Kwa Unayeutaka Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Unayeutaka Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abraham Lincon, Jan 14, 2011.

 1. A

  Abraham Lincon Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello great thinkers. Natumaini mpo poa. Kama wewe ni mmoja wa wanaotarajia kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi topic hii inakuhusu kwa namna moja ama nyingine.

  Yapo mambo mengi ambayo binafsi ningependa kuyaongelea lakini hapa nitasema machache kama angalizo tu kwa yeyote mwenye nia ya kuwa Rais wetu wa awamu ijayo.

  Jambo la kwanza, tafadhali sana naomba usiwe mbinafsi. Hii ni moja ya tabia mbaya sana kwani madhara yake yanaweza kuwa mzigo mkubwa sana (usio bebeka) kwa wananchi utakaowaongoza. Ubinafsi, kama ukiuangalia kwa mapana na marefu yake ndiyo chanzo cha matatizo yote duniani. Rushwa, udini, ufisadi, uchoyo, ulafi, mauaji, uuzaji madawa ya kulevya, majungu na yote uyajuayo wewe yasingelikuwepo kama watu tusingekuwa selfish. Binafsi nachukia sana ubinafsi na ninaulaani kwa nguvu zote! Narudia tena, tafadhali sana naomba uhakikishe wewe si mbinafsi na upo tayari kutumika kwa ajili ya wananchi na kwa faida ya taifa letu.

  Pili, nakuomba sana uwe tayari kuwekeza katika elimu kwa gharama yoyote ile. Binafsi naamini kama tunahitaji mabadiliko katika sekta yoyote ile nchini, lazima tuinue kiwango cha ubora wa elimu yetu. Hivi sasa shughuli zinazofanyika nchini zinafanyika kwa kiwango duni sana sawasawa na uduni wa elimu yetu. Elimu liwe jambo la kwanza na lipewe umuhimu wa juu. Uhuru wa kweli katika Tanzania utaletwa na elimu! Vile vile uwe tayari kuwekeza katika tafiti kwa kiwango cha juu pia.

  Zaidi ya yote naomba jitahidi sana, hakikisha wewe si kibaraka wa yeyote. Uwe mtu huru. Unapokuwa huru unafanya kazi zako kwa uhuru. Kamwe hutafanya kazi kwa ajili ya wachache waliokuweka bali kwa ajili ya wananchi waliokupigia kura zao. Hutapendelea bali utakuwa tayari kuwapigania wanachi wako na kuwalinda kwa gharama yeyote. Natamani sana kama utakuwa na tamaa ya mafanikio ya wenzetu 'majuu' na kuhahakisha nchi yako inayapata pia. Viongozi wa mataifa ya magharibi wapo tayari kubomoa kwa wenzao ili kujenga kwao lakini sivyo kwa viongozi wetu. Siku zote husikiliza wakubwa wa mataifa ya nje huwanyenyekea na kuwajali zaidi ya wananchi wao wanyonge. Tuache kujipendekeza kwa mataifa ya nje na tujenge nchi yetu mbona resources tunazo?

  Najua yapo mengi sana ya kuchangia. Kwangu mimi kwa leo haya yananitosha. Ungependa Rais wako aweje? Tafadhali mwaga sifa zilizobaki.

  'If You Can't See The Future, You Won't Have The Future! Dream The Imposible!'
   
 2. A

  Abraham Lincon Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello great thinkers. Natumaini mpo poa. Kama wewe ni mmoja wa wanaotarajia kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi topic hii inakuhusu kwa namna moja ama nyingine. Yapo mambo mengi ambayo binafsi ningependa kuyaongelea lakini hapa nitasema machache kama angalizo tu kwa yeyote mwenye nia ya kuwa Rais wetu wa awamu ijayo. Jambo la kwanza, tafadhali sana naomba usiwe mbinafsi. Hii ni moja ya tabia mbaya sana kwani madhara yake yanaweza kuwa mzigo mkubwa sana (usio bebeka) kwa wananchi utakaowaongoza. Ubinafsi, kama ukiuangalia kwa mapana na marefu yake ndiyo chanzo cha matatizo yote duniani. Rushwa, udini, ufisadi, uchoyo, ulafi, mauaji, uuzaji madawa ya kulevya, majungu na yote uyajuayo wewe yasingelikuwepo kama watu tusingekuwa selfish. Binafsi nachukia sana ubinafsi na ninaulaani kwa nguvu zote! Narudia tena, tafadhali sana naomba uhakikishe wewe si mbinafsi na upo tayari kutumika kwa ajili ya wananchi na kwa faida ya taifa letu. Pili, nakuomba sana uwe tayari kuwekeza katika elimu kwa gharama yoyote ile. Binafsi naamini kama tunahitaji mabadiliko katika sekta yoyote ile nchini, lazima tuinue kiwango cha ubora wa elimu yetu. Hivi sasa shughuli zinazofanyika nchini zinafanyika kwa kiwango duni sana sawasawa na uduni wa elimu yetu. Elimu liwe jambo la kwanza na lipewe umuhimu wa juu. Vile vile uwe tayari kuwekeza katika tafiti kwa kiwango cha juu pia. Zaidi ya yote naomba jitahidi sana, hakikisha wewe si kibaraka wa yeyote. Unapokuwa huru unafanya kazi zako kwa uhuru. Kamwe hutafanya kazi kwa ajili ya wachache waliokuweka bali kwa ajili ya wananchi waliokupigia kura zao. Hutapendelea bali utakuwa tayari kuwapigania wanachi wako na kuwalinda kwa gharama yeyote. Natamani sana kama utakuwa na tamaa ya mafanikio ya wenzetu 'majuu' na kuhahakisha nchi yako inayapata pia. Viongozi wa mataifa ya magharibi wapo tayari kubomoa kwa wenzao ili kujenga kwao lakini sivyo kwa viongozi wetu. Siku zote husikiliza wakubwa wa mataifa ya nje huwanyenyekea na kuwajali zaidi ya wananchi wao wanyonge. Tuache kujipendekeza kwa mataifa ya nje na tujenge nchi yetu mbona resources tunazo? Najua yapo mengi sana ya kuchangia. Kwangu mimi kwa leo haya yananitosha. Ungependa Rais wako aweje? Tafadhali mwaga sifa zilizobaki.

  'If You Can't See The Future, You Won't Have The Future! Dream The Imposible!'
   
 3. A

  Abraham Lincon Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello great thinkers. Natumaini mpo poa. Kama wewe ni mmoja wa wanaotarajia kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi topic hii inakuhusu kwa namna moja ama nyingine.

  Yapo mambo mengi ambayo binafsi ningependa kuyaongelea lakini hapa nitasema machache kama angalizo tu kwa yeyote mwenye nia ya kuwa Rais wetu wa awamu ijayo.

  Jambo la kwanza, tafadhali sana naomba usiwe mbinafsi. Hii ni moja ya tabia mbaya sana kwani madhara yake yanaweza kuwa mzigo mkubwa sana (usio bebeka) kwa wananchi utakaowaongoza. Ubinafsi, kama ukiuangalia kwa mapana na marefu yake ndiyo chanzo cha matatizo yote duniani. Rushwa, udini, ufisadi, uchoyo, ulafi, mauaji, uuzaji madawa ya kulevya, majungu na yote uyajuayo wewe yasingelikuwepo kama watu tusingekuwa selfish. Binafsi nachukia sana ubinafsi na ninaulaani kwa nguvu zote! Narudia tena, tafadhali sana naomba uhakikishe wewe si mbinafsi na upo tayari kutumika kwa ajili ya wananchi na kwa faida ya taifa letu.

  Pili, nakuomba sana uwe tayari kuwekeza katika elimu kwa gharama yoyote ile. Binafsi naamini kama tunahitaji mabadiliko katika sekta yoyote ile nchini, lazima tuinue kiwango cha ubora wa elimu yetu. Hivi sasa shughuli zinazofanyika nchini zinafanyika kwa kiwango duni sana sawasawa na uduni wa elimu yetu. Elimu liwe jambo la kwanza na lipewe umuhimu wa juu. Uhuru wa kweli katika Tanzania utaletwa na elimu! Vile vile uwe tayari kuwekeza katika tafiti kwa kiwango cha juu pia.

  Zaidi ya yote naomba jitahidi sana, hakikisha wewe si kibaraka wa yeyote. Uwe mtu huru. Unapokuwa huru unafanya kazi zako kwa uhuru. Kamwe hutafanya kazi kwa ajili ya wachache waliokuweka bali kwa ajili ya wananchi waliokupigia kura zao. Hutapendelea bali utakuwa tayari kuwapigania wanachi wako na kuwalinda kwa gharama yeyote. Natamani sana kama utakuwa na tamaa ya mafanikio ya wenzetu 'majuu' na kuhahakisha nchi yako inayapata pia. Viongozi wa mataifa ya magharibi wapo tayari kubomoa kwa wenzao ili kujenga kwao lakini sivyo kwa viongozi wetu. Siku zote husikiliza wakubwa wa mataifa ya nje huwanyenyekea na kuwajali zaidi ya wananchi wao wanyonge. Tuache kujipendekeza kwa mataifa ya nje na tujenge nchi yetu mbona resources tunazo?

  Najua yapo mengi sana ya kuchangia. Kwangu mimi kwa leo haya yananitosha. Ungependa Rais wako aweje? Tafadhali mwaga sifa zilizobaki.

  'If You Can't See The Future, You Won't Have The Future! Dream The Imposible!'
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Unafikiri ikiwa hivi inachosha kusoma na kutafuta mawazo ya mwandishi?
   
Loading...