Kwa upande wa mahusiano wanasayansi hawa walikuwa hamnazo kweli.........!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kila mmoja wetu amewahi kusikia kuhusu wanasayansi wakubwa walioonekana kama vichaa au Maprofesa waliokuwa kama wana upungufu wa akili.

Kwa mfano Albert Einstein ni mwanasayansi alieweza kuelezea kwa undani kuhusu uwiano mwingi wa masuala ya sayansi. Yeye alifurahia sana kuwa na nyumba ndogo. Hiyo nyumba yake ndogo alikuwa ni binamu yake na aliishi nae kwa takribani miaka mitano kabla hajamuacha mkewe wa ndoa ambaye alizaa nae watoto kadhaa kabla ya kufunga nae ndoa, na kuioa hiyo nyumba ndogo.

Charles Darwin huyu ningependa kumuita mzee wa utata, huyu nae ni mwanasayansi aliyezungumzia kuhusu mabadiliko ya viumbe (Evolution). Alikuwa akiishi peke yake kwa muda mrefu bila ya kuoa kwa sababu alikuwa akijiuliza faida ya kuoa na kuishi bila kuoa kabisa. Mwansayansi huyu nae alikuwa na vituko vingi, kwani kuna wakati alisema, "Kwa kiasi fulani mke ni bora kuliko mbwa, lakini ni kupoteza muda wako tu kuwa nae" Hata hivyo alikuja kuoa baada ya kuwa na uhusianao wa muda mrefu na mwanamke huyo aliyemuoa.

Sigmund Freud, Huyu ameweza kueleza vizuri kuhusu saikolojia na ufahamu, kwa ujumla alikuwa ni mtu mzuri, lakini alikuwa na mzozo na rafiki yake, kutokana na tabia zake za kushindwa kudhibiti hisia zake za kutojitosha, na hivyo kutaka kuabudiwa na kunyeyekewa.

Isaac Newton ambaye aliweza kukokotoa na kutoa kanuni za mwendo zijulikanazo kama Newton laws of motion, na kanuni ya nguvu za mvutano za dunia, alilelewa na bibi yake, baada ya baba yake kufariki na mama yake kuolewa na mwanamume mwingine, ambaye Newton hakumpenda kabisa. Newton alikuwa na tabia ya kupenda ugomvi na mizozo isiyo na umuhimu na wanachuo wenzake na hata marafiki zake, pia alishawahi kulelewa kwenye vituo vyenye kutoa ushauri nasaha. Kumbuka hapa namzungumzia mtu ambaye ugunduzi wake kwenye Fizikia haujavunjwa hadi leo.

Marie Curie ambaye aligundua Radioactivity, aliishi na mume wake kwenye nyumba iliyokuwa na vitu vichache na vilivyozagaa kwa sababu alichukia sana kazi za ndani, sijui wakati huo kulikuwa hakuna watumishi wa ndani (House Girls)? Wakati wakifanya shughuli zao za uchunguzi kuhusu radioactivity walikuwa wakiishi katika kibanda chao kilichokuwa na matundu, kiasi ambacho hata mvua ikinyesha maji yaliweza kuingia ndani. Hawakuwa na fedha nyingi na mara nyingi walitumia fedha kidogo walizonazo kununua kahawa na kunywa kwa furaha, huku wakiota katika jiko lao la stovu. Marie Curie nae alijishindia tunzo mbili za Nobeli.

Paul Erdos mmoja wa wanahisabati katika karne ya 20, ambaye amesaidia sana katika kutengeneza Kompyuta, huyu naye hakuwa ametulia sana. Hakuishi maisha ya kifahari, karibu maisha yake yote yalikuwa ya kifukara, kwani alitegemea misaada ya chakula na nguo kutoka kwa marafiki wema. Hakupenda kujilimbikizia mali ingawa angeweza kama angetaka.

Je sasa umeweza kushawishika kwamba watu wenye vipaji maalum (Geniuses), huenda ni watu ambao kwenye upande wa pili wa maisha yaani katika kujenga maisha yao, hawana uwezo? Lakini Je sio kwamba watu wanapokuwa na uwezo mkubwa kiakili hatimaye mambo mengine kama vile fedha na ufahari vinakosa maana kwao? Nadhani hili ndilo la msingi.

Lakini cha ajabu ni kwamba, wanaofaidi ni wale waliokaririshwa nadharia za wanasayansi hawa.
 
Je sasa umeweza kushawishika kwamba watu w
enye vipaji maalum (Geniuses), huenda ni watu ambao kwenye upande wa pili wa maisha yaani katika kujenga maisha yao, hawana uwezo? Lakini Je sio kwamba watu wanapokuwa na uwezo mkubwa kiakili hatimaye mambo mengine kama vile fedha na ufahari vinakosa maana kwao? Nadhani hili ndilo la msingi.

Lakini cha ajabu ni kwamba,
wanaofaidi ni wale waliokaririshwa nadharia za wanasayansi hawa.

Yeah...kina Karl Max,Alzavel Lwaitama,Nyerere ,kuna mzee mmoja alikuwa kijijini kwetu etc,etc to mention the few ni mfano wao.

My take:Inabidi ikitokea mtu ni genius_then serikali ichukue hatua mahususi kumjengea uwezo kimaisha i.e kumjengea nyumba nzuri,wafanyakazi wa kumsaidia kazi etc,..ili yeye aachwe ashughulike na mambo yake.
 
nimependa hiyo ya marie curie maisha ni kuridhika huku ukitafuta njia za kusonga mbele,utaishi kwa furaha kabisa.
 
Je sasa umeweza kushawishika kwamba watu wenye vipaji maalum (Geniuses), huenda ni watu ambao kwenye upande wa pili wa maisha yaani katika kujenga maisha yao, hawana uwezo? Lakini Je sio kwamba watu wanapokuwa na uwezo mkubwa kiakili hatimaye mambo mengine kama vile fedha na ufahari vinakosa maana kwao? Nadhani hili ndilo la msingi.

Lakini cha ajabu ni kwamba, wanaofaidi ni wale waliokaririshwa nadharia za wanasayansi hawa.

Binafsi mimi watu8 ninaweza jiita ni mtu mwenye kipaji kiakili(si mvumbuzi), hapa namaanisha akili za kupewa na Mungu kuweza kuwa na uelewa wa kirahisi katika kujifunza vitu vipya kama masomo n.k. Kuna mambo ambayo nimefanya na kuniweka miongoni mwa wachache waliofanikiwa kufanya.
Lazima tutambue ya kwamba maisha ni kupanga na kuchagua, zaidi maisha ni mtiririko wa matukio yaliyo muhimu na yasiyo muhimu. Mengi ya matukio hayo huwa tunapanga na mengine hutokea si kwa matakwa yetu bali kwa uweza wa nguvu zilizo juu yetu.
Maishani nimejifunza kitu kimoja, watu wengi wenye vipaji ambao binafsi nitawaita wavumbuzi walikuwa na vipaumbele ambavyo ndio vilikuwa elekezi za maisha yao. Kuna kitu ambacho kilikuwa ni kiu na shauku ndani ya bongo zao kiasi cha kwamba fikra zote zikaelekezwa huko, kumbuka watu hawa walikuwa wanahangaika kugundua kanuni, au formula. Naomba tutambue kuwa, ili mtu kuweza kuvumbua kanuni fulani ya kifizikia, au ya kihesabu, mathalani kanuni za mwendo ilikuwa inahitaji muda mrefu sana maana wakati huo haukuwa na teknolojia kubwa.
Huwa inasemekanika mtu kama Albert Einstein aliweza kutumia 9% tu ya ubongo na akafanya hayo aliyoyafanya, kwa mantiki hiyo basi unaweza kung'amua kuwa watu wa namna hii hawana habari na aina nyingine za maisha.
Kwa hiyo ndugu Mtambuzi, hao uliowataja walichagua kuishi hivyo kutokana na wito waliokua nao ndani yao na si kwamba hawakuweza kuishi kivingine.
 
Kuna jamaa mwingine kule Urusi - nimesahau jina - hivi majuzi tu amekataa kupokea tuzo zake mara mbili. Yule naye ni genius ambaye maisha yake ya kawaida ni ya ajabu-ajabu, anaishi kipweke-pweke tu.
 
Hivi, katika maisha unataka uwe na objectives ngapi???
Wao waliona ya uvumbuzi ndio kubwa kuliko ya kuoa au mahusioano ya kijamii

Mie naona wako poa tu

Kwanza Mahusiano is a complex phenomena..kwa sababu inahusu interaction ya watu wengi..Na wengi tu genius guys ukiwafuatilia utaona hawanaga muafaka mzuri kwenye mahusiano. Nadhani kuna tofauti kubwa ya kufanya kitu objectively na kufanya kitu subjectively. Mapenzi sounds like a subjective issue!!

Just guys like Mandela, Clinton et al nao mapenzi yaliwatesa tu!
 
ni swala la kudedicate and to them they dedicated their lives into science manake waliona mbali sana huwez ukafanya mambo mawili ukafaulu yte vizur kwa mara moja.
 
kuna filosofia moja inayosema kuwa binadamu katika maisha yake huwa siku zote anatafuta furaha ya kweli na ya juu(ultimate joy) na inasemekana zaidi ya 80% ya watu furaha zao zimegawanyika katika makundi makubwa mawili
la kwanza ni furaha itokanayo na vitu(material joy) na wengine furaha ya maarifa(intellectual joy)
wengi ya magenius huwa wanatafuta intellectual joy,wasomi wengi huishia kujali intellectual joy na kuishia kuishi maisha ya kimasikini kwa mtazamo wetu na ya furaha ya kweli kwa mtazamo wao.
 
Mkuu ninakubali nawe kwa haya, lakini mtu kama I. Newton angekuwa na maisha ya upande wa pili pengine asingeweza kufanya hayo aliyoyafanya. Ila mara nyingi watu wa namna hiyo huwa hawana habari na maisha ya upande wa pili.
 
Back
Top Bottom