Uongozi ni dhamana ambayo kiongozi anapewa na watu kwa kumuamini na kumpigia kura ya ndiyo. Mtu anadhaminiwa kwa majukumu ya uongozi anatakiwa kuwa na weledi na uwezo wa kuongoza. Huwezi kuamka tu na kuota kugombea uongozi mkubwa kama urais ilhali watu hawajawahi kukuona ukiwa hata mbunge, ili uwe na uongozi wa juu unatakiwa uanzie wa chini.
Matarajio ya vyama vya siasa ni kushika dola ama kuendelea kushika dola. Kutokana na matarajio hayo vyama vya siasa vinabidi viwe na watu madhubuti wa kuweza kusimamia mipango na mikakati ya kushika dola. Hili halina mjadala ndani ya CCM. CCM ni chama kikongwe na kina mbinu nyingi za kukiwezesha kuendelea kushinda kila uchaguzi na hivyo kushika dola lakini hali ni tofauti kwa vyama vya upinzani. Vyama vya upinzani havijatisheleza kuwa na rasilimali watu wa kutosha kiasi kwamba tuweze kuwaamini kuwapeleka ikulu. Huu ni ukweli mchungu ,ila ukosefu wa watu makini na wa kutosha kunafanya watanzania wakose imani nao.
Upinzani umegeuka dodoki la kusafisha kila uchafu. Ukiwa fisadi na kama una nia ya kusafishwa na kung’aa kabisa jiunge upinzani. Mifano ipo mingi. Kusafisha watu ambao wamechafuka kisiasa kunapunguza credibility yao ya kuonekana ni chama mbadala na kuonekana ni furushi la uozo kwa watanzania. Kuendelea na tabia hii msahau kuja kushika dola. Watanzania wanaona na wanamua kupitia ballot box.
Upinzani wa kupinga kila kitu. Upinzani umegeuka chaka la kupinga mazuri ya serikali. Hii si nzuri kwenu, kwa sababu watu wanahitaji maendeleo na wanavyoona serikali yao inajitoa kuwaletea maendeleo na ninyi kupinga hayo maendeleo wapiga kura wanashindwa kuwaelewa. Watu watapigia kura maendeleo na kwa sababu ni CCM ndio inayoyaleta hayo maendeleo , wataendelea kuichagua CCM.
Upinzani kuamini katika migomo na maandamano badala ya mijadala. Hii pia ni sababu kubwa inayoifanya upinzani kushindwa kuimarika Tanzania. Watu inabidi wahamasishwe kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza umasikini na si kuwajaza watu barabarani kufanya migomo. Maandamano ni ishara ya kukosekana kwa suluhu ya majadiliano ambalo si jambo la kweli. Upinzani unatakiwa utoke kwenye kuamini maandamano mpaka kuamini katika majadiliano. Upinzani wa migomo na maandamano hauwezi kushinda popote pale duniani.
Kama upinzani usipoweza kutatua hizi changamoto isahau kuongoza nchi. Watanzania wanaona yanayoendelea, wanapima na watakuja kuamua kwenye sanduku la kura. Upinzani uache kuwa wa matukio na uwe wa matokeo.
FPT 2040