Kwa vifo hivi vya kisiasa hofu ya Mungu imetoweka turudi kwenye mstari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa vifo hivi vya kisiasa hofu ya Mungu imetoweka turudi kwenye mstari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Jul 17, 2012.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi najiuliza hivi Watanazania tumefikia hatua hata ya kutomwogopa Mungu kiasi sasa kuua watu kwa manufa ya kisiasa ni jambo la kawaida kabisa. Hivi ndugu zetu wa CCM madaraka ya damu mnayongangani kwa damu za watu itawasaidia nini hamjui mnaleta laana kwenye nchi. Ndugu zangu wachaeni kufikiri kuwa Mungu ameenda likizo ni hatari sana mambo yanayofanywa na CCM. Mfahamu kuwa hakuna laana mbaya kama kuuwa mtu kwa kuwa Mungu mwenyewe kwenye kitabu kitakatifu anasema auae kwa upanga atakufa kwa upanga.

  Nawashanga sana viongozi wa dini wanaoishabikia CCM hivi mnamtumikia Mungu yupi maana wapo Miungu wengi lakini Mungu wa haki na amani yupo mmoja na anatabia ya kukataa uovu yupo upande wa haki mnakaa kimya CCM inangamiza watu Mungu wenu ni yupi maana nuru na giza haviwezi kukaa pamoja.

  Mmesahau kuwa madaraka ya damu ni laana kwa nchi na chukizo kwa Mungu. Ni vizuri Watanzania tujenge utamaduni tushindane kwa hoja tukishindwa tuwaache walioshinda kwa hoja waongoze nchi na sisi tujipange upya. Mnasababisha Wazungu watuone waafrika siobinadamu utapinga vipi ukifananishwa na nyani maana huna akili kama sio nyani unawezaje kuuwa mwenzio kwa ajili ya vitu vya kupita vya siasa.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni mbinu chafu za serikali ya ccm kutaka kubaki madarakani kwa nguvu. Wanasahau kuwa hakuna serikali duniani kote iliyodumu madarakani kwa nguvu.

  Itafanya hivyo kwa muda tu, muda ambao utaamsha zaidi hasira za wananchi, na mwisho wake utawadia. Mifano ipo mingi, Libya, Misri, Kongo ya Mobutu, Liberia, na kwingine duaniani.

  CCM inaweza kuendelea kubaki madarakani iwapo tu itajirekebisha na kuboresha maisha ya wananchi wake, sio kwa kuendelea na mauaji ya mawe, kuteka, na silaha za moto.
   
Loading...