Kwa viongozi wetu (hasa Marais na Wake zao) kutibiwa katika hospitali za 'Siri' na Watanzania 'kufichwa' pia ni sehemu ya tatizo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Ni Hospitali ambazo naziheshimu sana japo najua ni za Watu fulani fulani kutokana na Umuhimu wao hapa nchini Tanzania. Sikatai kuwa Kifo huwa hakina aina ya Hospitali bali muda wa ' Israeli Mtoa Roho ' ukifika tu hata ukiwa Umelaza katika Hospitali yenye Hadhi duniani 'utaondoka' tu kwenda zako Udongoni / Mavumbini.

Hoja yangu Kubwa tu hapa ni kwamba ni kwanini Viongozi hawa ' Waandamizi ' waliowahi Kuongoza nchi yetu hii ' pendwa ' wakipelekwa tu katika hiyo Hospitali huwa kunakuwa na ' Usiri ' mkubwa na hata Watanzania hwa ' tunafichwa ' pia labda mpaka ' Vifo ' ndiyo vitokee kama hivi tunajua? Na kwanini 95% ya Watumishi wenye ' Vinasaba ' na Hospitali hiyo ya ' Siri ' jijini Dar es Salaam huwa hawapendi kwenda Kutibiwa hapo na wapo ambao wanasema ' Wanaiogopa ' ila sababu ukiwaomba hawakupi ng'o.

Kuwaweka Viongozi Waandamizi katika Hospitali za ' Siri ' huku mkituficha Watanzania pia ni sehemu ya tatizo. Hawa Viongozi ni Mali ya Watanzania siyo ya Watu fulani na kuna wengine tukisikia ni Wagonjwa huwa tunapenda kwenda Kuwaona, Kuwaombea na ikibidi hata ' Kuwatambikia ' ili wapone haraka ila mkiwaweka katika Hospitali zenu ze ' Usiri ' tunaogopa hata Kuthubutu kwenda.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Gulwa,

Ukirejea vyema tu Maelezo ya Rais Mstaafu Kikwete kisha ukatuliza vizuri kabisa Akili zako na Kutafakari kwa Kina Ugonjwa na Sababu utaijua tu.
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,698
2,000
Watatuficha vyote lakini vifo ndio vitawaumbua, wanajua kabisa kwenye hospitali zetu za kawaida huduma ni mbaya ndio maana hawaendagi huko, hata masomo, shule ambazo wanasoma watoto wao pia zina huduma nzuri, sio kama za kwetu hizi za malofa(kayumba), kiujumla huduma zao hazifanani na za kwetu!
 

Bruno Toto

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
488
1,000
Tangu huu ugonjwa uingie Tanzania, watu wote wanaokufa utasikia COVID 19,hta ugongwe na gari, kwani hakuna ugonjwa mwingine wa kuua Hapa Tanzania?
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,713
2,000
Hospital zingine si vizuri kuzitaja taja kwa sababu ya kiusalama zaidi. Pale kuna kila huduma kwa kifupi ni zaidi ya MOI. RIP Mzee wetu, tulikuwa tunakuhitaji mno hasa kuelekea huu uchaguzi Mkuu ili ushuhudie mabadiliko wanayoyahitaji watanzania kwa macho yako. Mungu amekupenda zaidi - "Pumzika kwa Amani", hili ndilo tu tunaweza kulisema tu kwa sasa.
 

Mwana

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
5,260
2,000
Hospital zingine si vizuri kuzitaja taja kwa sababu ya kiusalama zaidi. Pale kuna kila huduma kwa kifupi ni zaidi ya MOI. RIP Mzee wetu, tulikuwa tunakuhitaji mno hasa kuelekea huu uchaguzi Mkuu ili ushuhudie mabadiliko wanayoyahitaji watanzania kwa macho yako. Mungu amekupenda zaidi - "Pumzika kwa Amani", hili ndilo tu tunaweza kulisema tu kwa sasa.
Amen and Amen
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom