Hawa kuku wa kisasa mwenzenu kuwala naogopa kuwafuga mie nitaweza?
FL usiogope utaweza tu, yaani mie ninawafuga muda tu, ila inataka moyo usile hela ya chakula chao na dawa, pia usiwe mtu mkarimu sana, uwachukulie kama biashara na sio chakula: kila mgeni akija apikiwe, unaingia bandani na kumfungia mwingine akapike kwake! hapo faida hamna kabisa!
Unajua kuna wengine wala hatauwali sana ila tunawafuga ni business, kuna watu hawali uyoga lakini wanalima, hii ni biashara.
Mie kwakweli hawa wa kienyeji ndio huwa nawaona kama pets kiasi unakuwa mmeishamzoea sana hata kumchinja mnamuonea huruma, kama ni watoto wanaweza lia kabisa!