Kwa uwezo wake mkubwa wa Akili, Kuchambua 'Masuala' na Kujieleza kwa Kujiamini Waziri wa Afya Dkt. Gwajima umeshauteka Moyo wangu

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Hakuna Kitu ambacho GENTAMYCINE nakipenda kwa Mwanamke na pia huwa natamani awe nacho kama Uwezo mkubwa wa Akili, Kuchambua Masuala ( Issues ) tena 'Professionally' kabisa na awe na Kiwango kikubwa cha 'Confidence' hasa akiwa anazungumza au anawasilisha Jambo ( Kitu ) katika Hadhira ( Public )

Kama kuna Waziri ambaye kwa sasa nikisikia tu anazungumza ( hasa Runingani ) achilia mbali katika Redio huwa napenda Kuacha ninachokifanya kwa wakati huo na Kumsikiliza tena huku Moyo wangu ukiwa Unasuuzika na Kushiba Madini yake ya Kiufafanuzi basi ni Waziri wa Afya Gwajima.

Nichukue tu nafasi hii adhimu Kumpongeza Mumewe kwa Kumwambia kuwa Hongera zake kwa kumpata Mke ambaye ni Intelligent naturally, Educated and Orator kama Waziri wa Afya Gwajima na hakka Mumuewe popote alipo anapaswa ajivunie kabisa.

Kwa sasa kwakuwa nahitaji kupata Mwanamke mwenye Sifa kama alizonazo Waziri wa Afya Gwajima awe 'Mamsampu' wangu ngoja nianze Utaratibu wa Kutembelea Mkoa na Kijiji anachotoka Waziri Gwajima kwani huenda nami nikabahatisha kupata 'Masalia' ya Wanawake 'Werevu' kama Waziti Gwajima baada ya Kuwatafuta mno bila Mafanikio hapa Juliana, Afrika Sana, Beach Kidimbwi, Brazil Pub Tegeta, Kwa Mpalange, Jackie's Pub Oysterbay, Kimboka Buguruni na pale Kahumba Morogoro.

Ukiwa na Mke kama Waziri wa Afya Gwajima ni raha tupu kwani kama Mume utakuwa huna Wasiwasi wa Kuzaa Watoto 'Intelligent' kama Mama yao japo kwa Kiasi fulani hata Wewe Mume ( Baba yao ) pia unatakiwa usiwe ama Ngumbaru ( Mjinga ) au Popoma ( Mpumbavu ) kwani utaharibu kabisa 'Chemistry' ya Kizazi chako ( Watoto )

Heko nyingi sana Kwako Waziri Gwajima.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,170
2,000
Ila kama ni yule yule slyeendesha wizara awamu ya tano, ndio huyu huyu aliyetema cheche kwenye uzinduzi wa chanjo, anastahili sifa zako mkuu. Ana ujasiri usio kifani. Yaani ni zaidi ya mwamba.
 

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Ila kama ni yule yule slyeendesha wizara awamu ya tano, ndio huyu huyu aliyetema cheche kwenye uzinduzi wa chanjo, anastahili sifa zako mkuu. Ana ujasiri usio kifani. Yaani ni zaidi ya mwamba.
Ukiona GENTAMYCINE namkubali Mtu basi jua 99.9% nimeshajiridhisha nae pasi na shaka juu ya Uwezo wake.

Sina tabia ya kupenda 'vibovu vibovu' kama labda kuishangilia Timu mbovu ya Manchester United badala ya Liverpool FC yangu.

Si unaona hata leo pia nimeupongeza Uongozi wa Simba SC kwa Kumteua Kaka yangu katika Fani Ezekiel Kamwaga kuwa Kaimu Msemaji wa Simba SC badala ya Yule 'Mzungu Pori' Msaliti aliyekuwa anatumiwa na Yanga SC Kutumaliza?

Na ndiyo maana pia nampenda Fundi Lionel Messi badala ya Mbovu Christiano Ronaldo. Nampenda Mtandao wa JamiiForums kuliko hata Facebook na Istagram.

Nikikukubali jua upo vizuri sana Mkuu.
 

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Tamko la kijinga kabisa limekwepa maswali ya mingi
1. Afrika ni nchi ipi iliyofanikiwa baada ya kuchanja?

2. Ni kwa nini tupewe chanjo na wazungu waliokufa sana na corona wakati sisi hatujaarithiriwa kihivyo
Acha Upopoma Mkuu kwani kuna mahala umeshikiwa Jiwe Kubwa la FATUMA na Kushurutishwa upigwe hiyo Chanjo?

Wanafiki wakubwa nyie sasa tunawaombeni nyote ambao leo hii mnaibishia na kuikataa hii Covid-19 Johnson & Johnson Jab ikipatikana Chanjo ya UKIMWI ( Dally Kimoko ) muibishie na muikatae hivi hivi tu sawa?
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,170
2,000
Tamko la kijinga kabisa limekwepa maswali ya msingi
1. Afrika ni nchi ipi iliyofanikiwa baada ya kuchanja?

2. Ni kwa nini tupewe chanjo na wazungu waliokufa sana na corona wakati sisi hatujaarithiriwa kihivyo

Narudia tena, kama ni waziri huyu huyu aliongoza hii wizara wakati wa awam ya tano na mambo yalienda kama tulivyoshuhudia, na waziri huyu huyu leo amesimamia uzinduzi wa chanjo...anahitaji nishani ya ujasiri.
 

Paroco

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,984
2,000
Mimi nimejikuta navutiwa nae awe bimdogo wangu. Kanajiamini balaaa alafu hayupo complicated mawigi nini mamekup. Yupo simple balaaa.

Ni wife material yule😊😊😊😊😊😊

Wadau mwenye namba yake basiπŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,889
2,000
Acha Upopoma Mkuu kwani kuna mahala umeshikiwa Jiwe Kubwa la FATUMA na Kushurutishwa upigwe hiyo Chanjo?

Wanafiki wakubwa nyie sasa tunawaombeni nyote ambao leo hii mnaibishia na kuikataa hii Covid-19 Johnson & Johnson Jab ikipatikana Chanjo ya UKIMWI ( Dally Kimoko ) muibishie na muikatae hivi hivi tu sawa?
Ukimwi una miaka mingapi na majaribiio ya chanjo yote yamefeli?

Kwanini hii imekuja chapu kwa haraka?

Eti teknolojia ndo imewezesha chanjo kuoatikana haraka. Hiyo teknolojia inaimudu korona na siyo malaria na ukimwi?

Sometimes chanjo ya korona inaacha mapengo mengi ya maswali na majibu kiasi kwamba hakuna anayeyajaza mapengo hayo.

Leo Marekani ambayo waliotumia chanjo ya J&J ni 3% tu, kisha wamikataa. Halafu huyo mchawi wenu anacheza mbele zetu akifurahia kuja kwa chanjo iliyokataliwa na walioitengeneza.

Hebu watanzania tuendelee kutafuta japo tone la ukweli kuhusu hizi chanjo.

Haiwezekani huko walikoanza chanjo hawajapata nafuu ya maambukizi, sisi tulio nafuu tunakimbilia chanjo.

Bado ninamwelewa Magufuli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom