Kwa vigezo hivi tupimeje mafanikio ya serikali?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Wadau,

Katika mfumo wa uendeshaji wa serikali, serikali iliyo serious huunda au kuimarisha taasisi zake ambazo hutumika kama watchdogs ili kuitazama na kuikumbusha katika maeneo muhimu.

Taasisi muhimu ambazo zipo kikatiba katika kuikumbusha Serikali, baadhi ni kama Bunge, Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Tume ya Utawala Bora na Haki za Binadamu.

Taasisi hizo zilifanya kazi nzuri awamu ya Serikali iliyopita. Tulishudia Bunge lenye nguvu na uwezo wa kuihoji Serikali na kuishauri. Tulipata fursa ya kutazama moja kwa moja. Tulishudia Ofisi ya CAG ikiwezeshwa kwa kutengewa bajeti ya kutosha kuweza kukagua hesabu za Serikali kuu, Serikali za Mitaa na hata Mashirika ya umma pale ilipoagizwa kufanya hivyo.

Awamu hii, pamoja kujitahidi kuthibiti raslimali za Serikali na kuziba mianya ya matumizi ya Serikali; bado kwa upande mwingine inajihujumu ama kwa kutokujua au kwa lengo maalumu.

Bunge. Ule uhuru na uwezo wa Bunge kuihoji, kuishauri na kuthibiti Serikali ni kama haupo tena. Bunge limeanza kutumika kuilinda Serikali na kuwathibiti Wabunge kutimiza wajibu huo na kama vile haitoshi, wananchi wamekatiwa fursa ya kuwasikia Wabunge wakati wa mikutano ya Bunge kwa matangazo mubashara!

Ofisi ya CAG. Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali imepunguziwa bajeti kwa kiasi kikubwa, CAG binafsi amekaririwa akilalamikia hili! Sasa Serikali na Bunge watawezaje kujua yanayoendelea kwenye Wizara na Taasisi zake?

Udhibiti wa Vyombo vya Habari. Katika kipindi cha ndani ya mwaka mmoja magazeti na redio vimeadhibiwa kwa kufungiwa kwa madai ya kumkashifu Rais na Serikali.

Ktk muda huu mfupi, tumeshuhudia pia matumizi makubwa ya Polisi katika mambo ya kisiasa yasiyo na tija zaidi ya kutengeneza tension isiyo ya lazima kwa masuala ambayo awali Polisi hao hao waliwaita wapinzanzani wa Serikali na kukubaliana namna ya kuendesha harakati zao za kisiasa.

Tumewahi kushuhudia madhira ya Polisi kutumia nguvu pasipo sababu dhidi ya wapinzani na kusababisha vifo kwa watu wasiohusika wala kuwa na hatia kule Morogoro, Iringa, na Arusha. Kutunishiana misuli kwa Polisi na wapinzani, licha ya kuleta mtanziko usio na sababu wala tija, ulitoa mwanya kwa watu waovu, majambazi nk kufanya uovu kwa urahisi zaidi kama tukio la kushambuliwa waumini wakiwa Kanisani Arusha.

Hata tukio la Polisi watu kuuwawa majuzi huko Mbande, Mbagala yaweza kuwa ni sababu ya mwanya uliosababishwa na mtanziko kati ya Polisi na wapinzani. Taratibu tunaanza kujiondoa kutoka kwenye utaratibu wa majadiliano na kuwa waumini wa kutumia nguvu. Hili ni kwa pande zote, watawala na wapinzani.

Najaribu kuwaza kwa sauti, utegemezi huu wa Serikali kuacha kuziwezesha taasisi na kuanza kutegemea 'vijana ' wa Rais kumpa taarifa, kunatosha kujua mambo yote yanayoihusu Serikali na Taasisi zake? Kama kila kitu kinaanzia Ikulu, kuna umuhimu gani wa kuwa na taasisi nyingine ambazo ziliundwa kwa lengo la kusaidia Utawala bora? Ikitokea bahati mbaya Rais wetu (Mungu aepushe mbali na tuendelee kumuombea) kwasababu za kiafya akadhindwa kutimiza majukumu yake ya Kikatiba, hizo taasisi zilizodorora zitaweza kutukwamua na athari hiyo?

Mungu atusaidie na kutuwezesha kuendesha mambo yetu kwa busara na amani ya kudumu.

Vv
 
Back
Top Bottom