Kwa wafanyabiashara wa Tanzania, hii ni fursa pekee kwenu. Itumike ipasavyo haraka

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,275
2,000
USHAURI KWA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA

Tangu jana Juni 5/2017 nchi za Saudia, Emirate, Bahrain, Misri, Yemen, Libya na Maldives zimeingia mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya Qatar. Mgogoro huo unatokana na tofauti za kiitikadi na siasa za ndani (chamngamoto za ndani za kidemokrasia) baina ya mataifa hayo na nchi ya Qatar.

Nchi hizo zimefunga mipaka (anga, maji na nchi kavu) pamoja na kusimamisha mahusiano ya kibiashara na nchi ya Qatar. Mashirika ya ndege ya Egypt Air, Saudi Airways na Emirate (Etihad) yamezuiliwa kutua nchini Qatar. Aidha, Qatar Airways imezuiwa kuruka/kupitia katika anga za nchi hizo.

Nchi ya Qatar ninaifahamu vizuri. Mara kadhaa [kwa muda mrefu, kipindi kabla ya miaka mitatu iliyopita] nilikuwa nikitembelea nchi ya Qatar. Ni taifa dogo ambalo sehemu kubwa ya nchi ni jangwa/mchanga, lakini ni nchi tajiri na watawala wake ni progressive ikilinganishwa na tawala nyingine za kifalme za Saudia, Bahrain au mataifa mengine ya Ghuba na Uarabuni kwa ujumla.

Takwimu za ulaji (consumption indices) zinaonesha kuwa asilimia tisini (90%) ya maisha ya kila siku ya wa-Qatari (wananchi wa Qatar) hutegemea vyakula na bidhaa nyingine vinavyoingizwa nchini humo kila siku kutoka nje (imports). Ikizingatiwa kuwa kwa sasa ni kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislam, ni dhahiri kuwa hatua zilizochukuliwa [dhidi ya Qatar] na mataifa hayo yakiongozwa na Saudia ni strategically timed.

Pengine kuwa Waqatari wakikosa chakula katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, itakuwa rahisi kuwachochea dhidi ya watawala wa nchi yao. Hata hivyo waswahili husema, ;kufa kufaana’. Tayari nchi ya Uturuki imetangaza kuanzia leo kupeleka ndege za shehena za vyakula.

WAFANYABIASHARA WA TANZANIA

Ujumbe huu ni mahsusi; nimekuandikieni wafanyabiashara wa Tanzania kuona, kutambua na kisha kuchukua hatua za haraka kuitikia fursa iliyojitokeza. Fanyeni tathmini ya soko la Qatar haraka na kisha kupeleka bidhaa [hususan chakula] sokoni nchini Qatar. Tumemieni ubalozi wao uliopo hapa nchini kutambua aina na viwango/kiasi cha bidhaa zinazotakiwa nchini humo.

Ingawa Tanzania peke yake kwa sasa haiwezi kupata bidhaa zote zinazohitajika kutosheleza soko la walaji wa Qatar, hata hivyo, angalau wafanyabiashara wa Tanzania wataweza kupata, kupeleka na kuuza vyakula anuwai ikiwa ni pamoja na nyama, samaki, vitunguu, iriki, mdarasini, ngano, mahindi, mchele, mafuta ya halizeti, maharage, mboga mboga na bidhaa nyinginezo.

Changamkeni, muda ndio huu, kwa kuwa Internet ipo, mabenki yapo, meli zipo, Qatar Airways inakuja na kuondoka hapa nchini mara mbili kila siku [asubuhi na jioni/pengine biashara ikiongezeka itaongeza cargo flight], na washauri wa masuala ya biashara za kimataifa na uchumi wapo.

Huo ndio mchango pekee ninaoweza kuutoa kwa sasa.

Haya twende kazini.
 
Oxx

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
730
1,000
Jambo jema na zuri sana.....

Hawa wametengwa na wenzao kwa sababu za kufadhil ugaidi, sasa kufungua mahusiana nao na kupeleka kile kilichowekewa vikwazo na wenzao itakua imekaa vipi kidiplomasia.......?
 
cerengeti

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,884

Safi saana
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,419
2,000
Good Idea,kama vipi jukwaa letu la matangazo na biashara litumike kuwahamasisha wadau.
Hasa hasa wale wa vikundi vya kinamama na wazalishaji wa mashambani.
Tumwomba pia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kupitia foundation yake kuona kama kuna uwezekano wa fursa hizi kwa kuanzia.
(Diplomatic cover).
Kwani tunaweza anza bila utaratibu wa kidiplomasia mwisho wake na sisi tukaingizwa kwenye urodha ya nchi zinazowasaidia magaidi.
Mkulima wetu mahili Mh.Jakaya Kikwete tunakuomba utoa neno hapa,fursa hizi watanzania tuzichangamkie.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom