Kwa utaratibu huu, hukumu ya wabunge wa ccm kwa 2015 ianze sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa utaratibu huu, hukumu ya wabunge wa ccm kwa 2015 ianze sasa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by KasomaJr, Jul 5, 2011.

 1. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  WanaJF Wasalaam,
  Baada ya kimya kirefu na kufuatilia mijadala ya bunge letu, maoni ya wanajf na wadau wengine wa siasa leo nimelazimika kuja na hii hoja ambayo kimsingi nahitaji kuona michango yenu kwa mustakabari wa taifa letu.
  Nimefuatilia sana sana majadiliano ya bunge kwa kipindi kirefu sasa, lakini nimekuwa mara nyingi sana nikisikitiswa na michango ya baadhi ya wabunge hasa wa CCM ambao michango yao mingi imekuwa ikijikita katka kutoa sifaaaaaaa hata ambazo kimsingi hazipaswi, na zaidi huenda mbali sana kwa kubeza hoja za wabunge pinzani bila kujali wala kutafakari mantiki ya hoja wanazowasilisha Upinzani. Kwa mfano Mbunge kijana kabisa toka jimbo la Kisarawe ambaye leo hii yeye ametumia muda mwingin kusifia ziara za rais tena kwa nguvu nyingi sana, huku akisisitiza Rais anafanya ziara za nje sana kwa lengo la kuomba misaada kwa maendeleo ya taifa letu (Kutembeza bakuri sijui kama ni suala la kujisifia au ni kudhalilika, mtasema wadau) Binasi nilipata taabu sana. Jambo lingine ni pale wabunge wanapozungumza mapungufu ya serikali, wakililalamikia kwa kutokutekeleza majukumu yake kwa wananchi lakini mwisho wanaunga mkono hoja kwa 100% mantiki yake ni nini. Mwisho ni hili la jioni ya leo ambao Bwana Chikawe ofisi ya Rais anapoliaminisha Bunge kwamba hakuna kashfa ya rushwa kwa mtanzania yeyote na kama kuna mwenye ushahidi awapelekee, hii ilifuatiwa na makofi mengi ya wabunge wa CCM (Tafsiri rahisi ni kwamba Kashfa ya Rada ni Uzushi wa Wapinzani). Sasa swali linakuja hivi leo hawa wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakishangilia kwa kila jambo bila kujali lina maslahi au madhara gani kwa taifa lengo lao ni nini, kuwepo kwao bungeni ni kwa maslahi ya chama au wananchi wao? Kama ni kwa maslahi ya chama chao ambayo yanapelekea kuwepo na ushindani wa kuhakiki hakuna lolote la maana linaloweza kuletwa na upande wa Upinzani bungeni..........Basi ufike wakati ambapo tunapaswa kuchukua hatua za makusudi kabisa kuhakikisha kuwa kura zetu zinaleta mabadiriko makubwa ili kutoa ujumbe mahsusi kuwa Ubunge ni kuwajibika kwa wananchi waliokupigia kura na si kwa chama chako, kwa msingi huo basi tuhakikishe majority wanabaki uraiani kwa kutowachagua ili ujumbe uwasilishwe kivitendo......Naomba kutoa hoja.
   
Loading...