Kwa vijana wa leo ijue historia ya vyama vingi awamu ya pili baada ya uhuru

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
Ni vizuri kwa vijana ambao hawakuwepo mwaka 1991 wakati wa kongamano la mageuzi Diamond Jubilee wakasoma hii habari na kugundua kwanini upinzani hauna nguvu kwa Tanzania ukilinganisha na nchi nyingine.

Kama tulisambaratika baada ya miezi tu je tutafika kweli tulikodhamiria kufika pale tulipokutana Diamond Jubilee?

Mwandishi Bubelwa Kaiza (Facebook)
HISTORIA YA HATUA ZA AWALI ZA KUTAFUTANA KWA WAASISI WA MAGEUZI YA SIASA ZA VYAMA VINGI NCHINI TANZANIA

Kunako majaliwa ninakusudia kuandika historia ya mageuzi ya siasa za vyama vingi hapa nchini. Inasikitisha, pengine kwa kuwa mwitikio wa wasomi kupigania mageuzi ya siasa za vyama vingi ulikuwa mdogo, historia ya vyama vingi hapa nchini haijaandikwa vya kutosha na bila kupotoshwa.

Kwa sasa tunaweza kusoma vipande kadhaa vya taarifa kuhusu harakati za siasa za mageuzi nchini ila si historia kamili na sahihi ikianinsha na kubainisha kumbu kumbu sahihi za muda wa na matukio makuu, sababu za matukio hayo, wahusika wakuu, michakato na minyukano, kupanda na kushuka kwa mashujaa wa kweli na wanyemeleaji wa historia ya mageuzi ya kisiasa nchini kuanzia 1989 hadi 2015.
Kwa kuanzia, nimeanza kwa kuweka kwa usahihi kumbukumbu kadhaa.

1. KONGAMANO LA KITAIFA LA MAGEUZI JUNI 1991
Juni 11-12/1991 kulifanyika Kongamano la kitaifa la mageuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam. Wahusika wakuu wa kongamano hilo walikuwa [vijana wakati huo] Mabere Marando, Ringo Tenga, Ndimara Tegambwage, Prince Bagenda, Mashaka Nindi Kimoto (apumzike kwa amani) na Mch. Christopher Mtikila (rip). Wazee [hawa wote ni marehemu kwa sasa na wapumzike kwa amani] walikuwa akina Chief Abdallah Said Fundikira, Kasanga Tumbo na Kasela Bantu.

Hao walitafutwa mahsusi na kupewa nafasi za kuoneka mbele ili kufuta hisia madai ya demokrasia ya vyama vingi nchini yalikuwa ni matakwa ya vijana. Kwa Zanzibar walialikwa washiriki 11, wafuasi na wawakilishi wa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa kizuizini wakati huo, wakiongozwa Mzee Shaaban Mloo (apumzike kwa amani) na aliambatana na Awesu Dadi na wenzake.

Aidha kulikuwa na Watanzania walikokuwa wanajulikana kwa misimamo yao ya kimageuzi tangu miaka ya 1960 ambao nao walialikwa pia, lakini pia wakimwakilisha Oscar S Kambona.

Hao ni Mzee Dastan Lifa Chipaka, Mzee Wilfrem Mwakitwange (apumzike kwa amani) - alikuwa mmiliki wa beach resort hotel ikijulikana kwa jina la Rungwe Oceanic), Mzee Kichoweko, Bwn. James Mapalala na wengineo.

Chuo Kikuu walialikwa akina Prof. Mwesiga Baregu na wanafunzi akina James Mbatia, Anthony ABC Komu, Idrissa Al Nuru (amekwisha tangulia mbele ya haki, apumzike kwa amani) na wanafunzi wengineo.

