Kwa ushaidi huu wa biblia Yohana ni Eliya

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Leo acha niondoe utata huu kwa hawa ndugu zangu wa damu,maana siku zote wamekuwa wakijiuliza kuwa "kwanini wakristo husema Yesu ni Mungu?Na tena kwanini wakristo husema Yohana mbatizaji ndiye Eliya?Basi leo nitaanza kuwafafanulia kwanini wakristo wanaamini kuwa Yohana mbatizaji ndiye Eliya.ila Mungu akinijaalia nitawafafanulia tena kwanini hata mimi naamini kuwa Yesu ni Mungu.
Tuanze na Yohana mbatizaji kuwa Eliya
2Wafalme 1:11>(Ikawa walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea,tazama!kukatokea gari la moto,na farasi wa moto,likawatenga wale wawili;naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.)

Hapo tunapata kuona ni jinsi gani Nabii Eliya alivyochukuliwa kwenda mbinguni bila kufa,Lakini japokuwa alichukuliwa kwenda mbinguni bila kufa,bado alitakiwa arudi tena duniani kwa kazi maalum.katika kitabu cha Malaki tunapata kusoma kuwa kabla ya kuja Yesu kristo yafaa kwanza Eliya arudi.

Malaki 4:4-6>(Ikumbukeni torati ya Musa,mtumishi wangu,niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israel wote,naam,amri na hukumu.angalieni,nitawapelekea Eliya nabii,kabla haijaja siku ile ya BWANA,iliyo kuu na kuogofya.Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao,ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.)

Hapa Mungu anadai kuwa atamrudisha tena Eliya nabii,kabla haijaja ile siku ya Bwana.na kazi ya Eliya ni kugeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao,na mioyo ya baba iwaelekee watoto wao.Lakini Mungu kasema atamleta Eliya kabla ya siku ya Bwana hebu tuone.

Yohana Mtakatifu 1:6>(Palitokea mtu,ametumwa kutoka kwa Mungu,jina lake Yohana.huyo alikuja kwa ushuhuda,ili aishuhudie ile nuru,wote wapate kuamini kwa yeye.)

Hapa unapata kuona kuwa Mungu alisema atamrudisha Eliya,lakini hapa tunaona Mungu kamleta Yohana.hii ikawapa wasi wasi watu wengi sana.mpaka wakatuma watu kuja kumhoji Yohana mbatizaji.

Yohana Mtakatifu 1:19>(Na huu ndio ushuhuda wake Yohana,Wayahudi walipotuma kwake makuhani wa Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize,Wewe u nani?Naye alikiri,wala hakukana;alikiri kwamba,Mimi siye Kristo.wakamwuliza,Ni nani basi? U Eliya wewe?Akasema,Mimi siye.Wewe U nabii yule?Akajibu La.Basi wakamwambia,U nani?Tuwape majibu wale waliotupeleka.Wanenaje juu ya nafsi yako?Akasema,Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani,Inyosheni njia ya Bwana!Kama vile alivyonena Nabii Isaya.)

Hapa Yohana amekataa kuwa yeye si Eliya,ila ukiendelea hapo walimuuliza,mbona basi wabatiza kama wewe si Kristo wala Eliya?hapo utaona kumbe kazi ya kubatiza ilikuwa ya wawili tu,Yesu kristo na Nabii Eliya.Sasa huyu Yohana kwanini anabatiza na wakati yeye anakataa kuwa siye Kristo wala Eliya?
Kwanini Yohana amekataa kuwa siye Eliya?

Luka mtakatifu 1:13-17>(Lakini yule Malaika akamwambia,Usiogope,Zakaria,maana dua yako imesikiwa,mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume,na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana;hatakunywa divai wala kileo;naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya,na nguvu zake,ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto,na kuwatilia waasi akili za wenye haki,na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.)

Hapo unaona kuwa Yohana mbatizaji atatumia roho na nguvu za Eliya,kumbe roho na nguvu zilizo ndani ya Yohana ni Eliya mtupu.ndio sababu Yohana alikataa kuwa yeye si Eliya kwa maana aliongea katika ulimwengu wa mwili,wakati yeye ni Eliya kwa 100% katika ulimwengu wa roho.na ikumbukwe hapo alikuwa akiongea na binadamu walioweza kutazama katika mwili tu,hivyo wasingeweza kutazama katika roho.
Je Yesu kristo alimfahamu kama Yohana mbatizaji au kama Eliya?

Mathayo mtakatifu 11:11>(Amin,nawaambieni,Hajaondokea mtu katika wazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana mbatizaji;walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu,nao wenye nguvu wauteka.Kwa maana manabii wote wa torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana,Na ikiwa mnataka kukubali,yeye ndiye Eliya atakayekuja.mwenye masikio ma asikie.)

Hapa Yesu kawathibitishia kuwa Yohana ndiye Eliya atakayekuja,nini maana ya neno hili "Eliya atakayekuja"Maana halisi ya neno "Eliya atakayekuja"ni kuwa,huyu ndiye yule Eliya mliye ambiwa atakuja.
Enyi wafilisti nadhani mtakuwa mmelewa sasa,maana huwa mnasumbua sana.eti kwanini wakristo husema Yohana mbatizaji ndiye Eliya,wakati Yohana yeye anakataa kuwa siye Eliya.majibu ni hayo,kama kuna swali unauliza,kama hujaelewa rudia kusoma mara 5 utaelewa.
Siku nyingine nitawaelewesha kwanini mimi ninaamini kuwa Yesu ni Mungu mkuu.Na mbarikiwe sana.
 
Ndio ni kweli kabisa ELIYA NI YOHANA likini tatizo ni kwamba wakristo wengi wabishi hatutaki kuelewa.
big up kwa kuchimba.
 
Ndio maana maandiko yanasema mnaangamia kwa kukosa maarifa, nasubiri ukija kuaminisha kwamba Yesu ni Mungu mkuu maana Yohana 3:16 kama sikosei inasema 'kwa maana hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amuaminiye...' maandiko yanasema 'mwanaye wa pekee' nadhani unaelewa hiyo statement sasa nasubiri ukija kuaminisha
 
Ndio maana maandiko yanasema mnaangamia kwa kukosa maarifa, nasubiri ukija kuaminisha kwamba Yesu ni Mungu mkuu maana Yohana 3:16 kama sikosei inasema 'kwa maana hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amuaminiye...' maandiko yanasema 'mwanaye wa pekee' nadhani unaelewa hiyo statement sasa nasubiri ukija kuaminisha
Ila si umeamini yohana ni Eliya
 
Angalia hapa injili ya mathayo 17:1-3
Isome kwa umakini utaona Yesu alitwaa wanafunzi wake watatu akapanda nao mlimani, kule Yesu akatokewa na Musa na Eliya. Kama Eliya alitumwa duniani na kuwa yohana, Eliya huyo aliomtokea Yesu alikua ni photocopy iliyoachwa mbinguni au?
Baada ya Eliya kutumwa kama Yohana duniani alikuja akauwawa na herode soma mathayo 14 alivyokufa akarudi mbinguni aliyemtokea yesu ni yeye wala siyo photocopy kwasababu alikuwa tayari amesharudi mbinguni una swali tena
 
Baada ya Eliya kutumwa kama Yohana duniani alikuja akauwawa na herode soma mathayo 14 alivyokufa akarudi mbinguni aliyemtokea yesu ni yeye wala siyo photocopy kwasababu alikuwa tayari amesharudi mbinguni una swali tena
Hebu tazama hapa alafu tuendelee japo swali kuu linatoka Yoh 1:21 ambapo inasema wakamuuliza unani wewe? U Eliya? akajibu akasema siye. Yohana akakataa kwamba yeye si Eliya au biblia inajipinga?
Tazama screenshot hii twende pamoja
Screenshot_2018-06-10-20-46-58.jpg
 
Hebu tazama hapa alafu tuendelee japo swali kuu linatoka Yoh 1:21 ambapo inasema wakamuuliza unani wewe? U Eliya? akajibu akasema siye. Yohana akakataa kwamba yeye si Eliya au biblia inajipinga?
Tazama screenshot hii twende pamoja
View attachment 799728
Wewe umesoma uzi wangu ukaelewa vizuri kwasababu huo mstari Yohana aliyokataa siyo Eliya nimeshaeleza na ni kwanini alikataa sina aja ya kurudia tena ndio maana mwisho wa uzi wangu nimesema soma ata mara tano ili uelewe
 
Wewe umesoma uzi wangu ukaelewa vizuri kwasababu huo mstari Yohana aliyokataa siyo Eliya nimeshaeleza na ni kwanini alikataa sina aja ya kurudia tena ndio maana mwisho wa uzi wangu nimesema soma ata mara tano ili uelewe
Andika tena hiyo sababu hapa kwani tatizo liko wapi?
 
Rudi kasome uzi kumbe ata ujasoma alafu unabisha tu soma uelewe uje na hoja za msingi kutoa kwenye biblia zinazothibitisha Yohana siyo Eliya
Sababu yako uliyoieleza haieleweki, unasema alikataa kwa sababu alikua anaongea ktk ulimwengu wa kimwili na si ulimwengu wa kiroho. Je wewe unaweza kuongea katika nafsi mbili tofauti? Katika ulimwengu wa kimwili unaongeaje na kiroho unaongeaje?
Kusema kwamba aliulizwa anabatiza kwani yeye ni Eliya au kristo ndio inamaanisha kwamba kazi ya kubatiza ilikua ya watu wawili tu? Onyesha maandiko ktk biblia kwamba Eliya alibatiza
 
Back
Top Bottom