Kulupango
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 288
- 534
Dogo yuko fm1 shule zetu za kata. Jana nikawa nambananisha maswali ya hapa na pale ya fm 1, kichwani hamna kitu.
Basi nikamwambia anitajie majina ya Topics za hesabu, akataja topic 1 tu inaitwa Real number. Nikamwambia taja topics za History, akataja Chimpanzee, taja topics za chemi hajaweza hata 1, taja topics za geography kataja Earth, taja topics za English kataja tenses, taja topics za physics kataja Matter. Kwa kweli nikachoka.
Baada ya hayo majibu nikaishiwa pose, huu ni mwezi wa 10 na anasema wameshamaliza kusoma topic zote za masomo yote, wamebakisha topic moja au mbili mbili kwa baadhi ya masomo. Masomo mengine wamemaliza kabisa.
Nikamuuliza dogo shida ni nini hadi unakuwa hivi? Akajibu hajui kiingereza, nikamuuliza somo gani wewe unaliweza vizuri akajibu kiswahili, nikamuuliza Nomino ni nini? akajibu Nomino ni maneno ambayo ni majina ya watu, vitu na hali, pia kajibu Nomino ni aina ya neno linalotaja jina la kitu, mahali, mnyama, mtu, sifa au wazo. Nika muuliza kuna aina ngapi za Nomino akajibu Kuna nomino za kawaida na nomino za kipekee, nikamuuliza taja topics za kiswahili akazitaja.
Nikaona isiwe shida huwenda huyu ni kichwa maji kwa hayo masomo mengine, kesho yake nikaenda shuleni kwao. Nikatulia sehemu pembeni karibu na wauza visheti, muda wa break nikawa natafuta vijana wa fm1. Nikawapata kama 10 hivi,
Nikawauliza maswali yale yale katika masomo yao, wote 10 hawakuweza, nikawaambia wanitajie majina ya topics za kila somo.
Kwakweli ni msiba, wale madogo 10 hakuna aliyeweza kutaja topic zaidi ya tatu. Nikawauliza shida ni nini, wakajibu shida ni kiingereza.
Maana tunakariri kiingereza bila kuelewa masomo. Kwa hiyo tunakuwa tunasahau sana kwasababu masomo ya kiingereza ni mengi.
Kesho yake nikaja tena pale shuleni, nikafanikiwa kuzungumza na vijana 20 wa form1. Majibu yakawa ni yale yale, maswali hawakuweza kujibu kiusaha, majina ya topics hawakuweza kunitajia zaidi ya topic tano kwa kila somo, lakini somo la kiswahili kila mtu yuko vizuri.
Sasa, siku ya 3 nikarudi tena pale shuleni, maana dogo nilimuuliza ni nani anatokaga wa kwanza form1. Akanitajia jina lake, nikaenda shule nikamtafuta nikampata.
Ndugu zangu inasikitisha sana kwa kweli, huyu dogo nikamuuliza maswali akawa anayajibu vizuri tu, maswali mbalimbali ya form1 akawa anayajibu safi kabisa, nikamuuliza majina ya topics akataja topics zote za masomo yote ambazo wameshafundishwa.
Nikamuuliza nipe siri ya mafanikio yako mpaka kuwazidi wenzako, akajibu ni juhudi tu na kumuomba MUNGU, nikamuuliza kwani wewe unadhania hawa wenzako wote karibu miatatu wao hawamuombi MUNGU na kufanya juhudi?
Dogo akajibu, Shida wengi wao ni tofauti na mimi, mimi nilisoma English medium shule ya msingi, kwa hiyo masomo ni kama nina yarudia yale yale ya shule ya msingi hakuna utofauti mkubwa.
Nikamuuliza kwanini hukwenda private secondary,? Akajibu kwasababu napenda kusoma shule niliyochaguliwa na serekali.
Sasa ombi langu, naona bora kubadili lugha iwe kiingireza tangu wakiwa shule ya msingi au waendelee kusoma kwa kiswahili hadi secondary, yamkini tunapoteza vipaji vingi sana kwa kigezo cha lugha.
HIV NDVYO WATOTO WA SHULE ZA KATA WANAVYOSISITZWA KUJFUNZA KIINGREZA, JAPO BADO NI TATZO :
AU serekali iweke mwaka mzima kwa watoto kujifunza lugha wanapotoka Darasa la 7, Kabla ya kuanza masomo ya kidato cha kwanza.