Uzandiki gani mkuu? Kutofautiana mawazo na mtu si kosa!!! Tatizo ni watu wanaotaka tufanane mawazo!!!! Haiwezekani!!!!!Japokuwa uteuzi huwa ni bakshishi za kisiasa kwa watu wa karibu wa mwenye mamlaka lakini teuzi lazima zizingatie maadili,utii na sifa njema.
Urais ni taasisi na sio mtu mmoja tu. Kama January alionyesha uzandiki na hila kwa rais aliyepita na kisha akanaswa akimsengenya kimajungu mkuu wa nchi, huyu anafaa kurudi kwenye kabineti tena?
Maana ilidhihirika wazi kuwa hakuwa na utii kwa rais. Na ndio maana alidiliki kupika majungu.
Clip zilirushwa wazi na akaomba msamaha. Sasa leo ofisi ya rais imeona vipi kuwa anafaa? Japokuwa ni mzandiki?