Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mkuu hakuna njia yoyote ya kuifadhi hizo dawa zaidi ya kuweka kwenye friji?Hasa kwa wale ambao wanaishi vijijini au mbali na miundo mbinu ya umeme.

Mheshimiwa Blacktiger, hakuna njia nyingine ya kuhifadhi chanjo isipokuwa kwenye JOKOFU ndio maana tunashauri kwa watu wa vijijini wakanunue chanjo pale wanapohitaji kuitumia.Itabebwa kwenye coolbox au chupa iliyowekwa barafu kwa ajili ya kutunza ubaridi. Coolbox iliyojazwa barafu zilizoganda vyema ina uwezo wa kutunza dawa kwa saa 24. Kama ni mfugaji ni muhimu kuwa na coolbox,huziuzwi ghali. Chanjo kama hazitahifadhiwa kwenye friji au zitasafirishwa nje ya Jokofu zinaharibika.
 
Mheshimiwa Blacktiger,hakuna njia nyingine ya kuhifadhi chanjo isipokuwa kwenye JOKOFU ndio maana tunashauri kwa watu wa vijijini wakanunue chanjo pale wanapohitaji kuitumia.Itabebwa kwenye coolbox au chupa iliyowekwa barafu kwa ajili ya kutunza ubaridi. Coolbox iliyojazwa barafu zilizoganda vyema ina uwezo wa kutunza dawa kwa saa 24. Kama ni mfugaji ni muhimu kuwa na coolbox, huziuzwi ghali. Chanjo kama hazitahifadhiwa kwenye friji au zitasafirishwa nje ya Jokofu zinaharibika.

Mkuu kwani ni Madawa/Chanjo za ugonjwa ngapi ambazo zinatakiwa kuwa kwenye jokofu, ni aina yote ya magonjwa ya kuku au zingine ni dawa tu za kawaida.

Na vipi kuhusu Dawa za Mitishamba? make nasikia kuna dawa za miti shamba nazo huwa ni nzuri sana kwa kutibu kuku,
 
Na vifaranga wanaweza safiri umbali gani bila kula? Mfano unawatoa Dar hadi Mwanza kwa basi, inawezekana? au ni lazima mtu awe na chakula cha kuwalisha njiani?
 
Mkuu kwani ni Madawa/Chanjo za ugonjwa ngapi ambazo zinatakiwa kuwa kwenye jokofu, ni aina yote ya magonjwa ya kuku au zingine ni dawa tu za kawaida,

Na vipi kuhusu Dawa za Mitishamba? make nasikia kuna dawa za miti shamba nazo huwa ni nzuri sana kwa kutibu kuku,
Ni chanjo ndizo zinazotakiwa zikae kwenye Jokofu na wala sio dawa za kawaida.Kuhusu dawa za kienyeji nasikia hivyo kuwa zipo ila mimi nashauri iwe altenative ya mwisho kabisa kutumia,vinginevyo kama una access na dawa dukani tumia za dukani.Hata binaadam kwanza huenda hospital akishindwa huko hutafuta mbadala,hata kwa wanyama kama itakuwa hivyo itapendeze.
 
Mkuu kwani ni Madawa/Chanjo za ugonjwa ngapi ambazo zinatakiwa kuwa kwenye jokofu, ni aina yote ya magonjwa ya kuku au zingine ni dawa tu za kawaida,

Na vipi kuhusu Dawa za Mitishamba? make nasikia kuna dawa za miti shamba nazo huwa ni nzuri sana kwa kutibu kuku,
Ni chanjo tu na wala si dawa nyingine.Kuhusu dawa za kienyeji hata mimi nasikia kuwa zipo ila sijawahi kutumia.Ushauri wangu kama unahitaji kutumia dawa hizo iwe ni last altenative,vinginevyo kama una access na dawa za dukani tumia hizo. Hata binadamu akiumwa kwanza ataenda hospital akishindwa huko kupata ufumbuzi wa matatizo yake atafuta mbadala.
 
Na vifaranga wanaweza safiri umbali gani bila kula? Mfano unawatoa Dar hadi Mwanza kwa basi, inawezekana? au ni lazima mtu awe na chakula cha kuwalisha njiani?
Vifaranga wana uwezo wa kukaa siku tatu bila kula toka wazaliwe. Muhimu wasionje chakula kabisa. Kwa mantiki hiyo, ukisafirisha vifaranga kuelekea Mwanza wanafika bila wasiwasi.
 
Vizuri sana, na Vipi wakisha safiri Umabali huo Bila kula, wakishafika wapewe Huduma gani ya kwanza kabla ya kuanza kuwapa chakula chao?
 
Mkuu glucose hii ya binadamu? na hao vifaranga si wanakuwa ni wageni kwenye maswala ya misosi vipi wataweza kuyanywa? Mkuu usichoke na maswali
 
Mkuu glucose hii ya binadamu? na hao vifaranga si wanakuwa ni wageni kwenye maswala ya misosi vipi wataweza kuyanywa? Mkuu usichoke na maswali

Mkuu mimi sio Mtaalamu kama Kichwa Mbovu ila nina uzoefu wa kuwapa Glucose vifaranga kabla ya kuwapa chakula ukiwaingiza bandani tu kitu cha kwanza ni maji yenye glucose kabla ya msosi ni hii hii glucose ya kawaida Ndugu Mtaalamu ataelezea zaidi
 
Na vifaranga wanaweza safiri umbali gani bila kula? Mfano unawatoa Dar hadi Mwanza kwa basi, inawezekana? au ni lazima mtu awe na chakula cha kuwalisha njiani?

mkuu Chasha

Noamba uniwekee ile database ya ufugaji wa Kuku uliiweka hapa jamvini. Ikionyesha matumizi, chakula na mahitaji mengine.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mimi sio Mtaalamu kama Kichwa Mbovu ila nina uzoefu wa kuwapa Glucose vifaranga kabla ya kuwapa chakula ukiwaingiza bandani tu kitu cha kwanza ni maji yenye glucose kabla ya msosi ni hii hii glucose ya kawaida Ndugu Mtaalamu ataelezea zaidi

Freshi mkuu, nimekupata kabisa,
 
Mkuu glucose hii ya binadamu? na hao vifaranga si wanakuwa ni wageni kwenye maswala ya misosi vipi wataweza kuyanywa? Mkuu usichoke na maswali

Mheshimiwa sabayi yuko sahihi kabisa,ni hii hii glucose ya kawaida ambayo binadamu wanaitumia. Kuhusu ugeni wao kwao si shida hivi vitu huenda automatic, hujifundisha mwenyewe kula na kunywa maji.

Kitu cha msingi zile siku 3 za mwanzo watandikie Magazeti juu ya maranda. Magazeti huwasaidia vifaranga kujifunza kula kirahisi kwani sauti inayotoka kufuatia wao wenyewe kutembea huwafanya wahisi kama wako na mama yao anawafundisha kula na hapo ndipo wanapoanza na wao kudonoa chini ili wasikie ile sauti.
 
Mheshimiwa sabayi yuko sahihi kabisa,ni hii hii glucose ya kawaida ambayo binadamu wanaitumia.Kuhusu ugeni wao kwao si shida hivi vitu huenda automatic,hujifundisha mwenyewe kula na kunywa maji.Kitu cha msingi zile siku 3 za mwanzo watandikie Magazeti juu ya maranda.Magazeti huwasaidia vifaranga kujifunza kula kirahisi kwani sauti inayotoka kufuatia wao wenyewe kutembea huwafanya wahisi kama wako na mama yao anawafundisha kula na hapo ndipo wanapoanza na wao kudonia chini ili wasikie ile sauti.

Mkuu that's funny tulikuwa tunatandika Magazeti na kumwaga chakula chini ila tulikuwa tunafanya kwa mazoea tu/Kuiga bila kujua logic yake leo ndo najua kuwa eti huwa wanafeel wapo na mama yao, that's good tunaanza kuelewa maana ya tunachofanya sasa.
 
Mkuu Kichwa vipi kuhusu Chakula cha Kuku hao Chotara na wakienyeji na lazima kiwe Pure na cha hawa kuku wa kisasa? na kwenye kutamisha mayai ukitumia ile njia ya Kuchagua sex ya mayai unaweza fanikiwa kutotoresha Majogoo tupu au Majike tupu?
 
Mkuu hizi mashine za kutumia Mafuta ya Taa ni pasua kichwa unaweza ukafa kwa presha, Tatizo ni kwamba watengenezaji wa hizo mashine hawajawekeza vya kutosha kwenye utafiti wao wako bise na pesa tu, Bado za Umeme ndo solution ingawa China unaweza pata za kutumia Umeme na Gesi yaani inaweza endeshwa kwa gesi endapo umeme haupo na vilevile zipo za kuweza kutunza moto kwa masaa zaidi ya 9,

Chasha asante sana kwa ushauri wako, ukiwakuta hao watengenezaji wa kibongo jinsi wanavyozifagilia nane nane utasema nimepata.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom