Kwa uzoefu wako ni biashara gani yenye mtaji mdogo lakini faida ni kubwa

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
77
150
Rejea kichwa apo juu,tusaidiane wadau
Biashara ya usafi

1.kutatua changamoto ya uchafu sugu katika Tiles na Masink

Gharama ya dawa ya kung'arisha Tiles na Masink Lita 1 ni 7,000

Gharama za usafi anazo lipia mteja wako

Kung'arisha sink 1 ni 10,000 na dawa Lita 1 inatumika kwa Masink 5

Kung'arisha Tiles za ukutani na za chini

Utatumia dawa nusu lita

Na gharama anazo lipia mteja wako kwa kazi hii ni 25,000 mpaka 35,000 kwa bathroom 1

2.Kusafisha sofa za kitambaa

Gharama za dawa ya Kusafishia Sofa ni 12,000 kwa Lita 1

Mteja analipia kuanzia 50,000 mpaka 80,000 kwa sofa set 1 ya watu 5 mpaka 8

Gharama za usafi zita ongezeka au kupungua kulingana na makubaliano yenu na mteja wako.

3.Kutengeneza dawa za Kung'arishia Tiles na Masink na kuuza

Mtaji wa Kutengeneza hizi dawa ni 55,000

Una pata Lita 30

Kila lita I inauzwa 7,000 na utatumia 20,000 kwa ajiri ya package na kuweka stika kwenye bidhaa zako

Hizo ni baadhi tu zipo pia dawa za Kusafishia Sofa unaweza Kutengeneza kwa gharama ndogo na ukapata faida kubwa.
 

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
15,183
2,000
Zipo,ila utatumia nguvu nyingi sana kupata faida kubwa; mfano kuuza kahawa iliyopikwa, itakuitaji utembee umbali mrefu kwenye misongamano ya watu ili uweze kuuza
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,887
2,000
Hey, I could show ya how to juggle anything and make it double
Weed, blow, real estate, liquor sto' wit' no trouble.
 

Mashaurijr

Senior Member
Oct 8, 2016
110
250
Mkuu mambo vp. Nilikuwa na maduka ya rejareja mawili . Moja nikaliuwa kutokana na kuugua , na changamoto za Mmiliki wa fremu, by laws za ulinzi , kuharibu kwa mfanyakazi, nikawa nimetaka kubadili biashara na fremu nilikuwa nishapata ila mwenye fremu nilimpa idea yangu nini nataka nifanye hapo , siku ya kulipia kufika nikakuta kaiba plan yangu , nilipanik nikawa nimepeleka hela kwenye ujenzi ambao haukwenda mbali nikajishtukia nimedondokea kwenye hali ngumu sana kiuchumi depression inanitafuna afya inakaa vibaya duka lililobaki lina mtaji unaozunguka 6.7M ila lina mfanyakazi anafanya vizuri sana wateja wamemzoea na anajituma sana, kiasi kwamba nakuwa na mashaka ukimtoa lazima duka liyumbe kwanza kutokana na kuzoeleka kwake na uwezo wake kwenye competition, sasa nipo tu sina ishu yoyote nikitegemea tena duka kuishi hilo moja jambo nisilolipenda natamani kuajiriwa angalau faida ninayozalisha dukani ikae benki nije nifungue biashara nyingine na sio mimi kuitumia
Na pia sijazoea kukaa free nimepona sasa natamani kazi yoyote ile itakayonipa kula na matumizi mengine, nakusave hata kidogo ili niweze kurudi kwenye hali yangu kiuchumi nahitaji nitoke dar mwenye nafasi yoyote ya kazi mimi ni mpambanaji huwa sijali ndio maana siwezi kukaa bila kazi . Naugua nikikaa hivi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom