Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwanza nioneshe masikitiko yangu kwa kijana mwenzetu, Zitto Kabwe ambaye hapo awali tulimuamini kwa kujenga hoja madhubuti kwenye mapambano dhidi ya ufisadi. Hakika mara kadhaa Zitto Kabwe aliibuka shujaa na hoja zake zilikuwa na mashiko.
Ila kwa sasa sijaelewa nini kimemkumba ndugu Zitto Kabwe. Kwa sasa amegeuka kuwa mtetezi wa Ufisadi na Mafisadi. Nimejiuliza sana nini kinaendelea nyuma ya pazia.
Awali alizusha kuwa Ndege Mpya zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya ATCL ni Mtumba kutoka shirika la Ndege la Kazakhstan. Tena Zitto akaenda mbali kwa kusema kuwa ndege hizo zilipaswa kununuliwa kwa dola za kimarekani milioni 9 kwa kila moja lakini Serikali imenunua kwa Dola milioni 61. Waandishi wa habari waliopata fursa ya kujionea ndege ya kwanza iliyowasili hakika wamestaajabu sana baada ya kubaini kuwa Zitto Kabwe kasema uongo. Baadhi ya waandishi ambao nilikuwa nao karibu wamehoji sababu hasa ya Zitto Kabwe kutunga uongo ule.
Leo amekuja na kihoja kingine kuwa eti Habinder Seth, mmiliki wa IPTL aligharamia mkutano wa CCM uliomchagua Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hicho na ndio maana Rais hachukui hatua dhidi yake. Lengo la Zitto Kabwe kutunga uongo huu ni kumpaka matope Rais na kumhusisha na matendo ya kifisadi ambayo hana.
Hapa ndipo ninapokumbuka maneno ya Zitto Kabwe kuwa Usimwamini Mwanasiasa. Kwa hili nimemdharau sana Zitto Kabwe