Kwa utaratibu huu TFF mnaua soka la Tanzania

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Ubabaishaji mkubwa ndani ya TFF ambao wanadhamana kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania utaangamiza soka letu. Wakati dirisha la usajili lilipofungwa, TFF waliongeza muda wa usajili kitu kilichoonesha nia yao ya kuvibeba baadhi ya vilabu ili vikamilishe usajili wao na huu ndo ukweli.
Ubabaishaji mwingine umeoneka wakati wa kushughulikia usajili. Leo wanazitaka timu zenye matatizo ya usajili 'KUKUBALIANA' ili kumaliza matatizo hadi leo wameshindwa kumaliza migogoro ya usajili wakati kanuni ziko wazi tu. Ndo maana kila siku tunasikia Twite, Twite mara Yondani, Yondami! TFF simamieni kanuni huu uSIMBA na YANGA unaua soka letu. Kama timu, mchezaji au Kiongozi amekiuka utaratibu ASHUGHULIKIWE kwa muujibu ya kanuni zinaoenesha soka!
 
Yanga ndiyo inayoumia, kanuni haziwezi kufuatwa. Hawako tayari kuziumiza nafsi zao ndio maana wanawaomba wakubaliane nje ya kikao.
 
Back
Top Bottom