Kwa uteuzi huu wa DC Longido, UKAWA wajiandae kupoteza Jimbo

Uteuzi wa wakuu wa Wilaya umeshafanyika,Rais ameteuwa kwa kiasi kikubwa makada watiifu wa chama Tawala,wengi wao wakiwa vijana na wenye elimu ya kutosha.

Moja ya majukumu waliyopewa leo ni kuhakikisha ilani ya chama Tawala inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yao ya utawala.Moja ya kuhakikisha ilani inatekelezwa ni kuhakikisha pia chama tawala kinapata nguvu na "mvuto" katika wilaya walizopewa.Kazi kubwa ni kwa wakuu wa wilaya ambapo majimbo/wilaya zao zipo chini ya UKAWA;Kwa mfano Wilaya Ubungo ndugu Polepole ni juhudi zake "kumpoteza" Kubenea na kuhakikisha Jimbo linarudi CCM mwaka 2020 mara baada ya kuwa chini ya CHADEMA kwa miaka 10.

Huko LONGIDO kwenye uchaguzi wa marudio amepelekwa DANIEL GODFREY CHONGOLO,huyu ni "mwanafunzi" na "mshirika" wa karibu sana wa NAPE MOSES NNAUYE,pale Makao Makuu ya Chama Chongolo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kilichokuwa chini ya idara ya Sera na Uenezi(Kitengo cha Propaganda).

Huyu ni kada kindakindaki aliyekuwa ameambatana na Magufuli katika kampeni nchi nzima,yeye akiratibu kitengo cha habari kwa umma zikiwemo picha kurushwa mitandaoni,habari nzuri "kumpamba" mgombea wa CCM kurushwa magazetini na kwenye Tv.Huku kwenye Tv alimkamata vizuri sana Emmanuel Buhohela wa ITV aliyekuwa anafukia mashimo ya Spencer Lameck(naye wa ITV) aliyekuwa anarusha habari za mgombea wa UKAWA.Kazi nzuri ya Buhohela imempa "ulaji" Kurugenzi ya Mawasialino IKULU.

Chongolo ni mzoefu sana wa chaguzi za marudio,amekuwapo Busanda,Igunga,Arumeru Mashariki,Kiteto na Kalenga.Uwepo wake Longido huku kukiwa na maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa jimbo hilo ni mkakati tosha wa chama tawala kulikomboa jimbo.Kama kada na kijana mtiifu,chini ya mamlaka ya kidola na kiserikali kama Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya,sioni wapi UKAWA watapenyeza.

Upande wa pili,wajipange...Leo Rais kawaambia Wakuu wa Wilaya watumie "vizuri" vyombo vya ulinzi na usalama,kuanzia TISS,Polisi na Mgambo kutekelezwa matakwa ya serikali na ilani ya chama tawala.

Longido ni kipimo tosha cha Demokrasia ndani ya utawala wa awamu ya tano.Mkuu huyu wa wilaya haendi tu kuwa "muwakilishi" wa Rais,bali ni kada wa CCM mtiifu,mwanapropaganda mwenye shahada ya Mawasilino ya Umma toka Chuo Kikuu Huria.Huyu hana chembe za kiserikali bali ana chembe za kichama chama.

Pole sana Ole Nangoro...Mwenyekiti wa Zamani wa CCM Mkoa wa Arusha,Wamekuletea kijana wako Chongolo,mliyeshirikiana wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki na mkabwagwa na Joshua Nassari.View attachment 361287View attachment 361288View attachment 361289
Jidanganyeni Arusha tunajielewa CCM msipoteze Muda bure
 
Wamasai Wana tabia ya kuwa na misimamo kwenye kufanya uamuzi,sizani Kama propaganda za huyo Dc zitawabadilisha,pia tambueni ile ni ngome ya lowasa,akipiga kambi pale sizani Kama Akina sindeka wataweza haya mapambano.
 
No...hawatakata rufaa.Hii itakuwa platfoam mpya ya kupiga siasa baada ya mikutano ya hadhara kupigwa STOP.na hapo ndipo CCM watajuwa rangi zote.
Good strategy though!
Je wana uhakika lkn kama POLISI hawatadhibiti muongee nn jukwaani?
 
Mtu mmoja, hata angekuwa mzuri kiasi gani, hawezi kubadilisha kitu japo anaweza kuchangia. Kwa Nasari ilipelekwa hazina yote ya CCM mpaka kikosi maalum cha akiba kikiongozwa na Mkapa na Lowasa (wakati ule akiwa CCM), kikosi cha mbinu chafu, akina Mwigulu, lakini mwishowe walishinda?
 
