Kwa umati huu wa wananchi kwa CHADEMA kuhitimisha kampeni za ubunge Jimbo la Ukonga ni dhihirisho la kuchokwa kwa CCM nchini

Hali kama hii ndio inawafanya CCM washindwe kuelewa wafanye nini kuimaliza CHADEMA na upinzani kwa ujumla.

Nilishwaambia kupitia hapa JF kuwa wanachokifanya kwa lengo la kutaka eti kuua upinzani hakina tofauti na mtu anaetaka kuua nyoka kwa kuponda mkia badala ya kichwa.

Watakachofanikiwa ni kuchelewesha tu safari ya mabadiliko lakini sio kukwamisha safari hiyo kufika mwisho.Safari hii kufika mwisho ni swala la muda tu na si vinginevyo.

Kwa kifupi, CCM wamepaniki, wamechanganyikiwa, wamejawa hofu ya kupoteza dola na zaidi wako very frustrated kiasi kwamba wameamua hata kama watatoka madarakani basi watoke wakiwa wamefanya kila aina ya vurugu, vituko, uovu, n.k kwani wameshajikatia tamaa na hivyo hawaoni hasara kufanya lolote maana hakuna hasara kubwa kwao kama kupoteza dola.

Yaani walichoamua ni kama ni yale ya kwenye soku kuwa hata kama mnatufanga, lakini na sisi chenga twawala.

Bahati mbaya wao chenga zao ni Polisi, NEC, Wakurugenzi wa Halamashauri, n.k.
kwani hao watu wote wamekuambia wataipigia kura Chadema? Kuna wana CCM hapo wamekuja kuwachora tu
 
Sina neno zaidi ya kumtakia ushindi Mh. mtarajiwa Asia Msangi.

Huyu mkurya hana jipya maana hawezi achia ubunge akiwa na kaki halafu arudi tena na kijani kuuomba tena ubunge ule ule sehemu ile ile kwa watu wale wale.

Ulipewa ukauacha sasa ngoja apewe mwingine wewe kalime matembele mabondeni huko na ndugu zako,shubaaaaamit.
Hakuna CHADEMA hapa mura tulilima matembele naye tunashiriki mambo mengi pamoja. Jimbo in la Waitara kabla ya misaa ya pili kuisha. Aanzeni kutafuta sababu za kushindwa maana ni lazima CDM Ishindwe Ukonga.
 
Nimeelewa sehemu moja katika uzi wa mtoa mada,
Chama tawala tendeni haki kwa makundi yote ya kijamii bila kujali matabaka,mwisho wa kunukuu
Upendo haulazimishwi bali upendo hushawishiwa ila binafsi sina chama
 
Nimeelewa sehemu moja katika uzi wa mtoa mada,
Chama tawala tendeni haki kwa makundi yote ya kijamii bila kujali matabaka,mwisho wa kunukuu
Upendo haulazimishwi bali upendo hushawishiwa ila binafsi sina chama
Uko chadema
 
Lkn hao wote ni wakazi wa ukonga na wanasifa za kupiga kura sio ikawa watu wametoka kimara na mbagala wanajaza uwanja uchaguzi ukipita matokeo yakitoka tunaanza lawama
Kama mtu anatoka kimara...kawe...anaenda kumsikiliza mbowe kwa gharama zake ni jambo jema sana....!!! Kuliko ccm wanaosombwa kwa maroli kama ng'ombe!!
 
Viongozi wa kitaifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dr Vicente Mashinji na Mbunge wa Jimbo la Kawe Mh Halima Mdee wakihitimisha kampeni za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kupitia Chadema dada Asia Msangi

Kwa umati huu ni salamu kwa Mwenyekiti wa ccm taifa kuwa upinzani kupitia vyama vya siasa ni imani iliyojengeka kwenye fikra za wananchi

Upinzani haumalizwi kwa nguvu ya dola, nguvu ya dola hunyamazisha tu upinzani lakini siyo kuufuta, ili mpunguze nguvu ya upinzani tendeni haki kwa makundi yote ya kijamii bila kujali matabaka

Ccm wajitafakari siasa zao za hovyo namna zinavyogawa taifa kwa misingi ya kisiasa, hali hii inaongeza upinzani dhidi ya ccm na serikali kwa ujumla badala ya kuupunguza nguvu

Chama kilicho na rasilimali watu wengi namna hii utasemaje kinakufa! Akili za kujipa faraja hewa kwa Viongozi wa ccm na serikali iliyopo madarakani kuwa upinzani umekufa ndio zinawafanya washindwe kuona jambo katika uhalisia wake

Tunaomba mpambano huu wa Chadema vs Ccm uwe wa kisiasa na siyo mpambano wa vyombo vya Usalama vs Chadema kama ambavyo tumeona chaguzi karibu zote zilizopita

Rais Magufuli simamia haki ya wananchi ya kuchagua chaguo lao sahihi na siyo vyombo vya dola viwe sehemu ya haki hiyo kuchagulia wawakilishi wao kwa niaba yao kama ambavyo imezoeleka chaguzi nyingi zilizopita
Ccm ilishachokwa kitambo sana ndiyo maana sasa wanalazimisha kukubalika
 
Back
Top Bottom