Mangi flani hivi
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 2,026
- 3,104
Ambonyi wakuu,
Nichukue fursa hii kuwapa pole na starehe za krismas na pia kuwatakia mwaka mpya Mwema wa 2017 in advance.
Nimeshuka kutoka Mlimani leo na kwa kweli ni lazima niwe na fadhila kwa nilichokiona moshi mjini na migombani kwetu. Hakyanani kaka Mbowe na wenzako mmefanya kazi ya ziada na hakuna haja ya kampeni 2020. Barabara ipo mpaka mlangoni kwa bibi yangu, maji yapo kila nyumba, hospital na zahanati kila kona, Shule ndo tusiseme kwa sababu ni asili yetu. Mungu awabariki sana viongozi wote wa kisiasa mkoani Kilimanjaro na Arusha (japo sitaki zungumzia sana). Kudos mbe kanyi.
Nimefika pale moshi mjini yaani mji wote umeunganishwa kwa Lami, na ukizingatia na usafi wake.... Itoshe kuwasifia kwa leo. Sasa nasemaaa...
Mbowe, Komu, Selasini, mbatia, mbunge wa Siha, na Mbunge wa moshi vijijini(nimesahau majina yenu). Kwa upepo unavyoenda, naomba kwa utashi wenu, muandae na mtuandae kisaikolojia kutengeneza forum maalumu itakayowezesha sisi tunaokaa nje ya Kilimanjaro kuchangia shuguli za maendeleo ili kuwaunga mkono katika harakati zenu. Tunajua kuwa halmashauri zetu hapo Kilimanjaro zinakusanya vizuri na kutumia vizuri ila sisi tuliopo nje ya Mkoa tunaona aibu tunapokuja na kukuta wazee wetu wamefanya mambo ya maana hapo moshi halafu sisi tunachangia maendeleo ya huku porini Ambapo hakuna anayehitaji hivyo michango yetu inaishia midomoni mwa wajanja wachache.
Kwa kweli tunaipenda Kilimanjaro yetu na ni ya kwetu kweli, wabunge wetu na tunatamani kuchangia garama za maendeleo. Hapo ndipo tutatakapozikiwa, ndipo tunaporudishwa tukizidiwa, ndipo tunapokimbilia Kama ya mjini yakitushinda... Sasa Kama hamtushirikishi kwenye kujenga Kili yetu mnataka kutufanyaje???
Mwenyekiti Kaka Mbowe, naomba hiyo forum ifunguliwe haraka.
Angalizo:
Sisi wote ni wa Kilimanjaro, asitokee mjanja akataka kupiga hata kumi ya mtu hapo...hakyanani wachaga hatulogi lakini tutajua la kufanya.