laki si pesa.
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 10,003
- 9,731
kwani hao watu wote wamekuambia wataipigia kura Chadema? Kuna wana CCM hapo wamekuja kuwachora tuHali kama hii ndio inawafanya CCM washindwe kuelewa wafanye nini kuimaliza CHADEMA na upinzani kwa ujumla.
Nilishwaambia kupitia hapa JF kuwa wanachokifanya kwa lengo la kutaka eti kuua upinzani hakina tofauti na mtu anaetaka kuua nyoka kwa kuponda mkia badala ya kichwa.
Watakachofanikiwa ni kuchelewesha tu safari ya mabadiliko lakini sio kukwamisha safari hiyo kufika mwisho.Safari hii kufika mwisho ni swala la muda tu na si vinginevyo.
Kwa kifupi, CCM wamepaniki, wamechanganyikiwa, wamejawa hofu ya kupoteza dola na zaidi wako very frustrated kiasi kwamba wameamua hata kama watatoka madarakani basi watoke wakiwa wamefanya kila aina ya vurugu, vituko, uovu, n.k kwani wameshajikatia tamaa na hivyo hawaoni hasara kufanya lolote maana hakuna hasara kubwa kwao kama kupoteza dola.
Yaani walichoamua ni kama ni yale ya kwenye soku kuwa hata kama mnatufanga, lakini na sisi chenga twawala.
Bahati mbaya wao chenga zao ni Polisi, NEC, Wakurugenzi wa Halamashauri, n.k.