Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kwa kweli kwa kila mtu aliyemsikiliza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akilihutubia Taifa kupitia social media, kuhusu madhira aliyopitia kwa miaka 5 mfululizo ya kunyanyaswa na kuteswa hadi kufungiwa akaunti zake za benki na hicho kinachoitwa Task Force ya TRA, hakika atakuwa amelengwa lengwa na machozi.
Nifahamuvyo Mimi ni kuwa kwa nchi inayoendeshwa kwa utaratibu wa utawala bora unaozingatia Katiba ya nchi, ambayo viongozi walioko madarakani waliapa kuitii, chombo pekee kilichopewa mamlaka hayo ni mhimili wa mahakama.
Ninachijiuliza ilikuwaje viongozi Wa utawala wa awamu ya 5 waamue kuivunja na kuisigina sigina Katiba hiyo ya nchi, waliyoapa kuitii na kuiheshimu?
Hivi hii serikali inawezaje kuendesha mambo yake bila kufuata Katiba ya nchi na taratibu za kisheria na kujifanyia tu mambo yake kienyeji ili mradi tu wameagizwa na yule mwendazake, ambaye ndiye aliyekuwa Mkuu wa mhimili wa Serikali?
Hivi utawezaje kutofautisha vitendo hivyo vya Task Force na vitendo vya majambazi kuwapora mali zao raia wasio na hatia?
Hakika Mungu amelipenda Taifa hili kwa kulinusuru kwa mengi, kwa kumpenda zaidi yeye na kumtwaa mbele za haki, alikodai kuwa atatuma "application" kwa Mungu ili kuomba nafasi ya kiwaongoza malaika.
Kila la kheri huko alikokwenda, tinamuombea kila aina ya baraka ili afanikishe azma yake ya kuwa Mkuu wa malaika.