Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,631
Wiki iliyopita wakati Klabu ya JKT Tanzania ikicheza dhidi ya Yanga SC katika Uwanja wa Jamhuri katika Mji Mkuu wa Tanzania Dodoma mara baada ya Mchezo huo haraka sana Katibu wa Wizara husika ya Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Dkt. Abbas pamoja na Waziri wake Dkt. Mwakyembe waliamua Kuzuia Watazamaji Kuingia tena kwa kile walichosema Kukiukwa kwa taratibu za Kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19 (CORONA) kwakuwa Uwanja ulijaa kupita Kiasi na Kuhatarisha Afya za Wahudhuriaji.
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida ambayo Mzukulu bila Uwoga wala Unafiki au Aibu alisema ni kwamba jana katika Mchezo baina ya Mbeya City na Simba SC katika Uwanja wa Sokoine Uwanja huo ulijaza kupita Kiasi na hata Picha zilionekana kwa tulioutazama huo Mpira lakini pia hapakuwa na kinachoitwa Social Distancing kama ilivyokuwa ikisisitizwa na mpaka hivi sasa Uwanja huo haujazuiwa Kuingiza Mashabiki na Wahusika Katibu wa Wizara Dkt. Abbas na Waziri wake Dkt. Mwakyembe wamenyamaza kama si Kuuchuna.
Najua fika kuwa hakuna hatua yoyote ile ya Kinidhamu ambayo itachukuliwa na Wahusika ( hasa Waziri Dkt. Mwakyembe ) dhidi ya Uwanja huo wa Sokoine Mkoani Mbeya kwakuwa Tukio zima la jana Waziri Dkt. Mwakyembe alilitumia kama Ngazi yake ya Kupandia katika Kujipatia Umaarufu zaidi wa Kisiasa, Kueneza Ukabila wake ambao kwa huko Mbeya umeota Mizizi. Na najua hata Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ambaye anautaka Ubunge wa Mbeya Mjini kwa Udi na Uvumba na alikuwepo lilimsaidia pia.
Mzukulu ninamalizia kwa kusema kama Uwanja wa Jamhuri Dodoma ulipewa adhabu basi na wa Sokoine Mbeya nao uadhibiwe pia tena haraka.