Kwa ungozi wa Shirika la Reli (TRL) kuhusu route ya Ubungo Stesheni

NjalangiJr

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
251
88
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa huduma mnayoitoa kwa wananchi wa mkoa wa dar es salaam, kiukweli mmetupunguzia adha ya kukaa muda mrefu kwenye foleni barabarani kwa hilo nawaponeza sana pamoja na serikali Yangu.

SASA nije kwenye point yangu ya msingi,cjui hivi vituo vyenu mlivipanga kwa kuzingatia vigezo gani.kwa sisi wakaz wa Tabata hususani, bonde la msimbazi,Matumbi,Aroma,Tabata Shule na maeneo ya Jirani na Bima, hii treni kwetu imekua haitusaidii Sana kutokana na kukkosekana kituo katikati ya Buguruni kwa mnyamani na round about ya Tabata ambayo nyinyi mnaita kituo cha Matumbi.

Kuna kundi kubwa la wakaz wa maeneo haya wanashindwa kutumia usafir huu kwa sababu inabidi aunganishe usafir mara mbili ili apande treni au anaposhuka vinginevyo ni bora upande daladala ili usiunganishe usafir.
Wakati mngeweka kituo hapa katikati mngeongeza idadi ya abiria na pia mngemsaidia huyu mwananchi wa kawaida kupunguza gharama za usafiri.

Naamini ujumbe huu utafika na utafanyiwa kazi,katika kuboresha huduma hii.
NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom