Kwa Wachina, Nyerere ni mtume kama alivyo muasisi wa taifa la CHINA, Mao Tse-tung

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
[h=1]Kudorora Reli ya TAZARA[/h] Felix Mwakyembe


Mbeya


tazara222.jpg



JIANG Jing Ying, mmoja wa raia wa China walioshiriki ujenzi wa reli ya TAZARA


Mchina ashangaa, ahoji hivi hakuna Nyerere?
Ni kati ya wajenzi reli TAZARA, asema kwao China Nyerere ni mtume
Ashangaa vibarua wa enzi hizo za ujenzi wakiteseka kimaslahi


JIANG Jing Ying, mmoja wa raia wa China walioshiriki ujenzi wa reli ya TAZARA, alijikuta akibubujikwa machozi baada ya kuiona hali ya reli hiyo ilivyo hivi sasa, pamoja na wastaafu wenzie aliofanya nao kazi wakati huo.
Jiang alifika kituo cha TAZARA, Iyunga Mbeya hivi karibuni. Pamoja na kushuhudia hali ya shirika hilo ilivyo sasa, pia alikutana na wafanyakazi Watanzania aliofanya nao kazi wakati huo, uduni wa maisha ya wastaafu hao na uchakavu wa shirika hilo kulimfanya Mchina huyo kutokwa machozi.
Alipokutana na baadhi ya wastaafu hao wenzake pale Iyunga, Jiang alitokwa machozi na hali duni alizowakutana nazo wakiwa wamechoka na hawana msaada wowote pamoja na mchango wao mkubwa kwa taifa, hususan ujenzi wa reli hiyo muhimu.
Wakati akiendela kuhuzunika na hali duni za wastaafu wenzake, alijikuta akiumia tena kuona jinsi reli ya TAZARA waliyoijenga kwa taabu na shida nyingi ikiwa taabani, kwani ni katika kipindi hicho alichofika kituoni hapo Iyunga, treni ilikuwa imesitisha safari zake kwa muda kutokana na ukosefu wa mafuta.
Katikati ya simanzi, Mchina huyo alijikuta akijiuliza; “Hivi hakuna Nyerere, na Tanzania haipo?”
Katika mahojiano yake na gazeti hili la Raia Mwema jijini Mbeya hivi karibuni, Jiang anamzungumzia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa hisia kali huku akionyesha mshangao wake kwa jinsi Tanzania inavyomuenzi muasisi huyo wa taifa.
Jiang alifika nchini kwa mara ya kwanza mwaka 1969, akiwa miongoni mwa Wachina waliokuja nchini kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Uhuru, sasa maarufu kama TAZARA (Tanzania Zambia Railway Authority) na aliondoka mara baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, mwaka 1973.
Mshangao wa Mchina huyo unatokana na jinsi Watanzania wanavyomuenzi muasisi wa taifa lao, kwamba haoni hapa nchini Nyerere akienziwa kwa vitendo, anaamini amesahaulika na kinachofanyika ni maneno tu.
Anasema kwa Wachina, Nyerere ni mtume kama alivyo muasisi wa taifa lao, Mao Tse-tung na anapomkumbuka hutokwa machozi na ndipo anapohoji akisema; “Wachina wanampenda Nyerere, Tanzania kuna tatizo gani? Mimi natembea na picha ya Nyerere.”
Mbali na picha anazotembea nazo, Mchina huyo hubeba chochote anachokiona chenye picha au jina la Mwalimu Nyerere. Na hata alipokuwa kwenye ofisi za Raia Mwema jijini Mbeya, aliondoka na toleo maalumu la miaka 50 ya Uhuru, ikiwa ni baada ya kuona habari kuu iliyosomeka; “Nani kama Nyerere,” huku kukiwa na picha yake kubwa pembeni.
Kuona jina na picha tu, alichekelea na kulichukua gazeti hilo akisema; “Rafiki hii Nyerere, nachukua mimi, naenda nayo, sawa!”
Kwa mujibu wa Jiang, Wachina wanamini kuwa reli ya TAZARA ni daraja la uhusiano baina ya nchi mbili hizi (Tanzania na Zambia) na katika kudhihirisha hivyo, anabainisha kwamba kila Mchina anayekuja hapa nchini huitembelea reli hiyo kwani wanaamini urafiki ulioasisiwa na waasisi wa mataifa haya mawili ni wa kudumu hivyo wasingependa kuona unakufa.
Mbali na reli hiyo, kikubwa kinachowaunganisha Wachina na Tanzania, ni msimamo wa Mwalimu Nyerere kuiunga mkono China katika Umoja wa Mataifa na anatoa mfano wa mgogoro wa nchi hiyo na Marekani kuhusu Taiwan, akisema Nyerere hakujali hata mabavu ya taifa hilo kubwa duniani, akaipigania China ambayo wakati huo haikuwa na uwezo mkubwa ikilinganishwa na Marekani, ni kumbukumbu inayodumu katika mioyo ya Wachina.
“Nyerere alijua kuhudumia watu wake, marafiki zake tunaamini Nyerere bado yupo, anaishi kutokana na matendo yake aliyoyafanya akiwa hai, alijenga daraja la urafiki kati ya Tanzania na China,” anasema Jiang.
Anasema, wao (Wachina) wanaamini kuwa urafiki wa nchi mbili hizi ni wa milele, na ni kutokana na imani yao hiyo wanasikitishwa zaidi na kulegalega kwa TAZARA, na kinachowasikitisha zaidi ni wao wakati ule kutokuona mbali, kwamba iwapo wangeona mbali zaidi basi wasingeondoka kabisa na kuisahau TAZARA.
Hivi sasa wanauona umuhimu wa Serikali ya China wakati ule kuweka utaratibu ambao ungehakikisha wanaendelea kuwepo kuihudumia TAZARA, kwamba haikuwepo sababu ya msingi ya kuitelekeza reli hiyo wanayoamini kuwa ndicho kielelezo cha kudumu cha urafiki kati ya nchi mbili hizi.
Pamoja na kuitazama TAZARA kama daraja la urafiki kati ya nchi mbili hizi, Jiang anasema reli hiyo ina umuhimu mkubwa zaidi katika kuchangia uchumi wa Tanzania, kwa msingi kwamba ni rahisi, inadumu na inasafirisha abiria na mizigo kwa wingi na uzito mkubwa zaidi, sifa ambazo kwa barabara haiwezekani.
“Reli inaokoa gharama, tofauti na barabara ambazo matengenezo yake ni ya muda wote na gharama,” anasema mjenzi huyo wa TAZARA.
Mjenzi huyo wa TAZARA, bado anauona umuhimu wa serikali yake kurudi nchini na kuimarisha reli hiyo, hatua anayosema itaisaidia zaidi Tanzania kutokana na nafasi ya reli katika ujenzi wa uchumi wa taifa lolote duniani.
Hatua ya kuimarisha reli hiyo itaokoa fedha nyingi zinazotumika katika ujenzi na matengenezo ya barabara hivyo kuzielekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo huku reli ikitoa mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa.
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Jiang hivi sasa yupo katika harakati za kuweka kumbukumbu za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere nchini ambazo anazitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa sanamu za shaba na ukumbi (Mwalimu Nyerere Memorial Hall).
Wanamtambua Mwalimu Nyerere kama mmoja wa waasisi wa vuguvugu la ukombozi wa Bara la Afrika na kwamba anaheshimika duniani kote kwa hilo.
Katika mkakati huo wa kuendelea kumkumbuka muasisi huyo wa taifa la Tanzania, Mchina huyo kupitia umoja waliouanzisha wa kudumisha urafiki baina ya mataifa haya mawili (SINOTA), walitengeneza beji 10,000 za mwalimu ambazo wamekuwa wakizigawa kwa watu na taasisi mbalimbali hapa nchini.
Anataja lengo kuu ya kumbukumbu hizo, sanamu, ukumbi na beji kuwa ni kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere na kurithisha mawazo yake vizazi hadi vizazi viweze kuendelea kumkumbuka.
Hata hivyo, kufanikiwa kwa mkakati huo itategemea kwa kiasi kikubwa na utayari wa serikali ya Tanzania, ikizingatiwa kwamba wamelenga kuweka sanamu hizo katika kila mkoa, lakini kwa kuanzia anapendekeza Dar es Salaam na Mbeya.
Jiang alirudi nchini mwaka 2,000, ikiwa ni miaka 27 tangu arudi kwao na safari yake ya sasa ni ya kibiashara zaidi. Alikuja kwa lengo la kuendesha biashara ya pikipiki, akiamini kuwa hali ya uhusiano iliendelea kuwa ile ile ya wakati wa Nyerere na Mao.
Hata hivyo, katika safari yake hiyo ya kibiashara alibaini kuwapo kwa nyufa katika uhusiano wa nchi mbili hizi ambazo, wao, wanaamini uhusiano wake ni wa milele na ndipo alipokuja na wazo la kuanzishwa kwa Umoja wa Urafiki wa China na Tanzania (SINOTA), uliosajiliwa rasmi Februari 26, mwaka 2007, lengo kuu likiwa kuimarisha urafiki uliokuwapo baina ya nchi mbili hizi.
MY TAKE
Lets take trouble kumuenzi mwalimu kwa vitendo kwa kuvienzi alivyovianzisha!
 
Back
Top Bottom