Kwa usajili unaofanywa na CHADEMA, isahau kuchukua nchi

CCM Wanajipa moyo tu, kwani hata wao wanajua wameshachokwa kabisa na mbele yao kuna anguko kubwa lina wangoja.
 
Swali la msingi. Je ni fisadi gani kabaki ccm ili tumchukue mbaki wasafi? Tupeni list sio mngoje atakayetoka mseme fisadi. Mkishindwa kuwataja mafisadi waliobaki ccm tusiwasikie mnakenua tena atakapotoka mwingine. Kuna wengine zaidi ya kumi watatoka hivi karibuni. Msipowataja wakiondoka tusisikie oohoo fulani fisadi wakati wakiwa huko ndani mnawalinda. Nikiwasikia nawakalisha kwenye msumari!!!
 
Msafara wa mamba na kenge wamo!
huu ni ukweli usiopingika chadema kinasajiri watu wachafu ndio mana kitasubiri sana katika kushika dola
Mbona hao wanaohamia Chadema wemetoka chama kinachoshika dola!!?
Maana yake majizi na Mafisadi ndio walioshika dola, wakiamiawote na Chadema itashika dola.
 
Wakuu
kwa haraka na mshitukizo, baada ya Lazaro Nyarandu kuachia ngazi aliomba kusajiriwa na chadema, bila ajizi chadema kimesajiri

Kuanzia mtaani hadi mitandao naona watu wanashangilia usajili huu, ukweli mchungu usajiri wa watu calibler ya Nyarandu hautakisaidia chama kushika dola katika nchi hii

Kwa hali ya siasa ilivyo hapa nchini, chadema kinahitaji kusajili wanachama wasafi wasio na kando kando ya ufisadi

Kila mtu ni shahidi, humu leo baada ya kujitangaza tu Nyarandu amechimbwa sana na madudu yake aliyokuwa akiyafanya kipindi cha uwaziri wake yamewekwa wazi

Sasa kwa style hii chama kitakuwa kinatumia muda wake na nguvu nyingi kumnadi huyu mtu kama ilivyokuwa kwa waziri mstaafu Lowasa(angepaswa kuwa rais)

Chadema kiwe makini na usajiri wa hawa watu kama kweli kinania ya kuchukua dola toka ccm
Umenikumbusha mbaaaali sana,kesiy ya mwalimu na mzee Kambona.Risk assessment ni muhimu mkuu.
 
Shida kubwa itakayokimaliza CDM ni kutokuwa na akiba ya maneno pindi wanapowashambulia viongozo wa CCM.
Kipindi kile walitembea nchi nzima kunadi UFISADI wa EL. Walimpaka matope na uchafu wa kila aina.
Punde, EL akaingia CDM. Watu wale wale waliosema EL ni FISADI tena kwa kishindo, walianza kumsafisha kwa nguvu zao zote na kwa akili zao zote. Hayo yaliyofanyika kwa EL ndiyo yanayofanyika kwa Nyarandu sasa.
Kabla walimponda sana Nyarandu, lakini sasa anaitwa DUME la CDM.
Katika mazingira kama hayo mtu mwenye akili timamu kabisa hawezi kudhani kuwa CDM ni chama safi. Ni LOFA tu anayeweza kuwaamini CDM.
Ukiacha hayo, kumbuka walivyosimama kidete kuwatisha watanzania kwamba tunapodai haki yetu Acacia eti tutapelekwa MIGA.
Hayo ni machache tu kati ya mengi.
Hawa watu ni binadamu na watanzania wenzetu lakini ni wa kuogopwa kama MKOSI.
 
Chadema mtajuta kwa Haya maneno ya kujifanya popo.Hamjulikani ni ndege au mnyama.poor political part.Kweli mlikosea sana kumuondoa Daktari Slaa mnaonekana kama mayatima.Kila msaada mnataka
 
Aliiba kipindi gani? wakati yuko na nyie wezi au baada ya kuhama? Au mmemfukuza nyie? vp kama aliiba kwa ajili ya chama? usijali ni utani tu
Amekimbilia chaka la majizi mkuu
C unajua ccm kwa sasa majizi hayatakiwi
 
Ushindi katika Siasa ni wingi wa watu... Tena chama chochote kinapopata wingi wa watu wenye ushawishi ndivyo kinavyojiimarishia ushawishi na ushindi..!!

Lakini kwanini wakitoka huko ccm ndo wanakuwa wabaya.. Mkiwa nao upande wenu mnawaona ka malaika..??

[HASHTAG]#Mshindani[/HASHTAG] wa kweli wa ccm atatokea ccm.. Good News ni kuwa Tangu 1992 hadi leo idadi ya washindani wa ccm inazidi tu kuongezeka..!!
 
Kila mara nashindwa kuelewa hasa pale ninaposikia nakuona kwa macho yangu Chadema kikipokea viongozi mbalimbali baada ya kukataliwa na ccm, na wakati huo huo chadema kudai kuwa ccm ni mbaya wakati huo huo watumishi wa chama hicho hicho unawapokea kwa nderemo. Naomba jibu la ukweli.
 
CCM kupokea viongozi na kuwapa "madaraka nyeti" kutoka ACT-Wazalendo inamaana ACT ni nzuri sana?

Inamaana CCM hakuna MTU kama Kitila na mama Anna!
 
CCM kupokea viongozi na kuwapa "madaraka nyeti" kutoka ACT-Wazalendo inamaana ACT ni nzuri sana?

Inamaana CCM hakuna MTU kama Kitila na mama Anna!
hujajibu swali bali umeongeza swali lingine,je si hawa ndio walikua wanaiponda ccm chafu leo iweje wamekubali kufanya kazi na hao wachafu??
 
usajil
i
CCM Wanajipa moyo tu, kwani hata wao wanajua wameshachokwa kabisa na mbele yao kuna anguko kubwa lina wangoja.
usajili ule na anguko hili linalowakuta sasa unalisemea vipi?

wataalamu wa siasa tuliliona hili mapema
 
Back
Top Bottom