Uchaguzi 2020 Kwa vituko vya Seif na CHADEMA, hakika upinzani bado sana Tanzania

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Ukisikiliza yanayoendelea ndani ya ACT na CHADEMA kuhusu suala la Wagombea urais Muungano na Zanzibar utacheka sana na utagundua dhahiri kuwa hakuna upinzani Tanzania bali wasaka tonge.

Mwanzoni ACT wamemshobokea Membe toka akiwa CCM. Baada ya hapo wakamdhamini NEC awe mgombea wao kwa sera ya 'Kazi na Bata'

Upande wa pili, CHADEMA wao wamemteua mgombea urais Zanzibar na kumdhamini ZEC. Anakuja Tundu ambaye alishiriki vikao halali kikatiba na kutangaza kutomtambua mgombea wa urais CHADEMA kwa upande wa Zanzibar.

Hizi ni akili za mbayuwayu huwezi kumkana mgombea aliyekwiteuliwa na NEC kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano au aliyeteuliwa na ZEC kugombea urais wa Zanzibar. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Zanzibar.

Waswahili tuna usemi wetu 'Ukiona kenge anatoa damu masikioni ujue anakufa'

Tarehe 28.10.2020 kipigo kipo pale pale.
 
Hawa ndio wanamlaumu Magufuli kwa udikteta lakini kna tofauti kubwa Magufuli anafanya hivyo kupitia vikao halali lakini wao hata vikao halali hawavieshimu bali wanatoa matamko jukwaani.

Ni kama walivyofanya maamuzi ya kumteua Lowassa waliogopa wakiweka ushindani asingepitishwa, kwa siasa za namna hii ccm wataendelea kubaki madarakani muda mrefu.
 
Umegonga nyundo utosini

Kama wana ubavu waiambie NEC na ZEC kuondoa kwenye ballot paper majina ya Mgombea wa ACT Bara na Mgombea Chadema visiwani. wakishindwa kufanya hivyo maana yake bado ni wagombea na nihalali kwa wafuasi wao kuwapigia kura. Rekodi itasema vyama hivyo vimepata kura ngapi za wagombea wao katika uchaguzi.
 
Shekhe Ponda kasema kuwa Membe atulie atapangiwa kazi katika siku mia za Lissu madarakani.

Vilevile Sheikh Ponda kasisitiza ndani ya siku ishirini za Raisi wa Watu Jemadari Tundu Antipas Lissu Mashekhe wa Uamsho na wale wa Answari Suna watarudi nyumbani kwao kwenye familia zap.
 
Shekhe Ponda kasema kuwa Membe atulie atapangiwa kazi katika siku mia za Lissu madarakani

Vilevile Sheikh Ponda kasisitiza ndani ya siku ishirini za Raisi wa Watu Jemadari Tundu Antipas Lissu Mashekhe wa Uamsho na wale wa Answari Suna watarudi nyumbani kwao kwenye familia zap
Afu wanajifanya kuwa wana kamati kuu, Ponda ni zaidi ya kamati kuu!
 
Shekhe Ponda kasema kuwa Membe atulie atapangiwa kazi katika siku mia za Lissu madarakani

Vilevile Sheikh Ponda kasisitiza ndani ya siku ishirini za Raisi wa Watu Jemadari Tundu Antipas Lissu Mashekhe wa Uamsho na wale wa Answari Suna watarudi nyumbani kwao kwenye familia zap
makubwa ponda sasa ndie kiongozi mkuu wa CHADEMA AU? Haya matamko duuuu
 
Vituko viko ccm, Juzi Magufuli analia kawe apelekewe Gwajima wakati yuko naye jukwaani.

Leo Gwajima anaitwa RASHIDI.

Kitila Mkumbo alishindwa kupeleka maji ubungo akiwa katibu mkuu wizara ya maji.

Leo anagombea Ubunge anaahidi kutuletea maji tukimchagua kuwa mbunge.

Utashangaa akili za CCM ziko wapi?
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom