Kwa utaratibu huu itakuwa ni vigumu sana kupata mke mwenye elimu kuanzai kidato cha 5

Vumbi

Senior Member
Nov 7, 2010
191
27
Mimi naamini elimu ni kitu cha msingi kwa mwanamke ili aweze kusimamia maisha yake mwenyewe, familia yake hata kukwepa manyanyaso yanayosababishwa na baadhi ya wanaume ndani ya jamii. Hata ndani ya ndoa mwanamke aliye elimika ni rahisi sana kukabilia na changamoto za mazingira yanayo mzunguka. Hebu angalia wanaojiunga kidato cha tano hapa chini

"Wanafunzi 36,366 ambao ni asilimia 98.31 ya waliokuwa na sifa stahili wamepangwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi, kati yao wasichana ni 11,210 sawa na asilimia 100 ya wenye sifa na wavulana ni 25,156 ambao ni asilimia 97.58 ya wanafunzi wenye sifa," .
Wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni asilimia 30.83 ya wanafunzi wote 36,366 waliopangwa.

Kutokana na uwiono 30:70 wa wanafunzi walijiunga kidato cha tano ni dhahiri kwamba kumpata mke mwenye elimu kuanzia kidato cha tano ni changamoto kubwa. Kumbuka hii dunia ya utandawazi elimu ni silaha kubwa ya kupambana nayo.
 
sijaelewa ss hapo unataka nini!! lbd nimelewa ugali, nitarudi badae!!
 
Ebwana weeee...kwahiyo sisi tuliofeli tulie tu???Mkikosa wasomi mtakuja!!!
 
Naomba msaada..!! ntapataje kuona wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kdata cha 5? Yanapatikana through link/url gani..? Kwenu wana JF
 
ukweli katika mada yako upo.ila,
kwa mimi, nikifanikiwa kupata mwanamke akawa vile ninavyotamani mke wangu awe (simaaniishi kumkontrol) namaanisha awe na tabia ninayoitamani wala kigezo cha elim hakimati saaana. hata ka 4m4 akiwa mcha Mungu wa kweli, na akili za asili(duniani), hekima, busara, anaeelewa maana ya kua mke wa mtu, mvumilivu, mchapakazi.na heshima.
me huyu ananifaa mnoooo!
na me ninazo sifa hizi ndo sababu nataka mtu kam huyu ili tumech.
 
Wale wale wa
Elimu
Dini,
Kabila,
Kazi,
Utaifa
Sura,
Rangi,
Wanene,
Wafupi,
Wembamba,
Warefu
nimechoka list ndefu mno
 
Naona Vumbi kawatimulia Vumbi mpaka mnaoka kivumbi :lol:
 
cjaelewa mbona mi mke wang nilikutana nae wkt anareseat mitian ya form 4 nikampeleka certificate akafauru nikamtupia diploma ya ualim sa hzi ana kazi na mikpo kibao bank na kwenye taasisi nyingne za fedha mwaka huu nampeleka degree 4m 5 kitu gan bana
 
Back
Top Bottom