Kwa ushahidi huu, Chura tulimlea Wenyewe, tujirekebishe!!

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,745
92,168
Nianze kwa kusema sina maslahi yoyote kwa mwenye Chura au mwenye Sauti ya chura na chura wake ila nina maslahi na nchi yangu.

Kwa wenye kumbu kumbu sahihi na zisizo na mtatizo wa kliitikadi watakubaliana na mimi kuwa zao la "Chura" huyu tuliyemuua jana alitokana na sisi wenyewe, tulikubali viwepo vimelea na viluilui vya chura, tukacheka tukafurahi, tukashabikia, leo hii chura amekua mkubwa ndio tunatambua kuwa huyu Chura hafai kuishi na sisi, nasema huu ni unafiki na kama ni dhambi basi watabeba waliolelea viluilui hao kuanzia yai, kuota mkia hadi kukatika mkia na kuwa Chura kamili.

Fumba macho yako, vuta oumzi kidogo, relax kisha vuta kumbu kumbu kipindi cha kampeni za CCM, sisemi kwa nia mbaya ila kwa hakika ngoma zile, style zile za kucheza uchi zilipaswa kukemewa instantly (viluilui), wengine tuliposema tulionekana tuna wivu, tutajinyonga kwa wivu, leo hii yamekuwa haya ndio tunaanza kumuua Chura, hakika nasema chura waliokwisha kuingia kwenye jamii yetu ni wengi na athari yake ni kubwa kuliko ya huyu chura mmoja ambaye kwa nature ya muziki wa Bongo wala asingechukua raundi kutoweka na kusahaulika.

Angalia Vidio na picha hapo chini kisha tuangalie ni wapi tulikosea? Ili makosa haya yasitokee kwa kizazi kijacho tena ni lazima tukubali kujikosa na kujisahihisha.
maxresdefault[1].jpg
hqdefault[8].jpg
 
Nyakati hizo huwa tunapagawa sasa kampeni zimekwisha ila wiki tatu bila shaka imepanda bei itakuwa inapatikana kama gongo
 
Makosa yaliyofanywa nyuma hayapaswi KUHALALISHA makosa mapya.

Tumeamua kulinda maadili, tufanye hivyo bila upendeleo.
 
Binafsi nashindwa kuelewa ni vigezo gani vinatumika mtu kuufungia wimbo
halafu nani mwenye mamlaka?
tukisema wizara je ni waziri?
mtu mmoja kwa busara zake ndo anajipa mamlaka?

je vigezo ni vipi?

halafu si nchi haina dini?
au msingi wa maadili yetu uko wapi?
 
Binafsi nashindwa kuelewa ni vigezo gani vinatumika mtu kuufungia wimbo
halafu nani mwenye mamlaka?
tukisema wizara je ni waziri?
mtu mmoja kwa busara zake ndo anajipa mamlaka?

je vigezo ni vipi?

halafu si nchi haina dini?
au msingi wa maadili yetu uko wapi?
Mkuu The Boss jiulize pia maswali yafuatayo:-

1) Ni mwongozo upi wa kimaadili ama sheria aliyoainishiwa Snura aifuate kabla ya kushoot video ya kazi zake na mwenye kutoa huo mwongozo ni nani?

2) Pia jiulize msanii ambaye hakuwa akitambulika na BASATA aliwezaje kuachiwa kutoa nyimbo zake zilozopita kabla ya huu wa chura?
 
Mkuu The Boss jiulize pia maswali yafuatayo:-

1) Ni mwongozo upi wa kimaadili ama sheria aliyoainishiwa Snura aifuate kabla ya kushoot video ya kazi zake na mwenye kutoa huo mwongozo ni nani?

2) Pia jiulize msanii ambaye hakuwa akitambulika na BASATA aliwezaje kuachiwa kutoa nyimbo zake zilozopita kabla ya huu wa chura?


Nchi hii inaendaga kwa upepo sana
 
Sina raha mtaani nikikatiza watoto wananishangilia chura huyooo...mamaa churaa
 
Back
Top Bottom