Kwa Waandishi wa Michezo, Kila Kitu Ni Goli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Waandishi wa Michezo, Kila Kitu Ni Goli!

Discussion in 'Sports' started by The Pen, Apr 19, 2012.

 1. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Simba ilisogea jirani zaidi na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania 2012 kwa ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana, huku watetezi Yanga wakilitema rasmi kombe kufuatia kipigo cha pili mfululizo katika siku nne wakati walipolala kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Kagera Sugar zikiwa zimebaki mechi mbili ligi kumalizika.
  Ushindi uliifanya Simba ifuzu kucheza michuano ya CAF msimu ujao baada ya kujihakikishia kumaliza katika moja ya nafasi mbili za juu kutokana na kufikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga iliyo katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 43 huku ikiwa imebakisha mechi tatu.
  Azam yenye pointi 50 huku ikiwa na mechi moja mkononi, itaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi Jumamosi.
  Yanga ambao Jumapili walikumbana na kipigo kisichotarajiwa cha 3-2 kutoka 'ndugu zao' wa Toto African baada ya kutanguliwa kwa mabao 3-0 katika dakika 39 tu za kwanza mjini Mwanza, jana walizamishwa na bao pekee lililofungwa katika dakika ya 29 na mchezaji wa Simba, Shija Mkina, ambaye yuko Kagera kwa mkopo.
  Simba ilianza kuhesabu goli la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa kiungo Uhuru Selemani aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Mganda Emmanuel Okwi na kiungo kipenzi cha mashabiki wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' akafunga moja ya mabao bora ya msimu wakati alipokimbia na mpira kutokea katikati ya uwanja na kupiga shuti lililomshinda kipa Amani Simba wa JKT katika dakika ya 17.
  Kiungo wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto alifunga goli la "nembo yake" la shuti la mbali katika dakika ya 64 na kuisogeza Simba jirani zaidi na ubingwa.
  Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, mechi ijayo ya Simba dhidi ya Moro United itachezwa Aprili 23 saa 1-0 usiku badala ya Aprili 25 ili kuwapa muda 'Wekundu' kujiandaa na mechi yao ya kwanza ya hatua ya 16-Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy itakayochezwa jijini Dar es Salaam.
  Katika mechi nyingine za ligi kuu ya Bara zilizochezwa jana, Ruvu Shootingi ilishinda 1-0 dhidi ya Moro United, Toto waliendelea kujinasua kutoka katika hatari ya kushuka daraja kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya African Lyon, huku vijana wa kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio', Coastal Union wakishinda 2-0 ugenini dhidi ya Polisi Dodoma.
  Vikosi kwenye Uwanja wa Taifa vilikuwa;

  Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Kelvin Yondani, Juma Nyosso/ Obadia Mungusa (dk.77), Patrick Mafisango, Uhuru Selemani, Mwinyi Kazimoto, Gervais Kago/ Edward Christopher (dk.79), Haruna Moshi 'Boban' na Emmanuel Okwi.
  JKT Ruvu: Amani Simba, Kessy Mapande, John Mhize, Hassan Kikwala, George Minja, Jimmy Shoji, Haruna John/ Furaha Tembo (dk.52), Nashon Matari, Hussein Bunu, Mohammed Banka/ George Mketo (dk.71) na Emmanuel Pius/ Samwel Kamtu (dk.59).

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wanakumbushia kichapo cha Yanga kutoka kwa Kagera (1-0).
   
Loading...