Kwa vile tatizo ni CCM, Rais Vunja Bunge chini ya Article 90 ya Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa vile tatizo ni CCM, Rais Vunja Bunge chini ya Article 90 ya Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 20, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa, kura ya kutokuwa na imani na waziri Mkuu ni nzuri sana kwani inamaanisha kuwa watu hawana imani na serikali yao na moja kwa moja inaonesha kuwa hawana imani na Rais. Huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na "Waziri Mkuu" halafu ukabakia na imani na Rais. Kwa sababu, hata Waziri Mkuu akiondoka bado utakuwa na rais yule yule na itakuwa ni rekodi tu kuwa mawaziri wakuu "wawili" wameshindwa kufanya kazi. Yawezekana kabisa hoja ikajengwa vizuri kuwa tatizo kubwa ni Rais mwenyewe kama mkuu wa serikali na utumishi wote wa umma nchini. Hivyo, kumwajibisha Waziri Mkuu ni njia moja tu nyuma ya kumwajibisha rais - kwani Rais anaweza kuwajibishwa na bunge kwa mashtaka ya kibunge (impeachment) chini ya Ibara ya 46.

  Lakini ukiondoa la kumwondoa rais tatizo kubwa la msingi linakabili utawala wa Tanzania ni CCM. Kumwondoa Waziri Mkuu wa CCM hakutaondoa tatizo la msingi kwani Waziri Mkuu atakayekuja atakuwa ni miongoni mwa wabunge hawa hawa na kwa hakika kabisa atakuwa ni mwana CCM. Sasa, je kumwondoa Pinda na serikali ya sasa na kuingiza serikali nyingine kutakuwa kumetatua tatizo la msingi yaani CCM yenyewe?

  Ushahidi uko wazi; baada ya kuondolewa Lowassa na mawaziri wengine aliteuliwa WM mwingine na baraza jingine lakini matokeo yake yamekuwa yale yale. Je, itakuwa ni ajabu sana kufikiria kwamba Pinda akiondoka ataingia Waziri Mkuu mwingine ambaye naye hatoukwa tofauti na hawa wengine kwa sababu na yeye kama waliomtangulia nao ni wana CCM? Au kwa namna moja tunapenda drama ya serikali kuangushwa, na mazingaombwe yote yanayotokana na hilo ili tuweze kusema serikali imeanguka? Vipi kama ikianguka na bado ikaja serikali nyingine?

  Binafsi naamini, njia pekee ya kuokoa nchi yetu na hasa utendaji serikalini siyo kuwaacha wana CCM waendelee kuteuliana na kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali; njia pekee ni kubadilisha chama tawala. Sasa hapa bila ya shaka ninatofautiana na wengine wengi ambao bado wana matumaini kuwa CCM bado inaweza "kutawala vizuri" kama Waziri Mkuu akiondolewa. Kuondolewa kwa Waziri Mkuu na baraza la sasa itakuwa ni kwa ajili ya kuwawajibisha wao tu kwa yaliyotokea na kwa haki hoja inaweza kutolewa kuwa wanastahili. Lakini, kudhania kuwa hawa wakiondoka tutakuwa tumegusa tatizo la msingi ni kujidanganya.

  Kwa kadiri ya kwamba CCM bado iko madarakani basi tatizo la msingi BADO lipo!

  Hivyo hoja inayotakiwa kutolewa kwa usahihi kabisa chini ya Ibara ya 90 ya Katiba ni Rais kuamua kuvunja Bunge. Ili hili lifanyike badala ya kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Azimio la Bunge litolewe kumtaka Rais avunje Bunge ili watu wote warudi madarakani na Chama cha Mapinduzi kitafute ridhaa mpya kwa wananchi! Hoja ya Zitto naikubali kwa asilimia 100 lakini pia naamini haitagusa msingi wa tatizo lenyewe; ningependa viongozi wa upinzani waende mbali zaidi ili wananchi warudi kwenye uchaguzi ndani ya miezi mitatu ijayo!

