Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Moja kwa moja kwene hoja.
Kile kinachoendelea Bungeni kwa sasa baada ya kifo cha Hayati Magufuli ni aibu tupu. Utawala(siyo Uongozi) wa Spika Ndugai unazidi kuliaibisha na kushusha hadhi ya Bunge la JMT. Nitaeleza:
Kile kinachoendelea Bungeni kwa sasa baada ya kifo cha Hayati Magufuli ni aibu tupu. Utawala(siyo Uongozi) wa Spika Ndugai unazidi kuliaibisha na kushusha hadhi ya Bunge la JMT. Nitaeleza:
- Kile ambacho Watz walikuwa wanakiona wakti wa uhai wa Hayati kwamba alikuwa ana limiliki Bunge kuanzia Spika, PM, Mawaziri na Wabunge sasa kinaonekana wazi. Bunge likixoea kupokea maelekezo toka kwa Hyaati Magufuli kupitia kwa Spika Ndugai hivo halikuwa na maamuzi yoyote(rubber stamp).
- Kikao kinachoendelea pale Dodoma kwa sasa hakuna uongozi wowote pale zaidi ya kuonekana limejaa maigizo na viroja badala ya hoja.Ndugai anaoonesha alishasahau hata namna ya kusimamia misingi, kanuni na taratibu za Bunge.
- Spika anadiriki kuwaruhusu Mbunge/Wabunge wa CCM KUWASHAMBULIA WENZAO WENYE MAWAZO AU MAONI TOFAUTI NA MAMBO MENGI YALIYOFANYIKA WAKTI WA KIPINDI CHA HAYATI! Tumesikia Wabunge Darasa la 7 kina Lusinde na Msukuma wakiwatukana Wabunge wasomi kiwango cha Doctors na Professors kuwa hawajui lolote na Spika Ndugai anashangilia mpaka anawapa muda wa bonasi. Hii ni aibu.
- Kwa sasa hakuna Wabunge rasmi wa Kambi ya Upinzani wanaounda KUB walkokuwa machachari sana. Hivo muda mwingi hawa Class 7 kazi yao ilikuwa kutukana Wanunge wa Upinzani kuzima hoja zao. Leo Wapinzani hawapo Ndugai ameelekeza hao Class 7 kutukana na kushambulia Wabunge wene maoni na mtazamo tofauti. Kauli ya Januari Makamba Bungeni jana imedhihirisha hilo!
- Spika Ndugai kwa maksudi na bila aibu AMERUHUSU BUNGE LETU KUTAWALIWA NA HOJA ZA WATU DARASA LA SABA. Kwamba badala ya Bunge kuongozwa au kutawaliwa na Hoja za Wasomi wetu walosomeshwa kwa gharama kubwa na fedha ya walipa KODI wa nji hii Bunge linaongozwa na HOJA ZA DARASA LA 7 failures....!!! What a shame is this?
- Ile hoja ya CHADEMA iliyowahi kutamkwa mbele ya Bunge na Mhe. Msigwa aliyekuwa Mbunge wa Iringa mjini sasa iko dhahiri!!! Kwamba TATIZO LA NCHI YETU TANZANIA TUMERUHUSU AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA. Ndicho kinacho endelea ndani ya Bunge letu. Ndugai nz Bunge lake Wamekubali Akili za Darasa la 7 zaongoza akili za kiwango cha Madaktari na Bunge lote linashangilia!!!
- Hii hali isipobadilishwa basi tunakwenda kutumbukia na kuzama shimoni na hakuna atakaye tukwamua!! Sishangai kumsikia aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Prof. Assad kudai kuwa UWEZO WA WATUMISHI WENGI WA SERIKALI HAWANA UWEZO about 60 wako chini ya Viwango na kidogo kama 40% ndio angalau ndo wanajaribujaribu.