Kwa usalama wako usinywe KITOKO

Hii ni kwa wanywaji na wapenzi wa ulabu.

Kuna pombe mpya imeingia mjini inaitwa KITOKO. Hii sio pombe ya kawaida ni hatarious mno. Ipo kwenye vifungashio vya makopo ya plastic yaliyopendekezwa na serikali, Ina rangi nyekundu na imeandikwa kuwa Ina kilevi cha 40%..... Ambao sidhan Kama ni ukweli.

Kwa waliowahi kuionja watakuwa na Simulizi zake tofauti kabisa. Ni pombe ambayo naamini mtengenezaji wake ametengeneza kwa teknolojia ya kizamani kiasi kwamba zile sifa zote za pombe za zamani zipo kwenye hii KITOKO.

Kwanza ni pombe ambayo ukinywa kuna uwezekano mkubwa wa kupigana bar...
Pili unaweza ukajikuta umesahau kwako na kuanza kuzunguka mtaani Kama umelogwa...
Kulala mtaroni ni jambo la kawaida sanaaaaaa.....
Kuongea lugha za kigeni kwa ufasaha ni sifa nyingine ya hii KITOKO.

Nazungumza haya kwa sababu nimeyashuhudia huku nilipo.

Wito:
Naomba Wakati mamlaka husika ikiwamo TFDA wanachunguza viwango vya huu ulabu, wanywaji wenzangu Hebu tuususie kidogo...
Madhara ni Mengi mno.

Naomba kuwasilisha.
Kama kichwa panzi si uache! Wengine ndio kinywaji pendwa kwetu kwa sasa
 
sawa sawa mkuu....ila matumizi ya pombe inategemea na kichwa cha mtu wengine wakinywa bia 3 basi hawajiwezi je, izo bia nazo zikatazwe..!??....kwenye kilabu yetu haijafika io ipo 'don nyati' tu.....nikuulize inauzwa sh ngapi??
 
Kuna pombe moja ipo iringa sikumbuki inaitwaje ila ukinywa leo, kesho ukikaa juani mzigo unaamka upya hata ukinywa chai au supu ya moto stimu zinaludi kama umefungua mzigo mpya
 
Hiyo kitoko cha mtoto Majaribu siku moja kuona double punch au chamukwale ...Utakuja kuleta mrejesho hapa kama hawajaenda kukuokota ununio kawe.
hahahaha hii nayo iko vzr ,ila kuna DON NYATI naye si MCHEZO,kuna kitu SHUJAAZ yaani uswazi ni full kugonga vitu vikali tu
 
Hii ni kwa wanywaji na wapenzi wa ulabu.

Kuna pombe mpya imeingia mjini inaitwa KITOKO. Hii sio pombe ya kawaida ni hatarious mno. Ipo kwenye vifungashio vya makopo ya plastic yaliyopendekezwa na serikali, Ina rangi nyekundu na imeandikwa kuwa Ina kilevi cha 40%..... Ambao sidhan Kama ni ukweli.

Kwa waliowahi kuionja watakuwa na Simulizi zake tofauti kabisa. Ni pombe ambayo naamini mtengenezaji wake ametengeneza kwa teknolojia ya kizamani kiasi kwamba zile sifa zote za pombe za zamani zipo kwenye hii KITOKO.

Kwanza ni pombe ambayo ukinywa kuna uwezekano mkubwa wa kupigana bar...
Pili unaweza ukajikuta umesahau kwako na kuanza kuzunguka mtaani Kama umelogwa...
Kulala mtaroni ni jambo la kawaida sanaaaaaa.....
Kuongea lugha za kigeni kwa ufasaha ni sifa nyingine ya hii KITOKO.

Nazungumza haya kwa sababu nimeyashuhudia huku nilipo.

Wito:
Naomba Wakati mamlaka husika ikiwamo TFDA wanachunguza viwango vya huu ulabu, wanywaji wenzangu Hebu tuususie kidogo...
Madhara ni Mengi mno.

Naomba kuwasilisha.
Unaitafutia Jamiiforums kesi nyingine ya uchafuzi wa jina na brand. Mods ondoeni hii takataka inayofanana na threadd
 
Back
Top Bottom