2. MAAZIMIO YA KONGAMANO LA KITAIFA
Mwishoni mwa kongamano kulitolewa maazimio kumi, mojawapo likiwa ni Tanzania kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya Siasa. Kisha iliundwa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba, kwa Kiingereza, ikijulikana kwa jina la National Comiittee for Constitutional Reform (NCCR) ikiongozwa na Chief Abdallah Said Fundikira, na Katibu wake Mkuu akiwa Mabere Marando.

Kamati hiyo kwa upande wa Zanzibar iliitwa Kamati ya Uhuru wa Kisiasa (KAMAHURU) ikiongozwa na Mzee Shaaban Mloo lakini aliyekuwa defacto leader ni Maalim Seif Sharif Hamad. Maazimio ya Kongamano hili yaliandikwa na kusambazwa katika kjitabu kilichojulikana kwa title ya TUNACHOTAKA SASA.

Katika Kongamano hilo la kitaifa hakuna kumbukumbu zinazoonesha Mzee Mtei, Freeman Mbowe na waasisi wengine wa Chadema kuhudhuria au pengine kufika tu hapo Diamond Jubilee. Kunako

3. KAMATI YA MAGEUZI NA UJIO WA CHAMA CHA NCCR -MAGEUZI NA VYAMA VINGINE
Februari 15/1992 NCCR [Kamati] ilijibadilisha jina na malengo na kisha kuwa Chama Cha Siasa kwa jina la National Convention for Construction and Reform (NCCR)- Mageuzi. Kwa hiyo NCCR [Kamati] ceased to exist right from 15/02/1992. Lengo lilikuwa ku-maintain jina (NCCR) na historia ya harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini (Mageuzi).

Wakati huo, kwa sababu mbali mbali, wakongwe akina Mzee Fundikira, Mzee Kasanga Tumbo, na mzee Kasela Bantu walishaamua kuondoka na kuanzisha chama chao cha UMD kikiongozwa na Chief Fundikira, James Mapalala akishirikana na Alec Chempnda (huyu sijui iwapo bado anaishi) walianzisha Chama Cha Wananchi (CCW), baadaye kiliungana na KAMAHURU na kujiita jina la CUF.

Mch. Christopher Mtikila akishirikiana na Kaoneka, Mwinjilist Kamara Kusupa, Mwingandoshi (apumzike kwa amani) na mtu mmoja aliyeitwa Kabati walianzisha chama chao kikiitwa Chama Cha Demokrasia (CCD) na kisha baada ya kugombana na Mtikila CCD ilibaki na Mwenyekiti wake Kabati, Mch. Mtikila (mjanja) alibadirisha CCD kutoka jina la Kiswahili kuwa jina la Kiingereza (Democratic Party /DP).

Kaoneka baadaye aliajiriwa Chadema kwa nafasi ya usimamizi wa ofisi (office supervisor), Kisutu, Dar es Salaam, na Mtikila aliendelea na DP (CCD kwa Kimombo) yake, kwanza akiwa mshauri na baadaye Mwenyekiti wa taifa hadi mauti yalipo mfika 2015.

Mzee Mwakitwange hakuelewana na wafuasi wa Mzee Kambona wakiongozwa na Mzee Dustan Lifa Chipaka na hivyo kuzaliwa vyama viwili, Popular National Party (PONA) kikiongozwa na Mwenykiti wake Mzee Mwakitwange na Katibu Mkuu Peter Terry (sijui kama bado anaishi).

Kundi la wafuasi wa Mzee Kambona likiongozwa na Mzee Chipaka lilianzisha chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA). Aidha kabla ya Julai 1992 vilianzishwa vyama vya Liberal Democratic Party (LDP) kilichoongozwa na Mzee Hilary Mapunda, aliyekuwa mhadhiri wa Chuo cha Chama Kivukoni;

National Reconstruction Alliance (NRA/NAREA) kilichoongozwa na Mzee Abubakar Olotu na baadaye Profesa Kigoma Ali Malima (muda mfupi sana-apumzike kwa amani); na chama cha National League for Democracy (NLD) kilichoongozwa na Dr. Emmanuel Makaidi (apumzike kwa amani) hadi alipofikwa na mauti mwaka 2015.

