Kwa Uteuzi huu wa Baraza 'wapambanaji' CCM wamebanwa?

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
WAKATI baadhi ya Watanzania wakifurahia kutangazwa kwa baraza la mawaziri huku baadhi yao wakionekana kufurahia Uteuzi wa Waziri wa Ujenzi John Magufuli na ule wa Prof. Anna Tibaijuka, uteuzi huu wa Rais Kikwete amekusudiwa kuua nguvu ya makundi ndani ya chama chake Bungeni.
Uteuzi huo wa Rais Kikwete umekuja wakati watu wakiwa wameguswa na mambo mengi chini ya Utawala wake. Kwanza walikuwa wameguswa na masuala ya ufisadi na kila siku walikuwa wakipiga kelele wakitaka wale wote ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ufisadi wasulubishwe.
Pili, kutokana na uifasi huo Chama chake (CCM) kilijikuta kikigawanyika na kuzaa makundi makubwa ambayo madhara yake yalitoa majibu katika uchaguzi mkuu uliopita na hivyo kukifanya chama hicho kikongwe kiingize katika orodha ya vyama vitarajiwa vikongwe ambavyo vilimekufa ama kupoteza dola kama vile KANU ya Kenya.
Sasa baada ya doa la uchaguzi ambapo wote twajua nini kilitokea, CCM iliingia katika mtihani wa pili nao ulikuwa ni ule wa Kumpata Spika wa Bunge ra jamhuri wa Muungano, pale alikuwepo mbunge wa Urambo Mashariki, Samwel Sitta ambaye wengi walitarajiwa CCM chini ya Mwenyekiti wake Kikwete angebaki hapo kwa vile alijionesha kuwa mmoja wa wapambanaji wa Ufisadi wakitumaini kuwa hata Kikwete anapambana nao.
Lakini kinyume na matarajio hayo, CCM walitoka na sera ya kuwawezesha wanawake na kuitumia kama Kigezo cha Kumuengua Spika Sitta na badala yake kumuweka Anna Makinda ambaye sasa amekalia kiti hicho cha unahodha wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wengi walingoja kuona baraza la Mawaziri la Rais Kikwete litakuwaje, huku wakiwa na hofu ya kustaajabu kusikia Edward Lowassa akiwemo ndani na wengine kama Chenge.
Lakini hasha..! Hawakujua kuwa hesabu ya Kikwete ilikuwa mbali, na dhamira yake ilikuwa ni kujijenga zaidi na kumaliza ufa ambao umewasumbua kwa miaka mitano kiasi cha kulifanya taifa hili kumpoteza waziri mmkuu wake wa serikali ya awamu ya nne Edward Lowassa kutokana na kashfa.
Kama nilivyoeleza hapo juu, mie sikuwa miongoni mwa watu wengi ambao walishangilia uteuzi wa baraza la Mawaziri. Hata kidogo…! Na wala sikufurahia kusikia Magufuli (Kuteuliwa wizara hiyo sawa), lakini Naibu wake akitajwa kuwa Dr. Harrison Mwakyembe.
Hapa ndipo nilipobaini sura na rangi ya Kikwete, sikufurahia mtu makini (Samwel Sitta) na ambaye aliendesha bunge vyema kwa maslai ya nchi, akiondolewa kwa fedheha na kisha kupelekwa katika wizara ya Afrika Mashariki.
Hesabu kali: Kiukweli ni kuwa Taifa lilikuwa katika vita likijaribu kupambana na Ufisadi, upande mmoja mafisadi wakijaribu kupambana na wanaopambana nao ili waweze kuendelea na kutanufa raslimali za nchi hii.
Ukweli unabaki kuwa kadhia iliyotokea katika Bunge la Tisa huko Bungeni, CCM na pengeni (CCM Mafisadi)*Hii nikimaanisha kambi ya wanaopigania kuendeleza Ufisadi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete hawakufurahia, kuutokana na ukweli huo waliazimia kuhakikisha Sitta anaondolewa ndani ya Bunge ili kuacha uwanja wazi kwao na wao kuendelea kutafuna Taifa kwa kiwango ambacho watataka.
Ni kutokana na hali hiyo, baada ya kufanikiwa kumpata Spika ambaye walitamtaka, kazi yao ya pili ilikuwa ni kuhakikisha wanawaondoa wale ‘Wapambanaji Bungeni’ ili kumaliza ufa na mpasuko wa kung’olewa Spika Sitta.
Kazi hiyo imejidhihirisha katika baraza la mawaziri ambalo maeliteua na kulitangaza. Ndiyo maana sikuungana mkono wa wale waliofurahia kuteuliwa kwa Dk. Mwakyembe kuwa msaidizi wa Magufuli badala ya kupewa wizara kamili kama Sophia SImba.
Sikufurahia kuona mtu kama Mustapha Mkulo akirejeshwa wizara ya Fedha wakati tunajuwa kuwa ameshindwa kusimamia uchumi wan chi hii uakisi maisha halisi ya Wananchi na badala yake amekuwa akiimba ‘Uchumi unakua’.
Sote tunajua, na nina hakika watanzania wanajua sasa kuwa, ilikuwa ni lazima Sitta aondoke Bungeni na hata iliponekana kubaki ni hatari apewe wizara tu kwa vile anapewa bila ya kujali utendaji wake na wapi ili aondoke katika mfumo wa kushambulia bungeni.
Kwa hali hiyo angebaki kamanda mpambanaji mmoja Dk. Mwakyembe, huyu naye ilikuwa ni lazima kuhakikisha anatupwa chini ya Magufuli ili mradi tu akiingia Bungeni aingie kama mjibu hoja badala ya kuachwa kani kazi ya ‘Upambanaji’ ingezidi kuendelea licha ya Sitta kutokuwa Spika na kuteuliwa kuwa waziri.
Hivyo kwa sasa na kwa Uteuzi huo imeonyesha kuwa CCM na ufisadi ni ndugu moja ndiyo maana hakuna hatua za kuwachukulia hatua wala kupambana nao, na hata wanaoonyesha kupambana nao wanangolewa mahari penye nafasi ya kupambania na kufichwa mbali na upeo wa macho ya kupambania.
Kwa baraza hili imeonyesha kuwa Mafisadi wamefanikiwa kuwanyamazisha wabunge wa CCM ambao walisaidia sana kushambulia Ufisadi pamoja na kambi ya Upinzani na kulifanya Bunge la Tisa kuwa moto.
Sasa tutarajie mvuto na nguvu ambayo tulitaka ionekene Bungeni kuisha kwa vile kilichobaki ni kambi ya Upinzani wa CCM wamefungwa kufulu huku tukiamini kuwa kwa matendo aliyofanyiwa Sitta, na Dk. Mwakyembe kutupwa jela la mbawa za Magufuli, hakuna tena toka ndani ya CCM wa kuinuka tena kuthubutu kuanzisha vita ya Ufisadi.
Nawasilisha.
Source: bidiiforums
 
hapa naungana na mtoa hoja na nimeamini mafisadi yana mastermind wa hali ya juu. mana walianza na mbwembwe za kutaka kugombea uspika ili tuone wanakoelekea na walivyopigwa chini tunafikiri ni sawa kumbe ilikuwa danganya toto walishapanga mpango mzima wanatuzuga.

Mi nasema bado tutawahukumu tu it is just matter of time. Kama wanafikiri hapa ndio mwisho basi wameumia mana tutawatoa muda muafaka kwa balot power and this time hakutakuwa na nafasi ya kuchakachua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom