Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,254
- 21,276
Kama mlivyosikia kwamba ukiwa na vyerehani vinne tayari ni kiwanda, yaani ukiwa na vyerehani 40 una viwanda 10.
Hii issue imenikumbusha mwaka 2013, kuna rafiki yangu flani alikua anafanya kazi kwenye kampuni flani ya wahindi ina deal na security, firefighting na mambo ya cartrucking, sasa wao walikua kitengo cha Marketing na mhindi flani, wanachofanya wanaenda site kuongea na wateja ambao sometimes wanawapata kupitia majarida mbalimbali na kuwapigia simu.
Sasa bwana wakaongea na Mangi mmoja kwenye simu kwamba wao wanatoa huduma mbalimbali kwenye makampuni, maduka, na office mbali mbali, basi wakapanga appointment, kumbuka kazi wanazofanya wao ni kwenye office kubwa kubwa, kwenye makampuni makubwa.
Sasa siku ya siku ikafika asubuhi na mapema wakaingia kwenye "NAVARA" safari ya kwenda kwa Mangi kibaha maili moja ikaanza, kichwani wanaimagine huko tutakuta supermarket, au kiwanda flan, au jamaa atakua ni Transporter, basi bwana, gia mosi, gia pili mara kibaha mizani ya zamani hii hapa, wakampigia simu, ndio tunaingia maili moja hapa tupe ramani vizuri.. Mangi akawaelekeza.
Mara Vuuu, break zinakanyangwa mbele ya Mangi, walichokiona ilibidi muhindi awashe sigara yake ya Malboro kwanza, ilikua ni kituko!! Yaani walikuta ni kioski, yaani ni kiduka cha mbao kidogo dogo flan hivi kimechoka sana, yaani kwa haraka haraka mali iliyokuwemo mule kioskini ilikua kama ya laki mbili hivi au pungufu ya hapo, Jamaa hata hawakutaka kuongea nae, wakatia reverse gear, wakarudi kinondoni wakiwa hoiii..
Sasa ukikumbuka jinsi CCM kupitia JPM ilivyokua inajitapa kuhusu viwanda utacheka sana jinsi saivi wanavyoongelea hivi viwanda. Nakumbuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika kibaha JPM akiongozwa na Bulembo waliongea maneno matamu sana kuhusu viwanda, ila kumbe walikua wanamaanisha viwanda kama vyerehani na kijiwe cha "shoe shine" cha kushonea viatu.
Na ili kulielewa hili wazia juzi wametangaza kua eti kiwanda cha "General Tyre" kimetengewa milion 70 kukifufua, REALY??? Yaani kiwanda cha matairi ukifufue kwa only 70,000,000? Pesa ambayo ambayo ukililia sana ndo utapata horse ya scania mtumba flan hivi umechokachoka wa R420!!
Yaani hiyo 70mil hakuna kitu itafanya, ikumbukwe hapo inainclude material and operational cost... Ifike mahala serikali iache utani na Nchi yetu. Wao wanatembelea chuma zenye thamani ya 200mil+ ila hata kusema basi hiki kiwanda tukipe japo pesa yenye thamani ya VX V8 japo 5 tu hawawezi.
Ukweli ni kwamba mpaka miaka Mitano itakapoisha hakuna kiwanda chochote kitakachosimama na kuwaajili Watanzania, hata hiyo General Tyre haiwezi kusimama kwa 70mil..
Nchi ya viwanda na uchumi wa kati ilikua ni AHADI HEWA NA HADAA KWA UMMA WA WATANZANIA. Sisi tumejizoelea maisha yetu ya kawaida tu, hamkua na haja ya kututamanisha vitu msivyoweza kutimiza, leo unasema vyerehani vinne ni kiwanda, basi sawa, kwahiyo basi hata kwa wakaanga chips ni "Food Processing Industries"
Nimalize na mfano Huu; kuna siku rafiki yangu mwengine mbali na yule wa hapo juu alijikoki na wenzie( kutoka Madrasa flani hivi Mabibo pale), walikua wanaenda kufanya Dua/ kisomo kwenye nyumba flani hivi ya Muarabu, kwenye akili yao wakajua leo huko kutakua na msosi wa nguvu kuanzia Biriani na mazagazaga ya kutosha(si unajua tena hawa ndugu zetu kwa msosi-samahani lakini, ni utani), maskini wakabeba ndizi wakazitia ndani ya kanzu kila mtu kwaajili ya makamuzi, kufika pale hamna harufu yeyote kusema labda msosi unasababishwa, wakajipa moyo anyway labda muarabu kaamua kuagiza "catering" so after duaa mzigo utaletwa hapa, weeeeeee, watu wamemaliza dua zimeletwa chupa za chai na biscuts..
Amkeni Watanzania, Hakuna Viwanda!!!!