Kwa wabunge wa ccm, chadema na spika wa bunge la jamhuri ya tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wabunge wa ccm, chadema na spika wa bunge la jamhuri ya tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ashakum, May 20, 2012.

 1. a

  ashakum Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ombi kwa wabunge wote makini bungeni wafanye yafuatayo bunge lijalo la Bajeti.

  1. Wajadili kwa kina kuhusu masuala ya profesa Mlacha wa UDOM kwani inaonekana anaendelea kusumbua watumishi na wanafunzi wa chuoni pale. Yeye anafanana sana na Blandina Nyoni wa Wizra ya afya.

  2 Wajadili taarifa ya CAG ya ukaguzi wa UDOM. Inafahamika CAG kuna kitu aligundua pale UDOM, lakini kwa maumbile ya utawala wa nchi hii ni ngumu rais kufanya maamuzi hadi ashauriwe na CC ya CCM.

  3. Bunge tukufu liunde kamati iende ikakague chuoni pale maana taarifa zinaonyesha kuna Umaige na Umkulo sana chuoni pale. Baadhi ya maofisa waandamizi wa chuo kile walihojiwa na tume maadili ya viongozi kwa utajiri usiolingana na mishahara yao, lakini mpaka leo bado wapo kazini.

  4. Kukemea udini unaoendelea kukua chuoni pale, maana watu wananyosheana vidole kwa ukristu wao au kwa uislam wao. Hii ni mbaya sana, nnjini mwetu. Baba wa Taifa hakuwajenga watu kwa misingi hiyo. Udini unakusaidia nini wewe Mkristu au wewe Muislamu? Si mkasome au kufanya kazi kwenye vyuo vya dini zenu kama mnataka kuendekeza libeneke la udini?

  Ili jambo hili liwezekane, wanahitajika wakina John Mnyika, Zito Kabwe, Deo Filikunzombe na Mkosamali walisemee hili bungeni. Lakini linahitaji spika wa bunge aridhie ukaguzi wa kamati ya bunge sio wa CAG kwani Taarifa za kiusalama zinaonyesha CAG ana mahusiano binafsi na Mlacha wa UDOM.

  Aking'olewa Mlacha UDOM kutakuwa na amani ya kudumu.

  Hata kama sio kwa malengo ya kisiasa, basi kwa maslahi ya nchi, Kikwete ng'oa Mlacha pale UDOM. Hana msaada wowote kiutawala wala kwa maslahi ya taifa hili.
   
 2. i

  imamu Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni kama mchawi fulani maana anapigiwa kelele lakini hakuna anayesikia. Dawa yake mwacheni tu aendelee kula nchi bwana.
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm
   
Loading...