Vyama vingine vilianzishwa mara baada ya sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya 1992. Vyama hivyo ni pamoja na chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kilichoasisiwa Bwana Leo Lwekamwa.

4. UJIO WA CHADEMA NA MZEE EDWIN MTEI
Kunako April 1992, Prince Bagenda akiambatana na James Mbatia alitumwa na viongozi wenzake kumfuata Mzee Mtei Nyumbani kwake, Usa River, Arusha. Kabla ya hapo kulikuwa kumefanyika mazungumzo ya simu kati ya Mzee Mtei na Mabere Marando, kumshawishi mzee Mtei ajiunge NCCR-Mageuzi.

Mzee Mtei alishauri apelekewe Katiba na andiko la Seraza Chama cha NCCR- Mageuzi. Kwa hiyo, safari ya Bagenda ilikuwa kwenda kuongea naye ana kwa ana lakini pia kumpatia nyaraka za chama alizokuwa amesahuri azisome na kuzielewa kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga NCCR-Mageuzi.

Baada ya Mzee Mtei kupokea nyaraka hizo aliahidi kuja Dar es Salaam kukutana na 'vijana' na kisha kuwapa msimamo wake. [sikumbuki tarehe, ila ni mwezi huo huo wa Aprili /92] Marando, Bagenda na Chimoto walipopata taarifa kuwa Mzee Mtei tayari alikuwa amerejea Dar es salaam walifanya miadi kwenda kumwona na kisha kupata jibu lake, wakiwa na matumani kuwa angejiunga na chama cha NCCR -Mageuzi.

Walipofika nyumbani kwake na kumkuta, Mzee Mtei aliwakaribisha na kisha kuwaambia maneno haya, "kuna watu wenye means and substance wamekuwa wakinishawishi kuanzisha chama. Nimeamua kuanzisha chama kwa hiyo ninyi vijana mwende mvuje chama chenu kisha mje kujiunga kwenye chama change nitakachoanzisha".

Kwa kauli hiyo vijana hao walipoa, ila Marando alimjibu na hapa ninamnukuu, "Mzee Mtei tumetumia muda, akili, nguvu, pesa na kunyeshewa na mvua nyingi wakati wa kuanzisha chama cha NCCR -Mageuzi, tunakushauri uendelee na juhudi zako ila tunaamini huko tuendako mvua itakunyeshea pia, na ikiwa hivyo, kisha ukitafuta mahali pa kujikinga tutakukaribisha kujikinga pamoja".

Kesho yake tulipata taarifa kuwa saa 5 mchana juu ya alama Mzee Mtei alikuwa aongee na waandishi wa habari pale Motel Agip. Mwandishi aliyekuwa ametumwa na NCCR-Mageuzi alirejesha feedback kuwa Mzee Mtei akiwa na marafiki zake wa enzi zake - Bob Makani, Edward Barongo na wengineo, alikuwa ametangaza kuanzisha chama mara baada ya kuwepo kwa sheria ya kuruhusu Tanzania kuwa nchi ya vyama vingi vya Siasa.

Kwamba chama hicho kingeitwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); na kwamba kwenye mkutano huo waasisi wote waliokuwepo walikuwa wamevaa sare - walifunga tai, makoti yakiwa yamening’inizwa ukutani na suruali zao zikining'nia kwenye suspenders.

Taarifa hiyo haikushangaza viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi ila nyaraka walizopewa waandishi wa habari zilikuwa ni zile zile (copy right) Prince Bagenda alizompelekea Mzee Edwin Mtei Nyumbani kwake Usa River - Katiba na Sera za NCCR Mageuzi isipokuwa kubadilishwa (replace with) maneno 'NCCR-Mageuzi' kwa 'CHADEMA' basi.

Ukiangalia nembo ya NCCR -Mageuzi utaona kuwa hata maneno Demokrasia na Maendeleo yalitolewa humo. Maneno ya Mzee Mtei na wenzake kwa jina CHADEMA ni [CHA] tu, DEMA ilichomolewa kwenye nembo ya NCCR-Mageuzi.

Hii ni historia kwa kifupi sana ya kutafutana na kukutana kwa waasisi wa mageuzi wakati wa harakati za awali za kuasisiwa [tena] kwa mfumo wa siasa za vyama vingi hapa nchini Tanzania.
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,767
2,000
Nilikuwa sijaiona hii...hongera sana Mbase1970 ila nina ushauri moja tu, hiyo historia inatakiwa ianzie miaka mitatu nyuma 1988 ikielekea 1989 na hapo usisahau ushiriki wa magazeti kama Family Mirror la Kiingereza na Shaba la Kiswahili. Pia usisahau kunukuu kauli ya kijana Mabere Marando dhidi ya Baba wa Taifa kwamba kafilisika kisiasa, kauli iliyowaacha wananchi wengi midomo wazi.
 
Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000

Historia nzuri ,Sijamuona Augustine Mrema hapo.
 
Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
Historia nzuri ,Sijamuona Augustine Mrema hapo.
Mrema siyo mhenga wa Mageuzi ni kama baada ya miaka 15 kuanzia sasa mtu akakuuliza yu wapi Lowasa, akma Sumaye, Wakati juhudi za mageuzi zinaendelea Mrema alikua naibu Waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani na mpiga zumari wa ccm pamoja na kina Lowasa na marehemu Kolimba wote wakisema watanzania wanataka ccm iendelee kama chama pekee na vitisho kuwa damu zitamwagika kama kukiwa na vyama vingi. Mrema tulikua tunamuita mzee wa siku saba tuonane Moshi.

Hii historia ni nzuri kwa vijana walioanza kufuatilia mageuzi July 2015,ili waelewi kina nani hasa vinara wa mageuzi
 
Ha ha ha wewe ni mhenga mkuu. Tukisema hivyo itabidi tuende mpaka miaka ya sitini baada ya Nyerere kufanya nchi ya chama kimoja hapo ndipo tutawaona wana mageuzi wa kweli kama mzee James Mapalala na mzee Abdalah FUNDIKIRA na Kina Kasanga Tumbo. Ila mtu yeyote ambaye ni TIS simuamini kabisa na mimi nadhani Marando ni chanzo cha kuuvuruga upinzani, ndiye aliyetusababisha tukose katiba mpya maana alituingiza katika uchaguzi wa mwaka 1995 huku akijua kabisa lengo la NCCR lilikua kudai katiba na katiba ya wakati huo ilikua ya ccm.
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,767
2,000
Historia nzuri ,Sijamuona Augustine Mrema hapo.
Hakuna Waziri wa Mwinyi aliyeyapiga vita mageuzi kama Augustine Lyatonga Mrema wakati huo akiwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani. Mrema aliliongoza Jeshi ya Polisi na hasa FFU kuwashambulia, kuwapiga na kuwatesa wana Mageuzi akidai kuwa yeyote anayeunga mkono mfumo wa vyama vingi ni mwehu.

Augustine Lyatonga Mrema aliwapa vilema vya maisha Watanzania wengi kwa kosa tu la kudai demokrasia zaidi na uhuru wa mawazo. Katika uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo mpya mwaka 1995, alipoona nafasi yake ya kuteuliwa na CCM ni finyu alijiuzulu na kula matapishi yake kwa kujiunga na upinzani.

NCCR-Mageuzi walimpokea akiwa maefuatana na wanachama kadhaa kutoka CCM na kuchukua fomu kugombea Urais. Mtu mwingine aliyedandia upinzani mwaka huo ni pamoja na Dr. Slaa baada ya kutemwa na CCM kugombea Ubunge wa Karatu. Yeye aliamua kujiunga na Chadema na kufanikiwa kuutwaa ubunge.
 
Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000
Mrema siyo mhenga wa Mageuzi ni kama baada ya miaka 15 kuanzia sasa mtu akakuuliza yu wapi Lowasa, akma Sumaye, Wakati juhudi za mageuzi zinaendelea Mrema alikua naibu Waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani na mpiga zumari wa ccm pamoja na kina Lowasa na marehemu Kolimba wote wakisema watanzania wanataka ccm iendelee kama chama pekee na vitisho kuwa damu zitamwagika kama kukiwa na vyama vingi. Mrema tulikua tunamuita mzee wa siku saba tuonane Moshi.

Hii historia ni nzuri kwa vijana walioanza kufuatilia mageuzi July 2015,ili waelewi kina nani hasa vinara wa mageuzi
OK.
 
Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000
Mzee
Hakuna Waziri wa Mwinyi aliyeyapiga vita mageuzi kama Augustine Lyatonga Mrema wakati huo akiwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani. Mrema aliliongoza Jeshi ya Polisi na hasa FFU kuwashambulia, kuwapiga na kuwatesa wana Mageuzi akidai kuwa yeyote anayeunga mkono mfumo wa vyama vingi ni mwehu.

Augustine Lyatonga Mrema aliwapa vilema vya maisha Watanzania wengi kwa kosa tu la kudai demokrasia zaidi na uhuru wa mawazo. Katika uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo mpya mwaka 1995, alipoona nafasi yake ya kuteuliwa na CCM ni finyu alijiuzulu na kula matapishi yake kwa kujiunga na upinzani.

NCCR-Mageuzi walimpokea akiwa maefuatana na wanachama kadhaa kutoka CCM na kuchukua fomu kugombea Urais. Mtu mwingine aliyedandia upinzani mwaka huo ni pamoja na Dr. Slaa baada ya kutemwa na CCM kugombea Ubunge wa Karatu. Yeye aliamua kujiunga na Chadema na kufanikiwa kuutwaa ubunge.

MZEE! Hii ndiyo ... !Hakika Umehifadhi Historia! Alienda UDSM kuwaonya Wanafunzi juu ya Ujio wa Mageuzi nchini kuwa ni hatari na yanalenga kuleta machafuko nchini! 95 akawa mgombea kwa kupitia hayo mageuzi.
 
Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
2,000
Mzee

MZEE! Hii ndiyo ... !Hakika Umehifadhi Historia! Alienda UDSM kuwaonya Wanafunzi juu ya Ujio wa Mageuzi nchini kuwa ni hatari na yanalenga kuleta machafuko nchini! 95 akawa mgombea kwa kupitia hayo mageuzi.
Ndiyo maana sisi wengine tukisema hakuna upinzani tunaitwa ccm lakini ukweli tunaujua na jinsi tulivyohenyeshwa na hawahawa leo wanasujudiwa na vijana wanajiita makamanda. Kwamimi mtu wa mageuzi aliyekua wa kweli ni marehemu mchungaji mtikila. Maana hakuwaamini kabisa kina marando lakini wengi walimuona mwehu.

Leo kina Lissu wanawaita mafisadi wakati Mtikila alianza vita hiyo miaka ya mwanzo kabisa kwa kuwaita MAGABACHORI na sisi wengine tulihamasika vibaya na baadhi yetu kuanza vurugu kupiga magari ya wahindi kwa kutomuelewa alikua na maana gani. Labda sababu gabachori tuliona kama ni kihindi watu wakawavamia hao tu.

Usiende mbali kwani Masha alifanya nini kwa wapinzani na yeye leo ati ni kamanda. Simpendi Mkapa lakini wakati mwingine nakubaliana naye kutuita wapumbavu maana ni wapumbavu kweli kweli tunawezaji kusahau watu kama kina Masha na Sumaye leo hii tuwasujudie badala ya kuwapeleka mahakamani pamoja na mkapa na kikwete kwa kosa la unyanyasaji wa upinzani? Watu wamekua kama ccm zidumu fikra za kiongozi Mbowe hata kama ni za kijinga.

Badala ya kung'ang'ania makapi ya ccm kwanini wasitayarishe damu mpya zisizo na uchafu wa ccm? Ama kwanini wasiwashawishi ccm wasafi kama kina Bashe na wengine. Sidhani kama Mwalimu aliposema mpinzani wa kweli atatoka ccm alimaanisha kila kapi kama ingekua hivyo basi angemwacha Mrema ashinde urais mwaka 1995 maana alitoka ccm.
 
Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000
Ndiyo maana sisi wengine tukisema hakuna upinzani tunaitwa ccm lakini ukweli tunaujua na jinsi tulivyohenyeshwa na hawahawa leo wanasujudiwa na vijana wanajiita makamanda. Kwamimi mtu wa mageuzi aliyekua wa kweli ni marehemu mchungaji mtikila. Maana hakuwaamini kabisa kina marando lakini wengi walimuona mwehu. Leo kina Lissu wanawaita mafisadi wakati Mtikila alianza vita hiyo miaka ya mwanzo kabisa kwa kuwaita MAGABACHORI na sisi wengine tulihamasika vibaya na baadhi yetu kuanza vurugu kupiga magari ya wahindi kwa kutomuelewa alikua na maana gani. Labda sababu gabachori tuliona kama ni kihindi watu wakawavamia hao tu.

Usiende mbali kwani Masha alifanya nini kwa wapinzani na yeye leo ati ni kamanda. Simpendi Mkapa lakini wakati mwingine nakubaliana naye kutuita wapumbavu maana ni wapumbavu kweli kweli tunawezaji kusahau watu kama kina Masha na Sumaye leo hii tuwasujudie badala ya kuwapeleka mahakamani pamoja na mkapa na kikwete kwa kosa la unyanyasaji wa upinzani? Watu wamekua kama ccm zidumu fikra za kiongozi Mbowe hata kama ni za kijinga. Badala ya kung'ang'ania makapi ya ccm kwanini wasitayarishe damu mpya zisizo na uchafu wa ccm? Ama kwanini wasiwashawishi ccm wasafi kama kina Bashe na wengine. Sidhani kama Mwalimu aliposema mpinzani wa kweli atatoka ccm alimaanisha kila kapi kama ingekua hivyo basi angemwacha Mrema ashinde urais mwaka 1995 maana alitoka ccm.

Mbase 1970 ! Umenena vema Mkuu.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,736
2,000
Ukiangalia kwa makini huwezi kuona Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa imesaidiaje Taifa, sana sana wanaofaidika ni mtu mmoja mmoja na baadhi ya familia.

Kwa mfano, angalia baadhi ya vyama vya upinzani ni vya kifamilia zaidi ukienda Vunjo na Moshi vijijini unakuta mtu na wifi yake wameteuliwa kugombea ubunge kupitia chama kimoja, kadhalika Morogoro Kulwa na Doto wote wameteuliwa.

Ndio najiuliza lengo la vyama vingi ni nini?

Hata uchaguzi wenyewe haueleweki, yaani mtu anapita bila kupingwa? Hata Mwalimu Nyerere na mzee Mwinyi wakati wa chama kimoja hawakuwahi kupita bila kupingwa, tuliwapigia kura lakini leo msimamizi wa Uchaguzi anatuteulia Mbunge.

Kwa mtu mmoja dhambi iliingia duniani na kwa mtu mmoja binadamu walikombolewa kutoka dhambini, Siasa isitufarakanishe Watanzania tupendane.

Nawatakia Ijumaa kareem.

Maendeleo hayana vyama!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom