Kwa viongozi wangu wa CHADEMA kitaifa kuhusu "CHADEMA ni Msingi"

RUTO

Senior Member
Dec 19, 2013
147
29
Kwanza napenda kutumia fursa hii kuwapongeza kwa uimara mnaouonyesha katika kukisimamia chama katika changamoto nyingi zinazokikumba. Ninyi ni wavumilivu na wenye msimamo katika mapambano haya makali dhidi ya maadui wa chama chetu. Hongera mwenyekiti wangu F. Mbowe pamoja na katibu wako mkuu Dr W.Slaa.

Lengo kuu la ujumbe wangu huu wa wazi kwenu ni kuwapa ushauri wangu juu ya mkakati huu wa maana wa CHADEMA NI MSINGI. Kusema kweli mkakati huu ndio roho ya chama chetu kwa sasa na kwa miaka mingi ijayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mkakati huu unakipeleka chama katika ngazi ya chini kabisa. Kama tukivuta subira tukautekeleza mkakati huu kwa ustadi wa hali ya juu,nawahakikishia kuwa CHADEMA itakuwa moto wa kuotea mbali kuliko ilivyo hivi sasa. Hii ni kwa sababu chama kitakuwa kimefika kila kona ya nchi hii na kwa kila mwananchi.

Wananchi wanaipenda sana CHADEMA. Tatizo kubwa ni kuwa hawajapelekewa CHADEMA. Ni nani anawajibu wa kuwapelekea CHADEMA? Kwanza ni mimi,wewe na yule. Na kwa mantiki pana zaidi ni sisi,ninyi na wale. Hivyo ni ni jukum la kila mwana CHADEMA kuhakikisha anaijenga CHADEMA popote pale alipo. Sasa katika utekelezaji wa mkakati huu wa CHADEMA ni msingi changamoto kubwa imekuwa ni ya kujitolea mno kiasi kwamba utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua. Ninaposema hivi si maanishi kuwa wale watekelezaji wake wanatakiwa kulipwa, bali wanatakiwa kuwezeshwa kivifaa haswa vifaa vya chama. Ni vigumu mtu anatoka nyumbani kwake tokea asubuhi anakitumikia chama hku akitakiwa kutoa tena vijisenti vyake vya alivyovitenga kwa ajili ya kutoa fotokopi ili shughuli za chama ziende. Au anatoa fedha yake ili anunue bendera ya chama kwa ajili ya wanachama waliofungua tawi lao jipya na hawakuwa na namna ya kupata bendera.

Lakini pia rasilimali fedha na vifaa visipelekwe katika makao makuu ya kanda tu. Zipo ofisi za mikoa,wilaya na kata ambazo zipo karibu na wananchi na wanachama wa CHADEMA. Kitendo cha kupeleka rasilimali zote kwenye kanda halafu hawa wengine wote wanajitolea sidhani kama ilikuwa sahihi. Kwani inasababisha kazi ya kanda kuwa ngumu kwani co-ordination na ngazi nyingine inakuwa haipo na hatimaye mkakati wa CHADEMA ni msingi kusuasua.

Jambo lingine ni chama kutumia gharama kubwa kwenye chaguzi ndogo. Wana CHADEMA na Watanzania wengi tunatamani kuona mabadiliko ya haraka. Jambo hili linakifanya chama kutimiza azma hiyo ya watanzania kwa gharama yoyote. Hali hii imekifanya chma kutumia gharama kubwa katika chaguzi ndogo badala ya kuwekeza rasilimali zake kwenye mipango ya muda mrefu ynye kuwahakikishia Watanzania mabadiliko wanayoyatamani. Rasilimali nyingi za chama zipelekwe kwenye hii programu ya CHADEMA NI MSINGI ambayo kimsingi ndio itawafanya watoto wenye miaka 5,7,9 11 n.k waanze kuinywa ile damu ya CHADEMA ambao kimsingi ndio wapiga kura wetu wa mwaka 2020,2025,2030..... na ambao ndio wafia chama wa baadae. Hili litawezekana tu kama CHADEMA ni msingi itakelezwa ipasavyo.

Mwisho kabisa naomba niwaambie viongozi wangu kuwa CHADEMA ikiwa dhaifu au ikifa itakuwa vigumu kwa Watanzania kuamini chama kingine chochote cha upinzani kwani vitakuwa ni vyama vya msimu tu. Ni wajibu wa viongozi na kila mwanachama kuilinda na kuitetea CHADEMA popote na kwa gharama yoyote ile. Mienendo yenu kama viongozi wa juu na sisi viongozi wa chini iwe inaendana na kile tunachokihubiri na chenye maslahi kwa Watanzania. Toauti na hapo Watanzania watatuacha muda siyo mrefu.

Naomba kuwasilisha
Ahsanteni
 
Kama ulisoma WARAKA WA SIRI wa Dr Kitila uliongelea yote hayo,Kwa kifupi ndugu yangu unapoteza nguvu zako bure kushauri hayo,Uongozi wa sasa wa CHADEMA upo pale kupiga hela tu basi.Mbaya zaidi wanakula peke yao labda na wale wanaowalamba miguu basi.Sahau kwamba hawa Viongozi watakuja kupeleka pesa kwenye ofisi za ngazi chini mikoani labda mpaka waondoke madarakani.
 
Kama ulisoma WARAKA WA SIRI wa Dr Kitila uliongelea yote hayo,Kwa kifupi ndugu yangu unapoteza nguvu zako bure kushauri hayo,Uongozi wa sasa wa CHADEMA upo pale kupiga hela tu basi.Mbaya zaidi wanakula peke yao labda na wale wanaowalamba miguu basi.Sahau kwamba hawa Viongozi watakuja kupeleka pesa kwenye ofisi za ngazi chini mikoani labda mpaka waondoke madarakani.

KATIBA kwanza
 
Kunahitajika usimamizi tofauti na huu uliopo sasa. Nina wasi wasi taarifa zinazotolewa.zinaweza kuwa za kupika, kumbuka sasa tuko kwenye uchaguzi ngazi ha kata tumejihakikishia kwa kiwango gani kwamba misingi na matawi yamekamilika?

Kiukweli Chadema ni msingi ndo kila kitu, lakini ikitokea isifanikiwe tutalia maana operesheni nyingine zimesimama kwa ajili hii. Nimewahi kuandika humu kwamba makao makuu wanahitajika kufanya operesheni maalum ya tathimini kama ile ya M4C kwa kila kanda.
 
Rejea waraka wa kitila,

kama kitila aliandika yote haya uliyoandika na mengine mengi akaitwa msaliti kwa nini na wewe usiitwe msaliti?
 
Chadema ni msingi inakkwamishwa na viongozi wa mikoa na wilaya. Wana hofu na ukiwa mshabi wa chadema ni msingi, uanachama wako uko hatarini.
 
Back
Top Bottom