(Kwa wadada wenye ndoa) Utii kwa waume zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(Kwa wadada wenye ndoa) Utii kwa waume zetu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lolyz, May 22, 2012.

 1. lolyz

  lolyz JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ……Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wapombe; bali waonyeshe mfano mwema. [SUP]4 [/SUP]Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda waume zaona watoto wao [SUP]5 [/SUP]nakuwa wenye kiasi na safi, wakitumia wakati wao kushughulika nyumbani mwao. Wawewema na watii kwa waume zao, ili neno la Mungu lisije likadharauliwa kwa ajili yao
  Mama mkwe wake alikuwa mfano mzuri mtiifu mbele za Mungu na kwamumewe,walidumu kwenye ndoa kwa miaka 60,na alikufa akiwa na miaka 83.
  Kwa kipindi kisichopungua miaka 17 ya ndoa yao baba aliuguamaradhi ya ubongo yaliyoharibu ubongo wake kabla hajafanyiwa upasuaji.Baada yaupasuaji alikuwa kama mtoto mdogo asiyejiweza kwa chochote na alihitajiuangalizi muda wote.

  Kwa miaka 17,mama alienda kila siku kumuona siku sita kwawiki,alikubali kutokwenda jumapili tu baada ya watoto wake kumlazimishaapumzike japo siku moja kwa wiki.Hakuweza hata kusafiri kwa kipindi chote hicho,alimpendasana baba zaidi tunavyoweza kuelezea,na alikuwa mtiifu na mwaminifu hadi kwamumewe hadi kifo chake.

  She was a model and example of faithfulness.
  What are the secrets to stick with your man?
  .kuweka ahadi ya kiapo chenu cha ndoa
  .Kwa msaada wa Mungu
  .Total commitment

  Kwa upande wangu in my marriage there has been rough timesduring our 5yrs of marriage but now we are both very strong and independent.Munguamenifundisha kwa neno lake TITO 2:5 kwenye mawazo yangu siku moja baada yakumpa maisha yangu ayatawale

  Wawe wema na watii kwa waume zao, ili neno la Mungulisije likadharauliwa kwa ajili yao;

  Neno hili limenisaidia sana kugundua sauti ya adui na uongowake.sifikirii tena wala sina mawazo ya kumuacha mume wangu kwa kosa lolote.kwakuwa namuheshimu Mungu na kumpenda na singependa kulitukanisha jina lake kwa kiaponilichoweka ktk nyumba yake kwa kutotii kwangu agizo lake.Mungu ametusaidiakuchukuliana kwa upendo na uaminifu to each other.

  Her mother inlaw set an example of “sticking with your man”to all womeneven you can also do it

  Baba; ulianzisha familia.Asante kwa kuwa utatupatia mahitaji yotetunayohitaji tunapaswa kuwa watii kwa waume zetu.Uliahidi kuwa hakuna jaribulisilokuwa na mlango wa kutokea na utatushindia yote daima.Umekuwa mwaminifukwa neno lako siku zote.Asante baba…Amen
   
 2. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Asante sana kwa neno la uzima kwa wanandoa
   
 3. wasaimon

  wasaimon R I P

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Barikiwa sna...somo zuri na linabariki pia.
  Amen
   
 4. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe 100%
   
 5. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nondo si kwa wanamama tu hata waume wote ingekuwa hivi basi ndoa nyingi sana zingesalimika. Asante mdau kwa chakula ulichotulisha leo na ubarikiwe
   
 6. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadada mpooo?mbona hatuoni mkitia maneno yenu yale?au hamjaolewa nini?
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  nani anataka kujifunga kitanzi?

   
 8. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kongosho;SO FAR MI NNACHOJUA NDOA NI NJEMA NA NI JAMBO JEMA KUFUNGA NDOA TATIZO SHETANI AMEDANGANYA WENGI KWA KASI ALIYOIANZISHA YA KUVURUGA WANANDOA HEBU CHUKULIA MFANO WA POST..KWELI NI WACHACHE SANA WANAOHESHIMU VIAPO WALIVYOKULA MBELE YA HADHARA..SHETANI AMEWAFANYA WASAHAU NA KUWAONDOLEA HOFU YA KIMUNGU.ILA KILA MTU AKIJIHESHIMU ASIKWAMBIE MTU HAMNA RAHA DUNIANI KUIPITA NDOA TAKATATFU WEWE
   
 9. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  heheh..............ngoja waje kina Cantalisia, FirstLady1, BADILI TABIA.......... etc.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana mtoa mada kwa maneno mazuri yenye hekima na upendo,nami sitasita kuongezea hapo kidogo..
  Mwenyezi mungu atuwezeshe katika haya


  1. Imani
  Mithali 31:26, 29, 30Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi 119;15
  ******************

  2. NdoaMithali 31:11-12, 23, 28Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3
  *********************

  3.MaleziMithali 31: 26, 28Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea. Mithali 22:6
  *************

  4. HudumaMithali 31:12-15, 17, 20Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.
  ***************

  5. MaliMithali 31:14, 16, 18Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23
  ******************

  6. NyumbaMithali 31:15, 20-22, 27Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2
  ********************


  7. MudaMithali 31:13, 19, 27Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha anakamilisha kazi zake za kila siku. Kamwe hapotezi muda katika kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu na yasiyo na faida.
  ******************

  8. Uzuri / UremboMithali 31:10, 21-22, 24Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri wa ndani unatoka kwa Yesu Kristo. Anatumia ubunifu wake na utanashati wake kuleta uzuri katika maisha yake na ya watu wake.
  Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe kweli tunamjua na kumwamini yeye.

  ************************************************************
   
 11. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Amina kubwaa......maana kulitimiza hilo neno yahitaji nguvu za kutosha!!

  Namsubiri na gfsonwin. RussianRoulette waje waongeze michango yao!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante mwaya,
  Mie nakubaliana kbs na wewe pamoja na FirstLady1,
  Japo kwa kizazi chetu cha do.com hili some ni gumu kwa wengi wetu kulitekeleza kwa vitendo,
  Ila huo ndio ukweli na ndivo inatupasa kuwa na kuacha mambo ya kidot com ya kutafuta usawa ambao kamwe haitatokea tukaupata,cha msingi ni kuwaheshim,kuwapenda na kubebeana mapungufu yetu na waume zetu,

  Nashukuru mme wangu Rejao anipa sapoti ya kutosha kuimarisha ndoa yetu na hakika tunabebeana mapungufu yetu na hatuna mpango wa kuachana japo wavimba macho wengi wanajitahidi kutusambatarisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,357
  Likes Received: 6,539
  Trophy Points: 280
  A good example is my Mom i really admire and love her, she did quit her very good job to take care of us..we are seven..and all successfull, it all comes to commitment and dedication..we love you MOM..
   
 14. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Una utani na wanaharakati wewe.Thanks though!
   
 15. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe mtoa mada naFirst lady
   
 16. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante SANA kwa kuniita dear Kipipi. Binafsi naamini kua Bibilia ina maneno mengi yenye busara ila sisi binadamu ndio tunachagua na kuyapa tafsiri inayo turidhisha hadi maneno yaonekane hayana maana (sometimes). Kila tunapo soma mistari ya Mungu, Tumuombe atupe mwangaza wa kuyaelewa haya maneno kama alivo taka tuyaelewe.

  Mwanzo wa kila kitu ni upendo. Ikiwa ndoa ina upendo ndani yake hayo yote yanatiririka tu yenyewe, huhitaji manual kukukumbusha. Ila ndoa ikikosa upendo, mume akiwa mnyanyasaji au mke akiwa mnafiki (anae-fake upendo kwa mume wake) hata mke akifanya hayo yote ni bure sababu hayatokei moyoni mwake, ni unafiki mtupu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. lolyz

  lolyz JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Cantalisia,Ni kweli wengi wetu tunaweza kufikiri kuwa bible ni ngumu na haieleweki au haiko applicable...lakini ukweli ni kwamba kwa maisha ya sasa ndoa nyingi zinaparanganyika ..sasa utaiokoaje ndoa yako bila kumkosea Mungu?ndipo hapo ukibahatika kuikumbuka unaikimbilia.kiukweli neno na ahadi zilizomo mle hazijawahi kudanganya ikiwa utaamini bila shaka ndipo inakuwa nyepesi zaidi. inatubidi wale ambao ni waamini tuwahimize wenzetu ni jinsi gani mtu unaweza kujitetea dhidi ya huyu adui kabla hujaenda kuombewa nje na watumishi.
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Asante sana mtoa mada, pia FirstLady1 nashukuru sana na ubarikiwe mno kwa haya. Kipipi nakushukuru sana kwa kuniita ili na mimi nitie langu japo dogo lakin litaongeza maarifa.

  Kwanza kabisa ikumbukwe kuwa ndoa ni sehem ya ibada ambayo mtu anaweza kuitimiza akiwa hapa dunian. Tena Mungu aliiweka hii ndoa kuwa kitu kitakatifu sana ambacho kwa mapenzi yake mema alifanya ndoa kuwa chombo cha kufanya kazi ya uumbaji. Nafikiri kama watu wote wangepata kujua kuwa ndoa kama ilivyo Mungu kaifanya kuwakilisha utukufu wa Mungu duniani kwa kuruhusu tendo la ndoa kutumika kuumba kama alivyoumba yeye.

  Sasa kwa kuyajua hayo yampasa mwanamke kuwa mwenye upole na upendo, anayeamka asubuhi kabla hakuja pambazuka na kuanza kuzipanga kazi za nyumbani kwake. Awe ni mtu anayelisha watu wake bila kunung'unika, awe ni mtu anayewavesha watu nyumbani kwakei. awe hodari katika kazi zote za mikono na apende kumtunza mumewe kwa uaminifu na mumewe huyu ajulikane aketipo barazani na wenzie. awe ni mtu mtu ambaye moyo wa mumewe humwamini na kamwe hatakosa mapato ya mikono yake.

  BABA yampasa kuwa mtu anayeipenda familia yake, awe tayari kuihudumia pasipo kuchoka, apende kuona watu wa nyumbani kwake wanafuraha na amani muda wote. Tena asiwe mlevi, wa mtu wa kuhadaiwa na mwanamke malaya, atamani sikuzote kuona mkewe na watoto wanastawi.
  MziziMkavu Asprin, Nyaningabu, Mr Rocky nk mnayatimiza hayo kwa familia zenu? mko responsible juu ya wake na watoto wenu wanakula nini wana lala wapi na wanaish vipi? hizi ndizo quality za baba bora. jitahmin mtuambie kama ninyi ni akina baba bora au ni bora baba. Tena mtuletee jibu hapa.
  Tena ikumbukwe upendeleo hudanganya kuwaandalia watu wa nyumbani kwake
   
 19. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  upendo ni KUTIIANA. unitii na mimi nikutii!

   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin mke wangu na Watoto wangu ni kitu muhimu sana katika maisha yangu hio kwangu halina matatizo nawaangalia sana familia yangu.
   
Loading...