  Faida za kuvunja Bunge:

  a. Kila chama kitatengeneza hoja mpya ya kwenda kwa wananchi na kutafura ridhaa yao
  b. Kundi la wabunge wachovu wataondolewa na wananchi
  c. Wabunge wapya ambao wanakubalika na wananchii watapatikana
  d. Rais ajaye atapewa nafasi ya kuunda serikali kutoka katika wabunge wapya
  e. Rais mwenyewe naye atatafuta ridhaa na kushindanishwa na wengi
  f.
   
 2. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  :msela:Imetulia Mkuu! Kazi ni kwa mibunge (wabunge) ya CCM imejaa unafiki. Ngoja tuone attempting ya Zitto na Pia M4C itarahisisha kazi ya kumuondoa mkoloni CCM.
   
 3. w

  wakijiwe Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suluhisho si kuvunja bunge, kinachotakiwa ni kuwaadabisha wanaohusika ili wengine wapate somo.
  At the end we need:
  "The government which is committed to greater accountability in the delivery of services to the people, and such government is committed to similar transparency in the use of the national development budget"
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Serikali ya CCM inajiita ni sikivu, lakini ukweli ni kwamba ni KIZIWI na imetia pamba masikioni.
  Chadema na wapenda nchi wote kwa ujumla wahakikishe kelele hizi za kufukuza wezi zinaendelea hata baada ya vikao vya bunge
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  F.rais atakayekuja atakua ana adabu na mtendaji
   
 6. i

  isoko Senior Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MzeeMwanakijiji hoja yako nzito na inamashiko lakini kwa wabunge wa ccm kazi ipo ngoja tuone
   
 7. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mkuu Rais akivunja bunge atakuwa kanya halafu kayakalia hapo hapo sidhani kama anaweza kufanya hili.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,
  Uchaguzi ukifanyika upya leo, CCM itarudi tena madarakani. Taasisi na Dola zinazosimamia mambo haya ni zilezile. Katiba itabidi iwe hiihii. Watanzania ni hawahawa. Binafsi nimefarijika mno na mjadala wa juzi na jana Bungeni. Angalau baadhi ya Wabunge wameamua kuwa wakweli. Wanasema wazi kiini cha matatizo yetu ni nini. Ubia wa DEO na ZITTO unanifurahisha sana. Utadumu?
  Baadhi yetu tumewasema sana hawa mawaziri wetu humu JF. Hatukusikilizwa kwa muda mrefu. Tumechelewa sana. Utajiri wa wanasiasa wetu wote waliowahi kuwa mawaziri umetokana na mchezo huu mchafu ulioanza zamani tangu miaka ya 80 mwishoni.
   
 9. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji wazo lako ni zuri lakini kwa mtazamo wangu naona unakuwa too ambotious na mabadiliko ambayo kiuhalisia yatatugharimu sisi walipa kodi bila umuhimu wowote. Nadhani hukutumia busara kufikiria pendekezo lako.

  Ni kweli tunataka uwajibikaji urudi serkialini lakini sidhani kama tunataka kuingia tena gharama za uchaguzi mkuu mwingine chini mwaka mmoja na nusu tu baada ya uchaguzi uliopita, sidhani kama hiyo ndio busara pekee tunayweza kuitumia kutatua tatizo la uwajibikaji, ukiachilia mbali kwamba uchaguzi wenyewe hatuna uwezo wa kusimamia wenyewe kikamilifu bila msaada toka nje.

  Hatua ya mh Zitto ni moja, na naamini ina busara ndani yake and is realistic ukiachilia mbali inaingia akilini.
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kwa hawa ccm hili hawawezi kulitekkeleza
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  kwa sasa ngumu ila katiba mpya itamke wazi NI MARUFUKU MWANA CCM KUPEWA WADHIFA WOWOTE SERIKALINI iwe kama misri
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanini wana CCM tu?
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa watu wanafikiria haya matatizo yametokea nje ya CCM; kwamba ni matatizu ya watu tu kwa hiyo tukibadilisha watu hapa na pale matatizo yataisha. Nimekuwa nikilisema sana hili mwaka huu kuwa asili ya matatizo mengi ni kushindwa kwa sera za CCM. Hoja ya wapinzani inatakiwa kuwa hiyo; kwamba sera za CCM zimeshindwa na ndio chanzo cha matatizo haya tunayoyaona. Tatizo siyo watu tu ni sera nzima; ni chama kizima. Hoja ikijengwa vizuri kuwa tatizo ni CCM basi hata ukiitishwa uchaguzi sasa CCM haiwezi kurudi madarakani. Lakini kama tatizo ni "mtu mmoja mmoja" basi hata 2015 hali itakuwa ile ile; watakataliwa watu na siyo chama!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gharama ya kuitisha uchaguzi sasa hivi ni ndogo sana kulinganisha na gharama ya wao kuendelea kutawala kwa miaka mitatu iliyobakia!
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu MMM impeachment unayoirejea iko ibara ya 46A ile ya 46 inapiga marufuku kumshtaki Rais akiwa madarakani. Mkuu nadhani Wabunge kwa maana ya Zitto ameangalia vizuri vifungu hivyo na kugundua kwamba ni vigumu sana kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais. Ukirejea Ibara ya 46A (2) vifungu vidogo vya (a), (b) na (c) utagundua ilivyo ngumu kumshtaki Rais. Ila ukirejea ibara ya 53A na Ibara ya 52 hasa ibara ndogo ya 1 basi utaona mambo yale yaliyoongelewa Bungeni jana yanamhusu PM moja kwa moja na kwa mujibu wa ibara hizo ni rahisi kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa mujibu wa Katiba. Hii itaonyesha hasira za wabunge kwa serikali na Rais itabidi awe makini kuanzia hapo.
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Precisely! As long as ccm wapo madarakani tusitegemee mabadiliko tunayoyahitaji isipokuwa tutegemee hali kuwa mbaya zaidi which means gharama kubwa maradufu ya ile uchaguzi mpya!
   
 17. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuvunja bunge na kufanya uchaguzi mpya ni hatua kali na yakishupavu lakini haitasaidia kwa sasa kwasababu system iliyowaweka madarakani waliopo leo bado inanguvu ileile yakuwarudisha. Wengi tunaamini serikali iliyopo madarakani imeingia kwa mgongo wa vyombo vya usalama.

  Tukiitisha uchaguzi mwingine kwakutumia utaratibu wa 2010 (katiba na vyombo vya usalama) tusitegemee matokeo tofauti sana. Wananch wameamka wanaona maovu lakin kwa namna moja au nyingine vyombo vya usalama vinanufaika na waliopo madarakani ndio maana ni rahisi kurubuniwa au kuamrishwa kusimamia matakwa ya wezi/mafisadi/manyang'au au wahujumu uchumi.

  Kubadilisha baraza la mawaziri peke yake hakutaleta matokeo mazuri sana na kubadilisha maisha ya mtanzania. Baraza la mawaziri libadilike na hatua kali zichukuliwe.
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mawazo ya watu kama hawa ndiyo yanawapa upenyo hawa wezi. Mtu anaona kuitisha uchaguzi ni gharama, lakini ndege mbovu inayokodishwa kwa dola milioni 200 haoni kama inamgharimu zaidi. VIP Lounge inayojengwa pale uwanja wa ndege kwa dola milioni 8 haoni kama ni tatizo. Na kibaya zaidi, haya ni awazo ya mtu anayejiita revolutionary na msomi.
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na hasa kama utafunaji kwa kasi hii utaendelea. Mawaziri wanashindana kuzitafuna zilizochini ya wizara zao. Mwanakijiji usidhani tatizo hili liko CCM tu. Utafunaji huu uko kila mahali. Hata ukiwapa CHADEMA madaraka ya kuongoza nchi leo hali itakuwa hiihii. Waulize CHADEMA ruzuku yao ya zaidi ya milioni 120 kila mwezi inatumikaje.
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ni heri gharama za uchaguzi mkuu kuliko hasara tunayozidi kuipata sasa,
   
Loading...