pamoja na roho zao mbaya. Hawa ni wale watu ambao hawatoi msaada hata kama mtu anaumwa labda kwenye msiba ndo utawaona wanatoa misaada ya sifa.Kwa nini iko hivyo wakati tunaambiwa kwenye dini kadri unavyotoa ndivyo unapata zaidi? Kwa nini mwenye roho ngumu ndo afanikiwe kuliko mwenye roho nzuri? Majibu yenu tafadhali. Pascal Mayalla, Mshana Jr na wahenga wengine, nahitaji busara zenu huku.