gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,045
Viongozi wa kitaifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dr Vicente Mashinji na Mbunge wa Jimbo la Kawe Mh Halima Mdee wakihitimisha kampeni za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kupitia Chadema dada Asia Msangi
Kwa umati huu ni salamu kwa Mwenyekiti wa ccm taifa kuwa upinzani kupitia vyama vya siasa ni imani iliyojengeka kwenye fikra za wananchi
Upinzani haumalizwi kwa nguvu ya dola, nguvu ya dola hunyamazisha tu upinzani lakini siyo kuufuta, ili mpunguze nguvu ya upinzani tendeni haki kwa makundi yote ya kijamii bila kujali matabaka
Ccm wajitafakari siasa zao za hovyo namna zinavyogawa taifa kwa misingi ya kisiasa, hali hii inaongeza upinzani dhidi ya ccm na serikali kwa ujumla badala ya kuupunguza nguvu
Chama kilicho na rasilimali watu wengi namna hii utasemaje kinakufa! Akili za kujipa faraja hewa kwa Viongozi wa ccm na serikali iliyopo madarakani kuwa upinzani umekufa ndio zinawafanya washindwe kuona jambo katika uhalisia wake
Tunaomba mpambano huu wa Chadema vs Ccm uwe wa kisiasa na siyo mpambano wa vyombo vya Usalama vs Chadema kama ambavyo tumeona chaguzi karibu zote zilizopita
Rais Magufuli simamia haki ya wananchi ya kuchagua chaguo lao sahihi na siyo vyombo vya dola viwe sehemu ya haki hiyo kuchagulia wawakilishi wao kwa niaba yao kama ambavyo imezoeleka chaguzi nyingi zilizopita