Kama ulichoandika ndio mh Rais anamaanisha basi maendeleo katika nchi hii ni jinamizi, Maana hawa ni wakuu wa wilaya si makatibu wa ccm. CCM ina watendaji wake kama mtindo ndio huu wakutegemea watendaji wa serikali ndio wawe makatibu mwenezi wa CCM siku inakuja ccm itapotea katika ramani ya vyama vya siasa yangu macho, ni kwa mtizamo wangu tu lakini
 
Acha kuwatisha watu wa Arusha wewe, hapa walikuja kina mwigulu, mkapa na serikali nzima bado wakaangukia pua itakuwa huyo chanongo? Aje akutane na watu wenye maamuzi shaihi atafanya kazi salama, akija kichamachama atajutia hiyo nafasi yake.
 
Uteuzi wa wakuu wa Wilaya umeshafanyika,Rais ameteuwa kwa kiasi kikubwa makada watiifu wa chama Tawala,wengi wao wakiwa vijana na wenye elimu ya kutosha.

Moja ya majukumu waliyopewa leo ni kuhakikisha ilani ya chama Tawala inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yao ya utawala.Moja ya kuhakikisha ilani inatekelezwa ni kuhakikisha pia chama tawala kinapata nguvu na "mvuto" katika wilaya walizopewa.Kazi kubwa ni kwa wakuu wa wilaya ambapo majimbo/wilaya zao zipo chini ya UKAWA;Kwa mfano Wilaya Ubungo ndugu Polepole ni juhudi zake "kumpoteza" Kubenea na kuhakikisha Jimbo linarudi CCM mwaka 2020 mara baada ya kuwa chini ya CHADEMA kwa miaka 10.

Huko LONGIDO kwenye uchaguzi wa marudio amepelekwa DANIEL GODFREY CHONGOLO,huyu ni "mwanafunzi" na "mshirika" wa karibu sana wa NAPE MOSES NNAUYE,pale Makao Makuu ya Chama Chongolo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kilichokuwa chini ya idara ya Sera na Uenezi(Kitengo cha Propaganda).

Huyu ni kada kindakindaki aliyekuwa ameambatana na Magufuli katika kampeni nchi nzima,yeye akiratibu kitengo cha habari kwa umma zikiwemo picha kurushwa mitandaoni,habari nzuri "kumpamba" mgombea wa CCM kurushwa magazetini na kwenye Tv.Huku kwenye Tv alimkamata vizuri sana Emmanuel Buhohela wa ITV aliyekuwa anafukia mashimo ya Spencer Lameck(naye wa ITV) aliyekuwa anarusha habari za mgombea wa UKAWA.Kazi nzuri ya Buhohela imempa "ulaji" Kurugenzi ya Mawasialino IKULU.

Chongolo ni mzoefu sana wa chaguzi za marudio,amekuwapo Busanda,Igunga,Arumeru Mashariki,Kiteto na Kalenga.Uwepo wake Longido huku kukiwa na maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa jimbo hilo ni mkakati tosha wa chama tawala kulikomboa jimbo.Kama kada na kijana mtiifu,chini ya mamlaka ya kidola na kiserikali kama Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya,sioni wapi UKAWA watapenyeza.

Upande wa pili,wajipange...Leo Rais kawaambia Wakuu wa Wilaya watumie "vizuri" vyombo vya ulinzi na usalama,kuanzia TISS,Polisi na Mgambo kutekelezwa matakwa ya serikali na ilani ya chama tawala.

Longido ni kipimo tosha cha Demokrasia ndani ya utawala wa awamu ya tano.Mkuu huyu wa wilaya haendi tu kuwa "muwakilishi" wa Rais,bali ni kada wa CCM mtiifu,mwanapropaganda mwenye shahada ya Mawasilino ya Umma toka Chuo Kikuu Huria.Huyu hana chembe za kiserikali bali ana chembe za kichama chama.

Pole sana Ole Nangoro...Mwenyekiti wa Zamani wa CCM Mkoa wa Arusha,Wamekuletea kijana wako Chongolo,mliyeshirikiana wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki na mkabwagwa na Joshua Nassari.View attachment 361287View attachment 361288View attachment 361289
Nasema hivi , hata DC wa hapo angekuwa Magufuri mwenyewe , ccm haitoweza kushinda longindo hata kama chadema haitofanya kampeni yoyote , nakupa hii mapema ili kisukari chako kisijekupanda baada ya matokeo .
 
Chongolo ni mzoefu sana wa chaguzi ndogo. Uwezo wake si wa kubeza. Na ikumbukwe kama ni kurudia basi itakuwa ni wakati JPM ni mwenyekiti wa chama hivyo ataenda kufanya kampeni kama mwenyekiti akiambatana na kada Dk. Tulia Ackson Mwansasu.

Sasa Tulia na tabia zake akipeleka kwa wamasai si ndio basi tena, unajua masai wanamchukuliaje Mwanamke?
 
Kwani mara ya kwanza wakati longido inachukuliwa hakukuwa na mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama???

Tusubiri tuone, naamini demokrasia itaachwa ifanye kazi..
 
Back
Top Bottom