Kwa wafugaji wa kuku wa kisasa | Page 75 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wafugaji wa kuku wa kisasa

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mlachake, Oct 23, 2009.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 3,098
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  Hey JF Members.

  Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. Naona soko la kuku ni kubwa sana. Hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss.. Yeyote mwenye idea naomba msaada please!

   
 2. Steven Nguma

  Steven Nguma JF-Expert Member

  #1481
  Nov 11, 2017
  Joined: Dec 6, 2016
  Messages: 400
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 80
  Ndio kuloiler unaweza fuga kienyeji na wana kubali
   
 3. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #1482
  Nov 12, 2017
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 937
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  *PATA ELIMU FUGA KUKU*

  Kutokana na shauku kubwa ya watu kutaka kufanya mradi wa ufugaji wa kuku kwa ajili ya kujiongezea kipato nimeona niendeshe mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wafugaji na watu wote wenye nia ya kutaka kufanya mradi wa ufugaji wa kuku kama kazi.

  Mafunzo haya ni ya siku tatu. Yataanza rasmi siku ya jumatano tarehe 15/11/2017 hadi 17/11/2017. Ni mafunzo yatakayotolewa kwa njia ya Whatsap kwa ada ya tsh 3000 tu.

  Tutamsoma kuku kwa undani kabisa. Tutaangalia mnyororo mzima wa thamani katika biashara hii ya ufugaji wa kuku. Tutaangazia changamoto mbalimbali. Hakuna kitu kitakachoachwa bila kufundishwa. Kuanzia Magonjwa, chakula, Uandaaji wa malighafi mbalimbali za kutengenezea chakula na uchanganyaji wake, namna ya kuanzisha mradi wa utotoleshaji wa vifaranga, utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku, namna ya kudhibiti vifo, Dawa salama za kuku, namna ya utoaji wa chanjo, Namna ya ujengaji wa mabanda bora ya kuku, masoko na mambo mengine mengi. Itatolewa pia elimu ya vitendo ili kuongeza uelewa wa wafugaji.

  Halikadhalika kutakuwa nafasi pana ya kuuliza maswali yatakayojibiwa kwa ustadi mkubwa. Kwahiyo hii ni fursa kwako wewe mfugaji au mdau unayetaka kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Kama ulikuwa na jambo lolote lililokutatiza kwa muda mrefu kuhusu ufugaji huu wa kuku basi hapa ni mahali pake pa kupata ufumbuzi. Mwisho wa mafunzo haya, kitabu cha mwongozo wa ufugaji bora wa kuku soft copy kitatolewa kwa mchango wa shilingi elfu kumi tu ni kitabu kizuri sana si cha kukosa kama unataka kufanya mradi wa ufugaji kuku wenye tija.

  Ufugaji wenye tija unaanzia kwenye maarifa sahihi. Usifuge kuku kwa kuwa umemwona fulani anafuga, fuga kuku baada ya kupata elimu sahihi. Ufugaji wa kuku bila elimu ni pasua kichwa.

  Kama utahitaji kujiunga na kundi la *PATA ELIMU FUGA KUKU* tafadhali wasiliana nami kupitia namba 0767989713 au 0715989713 ili nikupatie namba utakayofanyia malipo yako.

  Mara baada ya kukamilisha malipo, nitakuunga rasmi kwenye Group hilo la *PATA ELIMU FUGA KUKU*

  Mafunzo haya yataendeshwa na Ndugu Aman Ng'oma aliyebobea na kuwajua vizuri Kuku. Bwana Ng'oma ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd. Ndugu Ng'oma kitaaluma yeye ni afisa Mifugo, Mchumi Kilimo na Biashara, na pia Mtu wa Miradi. Ndugu Ng'oma ana Cert. Animal Health and Prod., Dip. Animal Health, BSc Agric.Eco.&Agr and Post Grad. Dip. Project plan.&Mgt.

  Wote mnakaribishwe kwenye mafunzo haya muhimu na ya aina yake kuwahi kufanyika.

  *Tafadhali saidia kushare*
   
 4. a

  antimatter JF-Expert Member

  #1483
  Nov 12, 2017
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 698
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  Ok, asante mkuu
   
 5. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #1484
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 937
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  *ANDAA DAFTARI, ANDAA KALAMU JIUNGE KWENYE GROUP LA WHATSAP LA "PATA ELIMU FUGA KUKU" UONE TOFAUTI*

  *Pata Elimu Fuga Kuku* ni kundi jipya la Whatsap lenye lengo la kutoa elimu kabambe na ya aina yake ya namna bora na yenye tija ya kuendesha mradi wa ufugaji wa kuku.

  Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa mfugaji wa kuku anapata elimu sahihi itakayomsaidia kuendesha mradi wa ufugaji wa kuku kwa faida. Kutokana nafasi niliyonayo ya kuwa kwenye tasnia hii ya kuku kwa muda mrefu kama mtaalamu na mzoefu, nina nambo mengi ya msingi ambayo naamini mfugaji akiyapata yatamsaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza ujuzi katika ufugaji wake. Hakuna atakayejuta kwa kushiriki darasa langu.

  Natambua katika ufugaji wa kuku kuna changamoto nyingi lakini kubwa ni vifo vya ghafla vya kuku, kutamalaki kwa magonjwa, utagaji usiyoridhisha, chakula kutokidhi viwango na bei yake kuwa juu, tija ndogo katika ufugaji, kukithiri kwa matumizi ya dawa, gharama za uendeshaji wa mradi kuwa juu nk

  Mradi wa ufugaji wa kuku si mradi rahisi kama ambavyo watu wengi wanadhani. Naamini waliyowahi na wanaofuga kuku wanalijua hili. Ufugaji wa kuku ni tofauti kidogo na ilivyo ufugaji wa wanyama wengine wenye miguu minne. Kuku anapoumwa anahitaji apate tiba haraka. Na tiba hiyo haiitaji kubahatisha. Lazima ugonjwa ujulikane, ujue pia dawa halisi. Vinginevyo utaishia kulia na kupata hasara kila siku wakati wenzako wakipiga pesa kupitia ufugaji huo huo wa kuku. Asikuambie mtu, kuku wanapokufa inauma sana kama una moyo mwepesi lazima Pressure ikushike hasa kama pesa iliyotumika kuanzishia mradi ulikuwa umeikopa.

  Kufugaji kuku bila kuwa na elimu ni sawa na kutaka kujitumbukiza kwenye shimo huku ukijua wazi madhara yake. Kuku wana kawaida ya kubadirika badirika. Unaweza ukawaona leo wazima lakini si ajabu baada ya muda mfupi ukashangaa wakaanza kuumwa na wanapoumwa haichukui muda wanaanza kufa mara moja.

  Vifo vinapotokea, mapigo ya moyo yataanza kukupanda, jasho litakutoka na hata usingizi utashindwa kulala. Mawazo mengi yatakujaa. Utawaza hasara unayoipata kwa kuwapoteza kuku wako.

  Kwa kuona hili nimeamua kuanzisha mafunzo haya maalumu kwa njia ya whatsap yatakayoendeshwa kwa siku tatu kuanzia tarehe 15/11/2017 hadi 17/11/2017 ili niweze kutoa elimu yangu kwa watanzania wenzangu kwa gharama ndogo kabisa ya shilingi elfu tatu tu ili kuwangozea maarifa wafugaji na wale wote wenye lengo la kutaka kufanya mradi wa ufugaji wa kuku kama kazi.

  Kuku wanahitaji uangalifu wa hali ya juu. Wafugaji wengi wanakosea sana. Unakuta anaanzisha mradi wa ufugaji wa kuku, halafu anamwachia mfanyakazi wake auendeshe. Ukimtazama mfanyakazi huyo, unakuta hajawahi kupata mafunzo ya aina yoyote hivyo anakuwa hajua hata zile ABC za ufugaji wa kuku matokeo yake mradi hauwi endelevu.

  Kwa msingi huo, kama unamfanyakazi wako anayekusaidia kwenye shughuli za uangalizi wa shamba lako si vibaya naye ukamlipia ada ya shilingi elfu tatu ili aweze kupata mafunzo haya muhimu, mafunzo yatakayo mwongozea maarifa na stadi za kuwahudimia kuku wako. Halikadhalika si vibaya kama utaamua hata mke wako naye ukamlipia ili aweze kushiriki na kunufaika na mafunzo hayo maridhawa.

  Maarifa siku zote hayaozi. Tunawahamasisha watumishi mbalimbali na hata wastaafu nao waweze kushiriki katika mafunzo hayo ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kutekekeza mradi wa ufugaji wa kuku kwa weledi.

  Kama utahitaji kujiunga na kundi la *PATA ELIMU FUGA KUKU* tafadhali wasiliana nami kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia namba 0767989713 au 0715989713 ili nikupatie namba utakayofanyia malipo yako.

  Mara baada ya kukamilisha malipo, nitakuunga rasmi kwenye Group hilo la *PATA ELIMU FUGA KUKU*

  Mafunzo haya yataendeshwa na Ndugu Aman Ng'oma aliyebobea na kuwajua vizuri Kuku. Bwana Ng'oma ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd. Ndugu Ng'oma kitaaluma yeye ni afisa Mifugo, Mchumi Kilimo na Biashara, na pia Mtu wa Miradi. Ndugu Ng'oma ana Cert. Animal Health and Prod., Dip. Animal Health, BSc Agric.Eco.&Agr and Post Grad. Dip. Project plan.&Mgt.

  Wote mnakaribishwe kwenye mafunzo haya muhimu na ya aina yake kuwahi kufanyika.

  *Tafadhali saidia kushare*
   
 6. mkombengwa

  mkombengwa JF-Expert Member

  #1485
  Nov 16, 2017
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 844
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 80
  Lini unatarajia kuanza mafunzo tena?nahisi tarehe zmepita...
   
 7. mbegubora29

  mbegubora29 JF-Expert Member

  #1486
  Nov 16, 2017
  Joined: Mar 14, 2015
  Messages: 222
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Acheni uongo jmn hiv mnajua faida ya mil 30?
   
 8. falcon mombasa

  falcon mombasa JF-Expert Member

  #1487
  Nov 17, 2017
  Joined: Mar 5, 2015
  Messages: 8,158
  Likes Received: 5,315
  Trophy Points: 280
 9. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #1488
  Nov 17, 2017
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 937
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Hatujafikiria bado ila ukihitaji masomo tuliyoyatoa tunaweza kukutumia kwa ada ya tsh 5000
   
 10. MILCAH28

  MILCAH28 JF-Expert Member

  #1489
  Nov 23, 2017
  Joined: Jul 9, 2014
  Messages: 1,096
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
  ( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..

  *_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
  * _Popote ulip0 dar unaletewa..*_
   
 11. MILCAH28

  MILCAH28 JF-Expert Member

  #1490
  Nov 23, 2017
  Joined: Jul 9, 2014
  Messages: 1,096
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
  ( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..

  *_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
  * _Popote ulip0 dar unaletewa..*_

  CALL-0752-109265
   
 12. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #1491
  Dec 5, 2017
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 5,212
  Likes Received: 3,177
  Trophy Points: 280
  Uko wapi?
   
 13. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #1492
  Dec 5, 2017
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 5,212
  Likes Received: 3,177
  Trophy Points: 280
  Naongelea Broiler, bado watuangalie kwenye bei ya vyakula, kwa kweli bei za vyakula kwa kuku wa broiler bado kubwa sana, wanaumiza...
   
 14. MILCAH28

  MILCAH28 JF-Expert Member

  #1493
  Dec 11, 2017
  Joined: Jul 9, 2014
  Messages: 1,096
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  niko ubungo dar es salaam nicheki

  0752-109265
  0714-111058
  0654-938976
   
 15. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #1494
  Dec 12, 2017
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,338
  Likes Received: 8,169
  Trophy Points: 280
 16. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #1495
  Dec 18, 2017
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,338
  Likes Received: 8,169
  Trophy Points: 280
  MWONGOZI WA UFUGAJI WA KUKU BORA WA MAYAI

  SIKU YA 1-5

  Wape Glucose na mchanganyiko mmojawapo kati yah ii ifuatayo;

  · Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin

  · Fluban na vitamin kama vile aninovit au supervit au vitalyte  CHAKULA

  Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis. Baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wanapoanza kutaga mayai.

  SIKU YA 6

  Wape vitamin ambayo ni vitastress

  SIKU YA 7

  Chanjo ya Newcastle masaa mawili tu. Weka maji ya vitamin(vitastress) mara baada ya kutoa maji ya chanjo

  WIKI YA PILI

  Chanjo ya gumboro masaa mawili tu. Halafu endelea na maji ya vitamini (vitastress)

  WIKI YA TATU

  Wape doxycol au otc 20% au anflox gold au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

  WIKI YA NNE

  Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress)

  WIKI YA TANO

  Hakikisha kuku wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress)

  WIKI YA SITA

  Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni  WIKI YA NANE

  · Wape kuku chanjo ya ndui

  · Dawa ya minyoo (piperazine au levamisole)

  · Vitamin (supervit layers)

  · Walishe grower mash hadi miezi 3 na nusu na tumia layer mash wakifika miezi 4 kamili

  · Pia hakikisha wanapata chakula chenye ridocox hadi wanapoanza kutaga, pia kumbuka kuwapa majani

  WIKI YA KUMI NA MBILI

  Chanjo dhidi ya Newcastle ( rudia kila baada ya miezi mitatu) kwa masaa mawili kasha wape maji ya vitamin

  WIKI YA KUMI NA SITA

  Kata midomo kisha wape neoxyvital kwa siku 3-5 na pia anza kuandaa viota kwa ajili ya kutagia mayai

  WIKI YA AROBAINI NA NANE

  Wape virutubisho vyenye kuongeza wingi wa mayai kama vile G.L.P (kilo moja kwa kila 50 za chakula wiki ya kwanza na nusu kilo kwa wiki zinazofuata) na vitamin

  WIKI YA HAMSINI NA MBILI

  Chagua kuku wasio na dalili za kutaga kabisa, wenye magonjwa sugu na wenye tabia zisizofaa wauze ili kupunguza gharama

  WIKI YA SABINI NA MBILI

  Tumia V-RID kusafisha mabanda ili kuua vijidudu. Pia weka maji ya dawa hii kwenye kusafisha miguu (footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (biosecurity) na kwamba vifaranga wanowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo kwa lengo la kuepuka magonjwa

  WIKI YA TISINI NA SITA

  Ondoa kuku wote waliozeeka kwa ajili ya batch mpya ya vifaranga

  HITIMISHO

  Kwa maswali na maelekezo zaidi usisite kuwasiliana name kwa maelezo zaidi

  Imeandaliwa na Doctor of veterinary medicine

  Phone: 0712784472

  theriogenology
   
 17. Mpare wa Mtwara

  Mpare wa Mtwara Member

  #1496
  Jan 8, 2018
  Joined: Jan 7, 2018
  Messages: 52
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 25
  Habari zenu wakuu,
  Kama title inavyojieleza, nataka kujua ni nini au vitu gani vya kuzingatia kabla na nitakapoanza kufuga kuku wa mayai, KIBIASHARA
   
 18. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #1497
  Jan 8, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,338
  Likes Received: 8,169
  Trophy Points: 280
  Una mpango wa kuanza na kuku wangapi?
   
 19. Helicobacter pylori

  Helicobacter pylori JF-Expert Member

  #1498
  Jan 8, 2018
  Joined: Feb 15, 2013
  Messages: 353
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  1. Aina ya kuku wa mayai uanaitaji (wapi utawapata, na wakiwa na Umri gani (wa siku moja au mwezi nk))
  2. Idadi ya kuku unataka kufuga
  3. Wapi Utawafugia (eneo)
  4. Upatikanaji wa Chakula kwa Muda wote kabla na miezi michache baada ya kuanza kutaga.
  5. Fedha kwa ajili ya kuendesha mradi wako (bajeti)
  6. Mfanyakazi
  8. Soko unalolenga ni lipi na umbali kutoka unapofugia
  9. Wapi utapata huduma za kitaamu
  10. Usalama wa kuku.

  Nk.
   
 20. A

  Andiet New Member

  #1499
  Jan 11, 2018
  Joined: Aug 16, 2017
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Natafuta soko la kuku wa mayai ninao kama 500 hivi
  Nichek kwa 0713700066
   
 21. Lukwafya bhagasi

  Lukwafya bhagasi JF-Expert Member

  #1500
  Jan 14, 2018
  Joined: Oct 21, 2017
  Messages: 1,260
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Naomba kuunganishwa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...