Kwa uteuzi huu wa DC Longido, UKAWA wajiandae kupoteza Jimbo

Huwa kuna majina mawili yanawachanganya sana waandishi maeneo mbali mbali. Benidict Ole Nangoro na Onesmo Ole Nangole. NANGORO aliwahi kuwa naibu waziri kilimo, mifugo na uvuvi enzi za Kikwete na ni Mbunge wa kiteto aliyepoteza nafasi yake. NANGOLE ni mwenyekiti wa CCM wa zamani wa mkoa wa Arusha aliyehamia CHADEMA na sasa ni Mbunge wa Longido aliyetenguliwa ushindi wake na mahakama kuu Kanda ya Arusha. Natumai waandishi na wadau mbalimbali hamtochanganya tena majina haya mawili.
Mkuu hivi Ubunge wa huyu bwana umefikia wapi?Je alikata rufaa kuhusu kutenguliwa kwa ushindi wake?Muendelezo vipi juu ya hii kesi?Kama una taarifa kuhusu "status" ya jambo hili naomba unijuze mkuu free freed
 
Kama hawajachimba hata kisima cha maji kwa nini wasipigwe Chini

Wapinzani wao wanajua kuandamana tu.
 
Mkuu hii si Arusha ile ya "R-Chuga" hii ni ile ya Wafugaji,ipo kuleeee mpakani na Kenya,Jamii hii ya wafugaji itawekwa sawa na wote wataelekea kibra!!Hili jimbo lina hathati kubwa sana ya kurudi CCM
TUTARUDI HAPA BAADA YA UCHAGUZI Akida MALCOM X
Mutaua tu watu lakini mumechokwa.
 
Uteuzi wa wakuu wa Wilaya umeshafanyika,Rais ameteuwa kwa kiasi kikubwa makada watiifu wa chama Tawala,wengi wao wakiwa vijana na wenye elimu ya kutosha.

Moja ya majukumu waliyopewa leo ni kuhakikisha ilani ya chama Tawala inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yao ya utawala.Moja ya kuhakikisha ilani inatekelezwa ni kuhakikisha pia chama tawala kinapata nguvu na "mvuto" katika wilaya walizopewa.Kazi kubwa ni kwa wakuu wa wilaya ambapo majimbo/wilaya zao zipo chini ya UKAWA;Kwa mfano Wilaya Ubungo ndugu Polepole ni juhudi zake "kumpoteza" Kubenea na kuhakikisha Jimbo linarudi CCM mwaka 2020 mara baada ya kuwa chini ya CHADEMA kwa miaka 10.

Huko LONGIDO kwenye uchaguzi wa marudio amepelekwa DANIEL GODFREY CHONGOLO,huyu ni "mwanafunzi" na "mshirika" wa karibu sana wa NAPE MOSES NNAUYE,pale Makao Makuu ya Chama Chongolo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kilichokuwa chini ya idara ya Sera na Uenezi(Kitengo cha Propaganda).

Huyu ni kada kindakindaki aliyekuwa ameambatana na Magufuli katika kampeni nchi nzima,yeye akiratibu kitengo cha habari kwa umma zikiwemo picha kurushwa mitandaoni,habari nzuri "kumpamba" mgombea wa CCM kurushwa magazetini na kwenye Tv.Huku kwenye Tv alimkamata vizuri sana Emmanuel Buhohela wa ITV aliyekuwa anafukia mashimo ya Spencer Lameck(naye wa ITV) aliyekuwa anarusha habari za mgombea wa UKAWA.Kazi nzuri ya Buhohela imempa "ulaji" Kurugenzi ya Mawasialino IKULU.

Chongolo ni mzoefu sana wa chaguzi za marudio,amekuwapo Busanda,Igunga,Arumeru Mashariki,Kiteto na Kalenga.Uwepo wake Longido huku kukiwa na maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa jimbo hilo ni mkakati tosha wa chama tawala kulikomboa jimbo.Kama kada na kijana mtiifu,chini ya mamlaka ya kidola na kiserikali kama Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya,sioni wapi UKAWA watapenyeza.

Upande wa pili,wajipange...Leo Rais kawaambia Wakuu wa Wilaya watumie "vizuri" vyombo vya ulinzi na usalama,kuanzia TISS,Polisi na Mgambo kutekelezwa matakwa ya serikali na ilani ya chama tawala.

Longido ni kipimo tosha cha Demokrasia ndani ya utawala wa awamu ya tano.Mkuu huyu wa wilaya haendi tu kuwa "muwakilishi" wa Rais,bali ni kada wa CCM mtiifu,mwanapropaganda mwenye shahada ya Mawasilino ya Umma toka Chuo Kikuu Huria.Huyu hana chembe za kiserikali bali ana chembe za kichama chama.

Pole sana Ole Nangoro...Mwenyekiti wa Zamani wa CCM Mkoa wa Arusha,Wamekuletea kijana wako Chongolo,mliyeshirikiana wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki na mkabwagwa na Joshua Nassari.View attachment 361287View attachment 361288View attachment 361289
Kwa siasa za ukabila zilizoanza, Hilo jimbo wasitegemee kurudi CCM.

Kama ingekuwa kanda ya ziwa ningekusapoti ndugu mtoa mada.
 
Huyu ndio Gazeti limemtaja kuwa anajua mtambo wa kuchapisha magazeti ya Uhuru na Mzalendo umeuzwa wapi?
 
Piga kazi chongolo big up !!!.
 
UKAWA watakata rufaa Mahakama ya Rufaa na watarudishiwa JIMBO lao
Imeshindikana...Jimbo lao wamepokwa,sasa uchaguzi ndio huo unarudiwa
Hiki nilichoandika mwaka mmoja uliopita,kinaweza kutokea
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom