Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

★ Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba

> Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.

> Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.

> Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.

> Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.

> Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba

> Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.

> Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.

> Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.

> Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

★ JOTO

> Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.

> Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).

> Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

★ RATIBA MWANGA

> Angalia jedwali katika picha hapo chini

> Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35kwa kutumia digital balance

★ MAJI

> Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida).

> Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

★ CHAKULA

> Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders.

> Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).

> Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.

> Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

★ AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

a) Chick starter

Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

b) Grower

Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

c) Finisher

Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza.

★ CHATI YA ULISHAJI WA KUKU BROILER

> Angalia katika jedwali hapo chini

ZINGATIO: Jedwali hili lipo applicable kwa broiler waliokuzwa kwa wiki 6 pekee kwa wale wanaowatoa ndani ya wiki tano gharama za uendeshaji pia zinapungua.

★ BROILER TIPS

a) SIKU 1-5

Wape glucose na mchanganyo mmoja wapo kati yah ii ifuatayo;
> Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
> Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

CHAKULA

> Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

★ SIKU YA 6

> Vitamini (vitastress)

★ SIKU YA 7

> Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

★ WIKI YA PILI

> Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

★ WIKI YA TATU

> Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

★ WIKI YA NNE

> Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA TANO

> Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA SITA

> Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni

> Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo

★ HITIMISHO

> Na imani kwa muongozo huo hapo juu utakuwa msaada mkubwa kwa wale ambao wangependa kuanzisha project ya kuku wa nyama na pia kwa wale wenye project hiyo.

> Kama upo na uhitaji wa muongozo bora wa kuku wa mayai na pia formular za kutengeneza chakula cha Kuku ili kuepeuka gharama zaidi basi usisite kuwasiliana nasi nasi tutaitikia wito wako

> Kwa maswali na msaada zaidi usisite kuwasiliana nami
C.E.O ( JMVC)
464bd28e64ec39af880e0018369f467d.jpg
0ade42736bc1cdb649c97aa62c435d78.jpg

Dr : Theriogenology
Phone : +255686236365 (whatsaap)
 
Naomba kuunganishwa pia kwenye hilo group la wafugaji wa kuku , na mpango wakuanza kufuga kuku mwezi watatu na malizia plan yangu kwanza no. 0758878692
 
Habarini wakubwa kwa wadogo...nipo hapa kushea kile ambacho kipo katika akili yangu na kinanisukuma sana kufanya hicho kitu...
Kwa ufupi nipo Dodoma mjini na sio mwenyeji sana maana nipo kikazi huku dodoma, kwa hiyo maeneo mengi siyajui Ila kadri siku zinavyozidi kwenda napatapata picha ya maeneo mbalimbali.
Katika akili yangu na nafsi yangu nashauku sana kufanya ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji, ambayo mwisho wa siku iwe kama seheehhemu ya biashara ya kuweza kuniingizia kipato cha ziada.
Swala la ufugaji ni kitu ambacho kipo katika damu yangu kwa sababu napenda sana wanyama.
Najua kuna ambao wanafanya hizi shughuli na wanajua changamoto zake na wanajua namna ya kutatua hizo changamoto lakini pia najua watakuwa na uelewa mzuri kuhusu mbegu zipi za jogoo na tetea ni nzuri kuanza nazo na bei zake.
 
Mkuu Karibu GMBD Consult ltd tunao uzoefu wa kutosha kuandaa michanganuo kutoa ushauri wa mradi wa kuku(broilers, layers, cross breeds n.k) ptunao uzoefu wa kutosha kwenye kunenepesha ngombe(cattle fattening), ufugaji wa nguruwe n.k Tuna mifano mingi Korogwe 9 kilomtre kutoka Segera on the way to Moshi kuna shamba la nguruwe (400) na Kuku (6,000), Cattle fatterning in Mtibwa, e.t.c Pia tunao uzoefu wa kutosha kwenye animal feed processing(Dodoma - Mapusa Rajab), Mbezi Luis (M & M Food Procesor) e.t.c karibu sana. wasiliana nasi +255715 737302 au +255784 737302 ama kwa email info@gmconsultz.com pia tembelea website yetu www.gmconsultz.com
mkuu ni dawa gani inatumika kunenepesha kuku wa kienyeji ? wawe na uzito mkubwa na pia wakuwe haraka?
asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom