kwa uharamia huu watoto wa masikini wataendelea kukosa elimu bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa uharamia huu watoto wa masikini wataendelea kukosa elimu bora

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ptz, Feb 26, 2012.

 1. P

  Ptz JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  [FONT=&quot]Saloom wanaJamvi, nashindwa kuwaelewa watumishi wakuu na watendaji watoa maamuzi wanapokula matapishi yao, hivi karibuni wizara ya elimu ilitoa ajira mpya za walimu na kutoa angalizo kuwa[/FONT] “KilamwalimuanatakiwakwendakwenyeHalmashauri alikopangwa. HAKUNA MABADILIKO YATAKAYOFANYWA. Mwalimu anatakiwa kwenda na VYETI vyake halisi, ambaye hataripoti ifikapo tarehe 14 Februari 2012 atapoteza nafasihiyo.” Cha kushangaza tarehe 17 Februari wizara hiyo hiyo katika tovoti ile ile wametoa tangazo lifuatalo “AJIRA MPYA WALIMU MWAKA 2011/12 WALIMU WALIOBADILISHIWA VITUO Walimu ambao waliomba kubadilishiwa vituo kwa sababu mbalimbaliwanatakiwa kuripoti katika vituo vipya walivyobadilishiwa. Mwalimuanatakiwa kwenda na VYETI vyake halisi, ambaye hataripoti ifikapo tarehe25 Februari 2012 atapoteza nafasi hiyo.” Ukiangalia kwa makini orodha ya walimu waliopangiwa vituo vipya utakuta kuwa walimu hao walipangwa katika vituo vyenye mazingira magumu sana na sasa wamepelekwa mijini kama kwa mfano, toka Sumbawanga DC kwenda Morogoro manispaa, toka Rorya kwenda Kibaha TC, Mbeya vijijini kwenda Mbeya jiji nakadharika. Nimeona pia jina mtoto Mh Mwanry Aggrey kamtoa mwanaye aliyekuwa kapangwa Rorya na kumrudisha nyumbani Siha (angalia jina namba 7) Kwa hali hii bado shule zilizokatika mazingira magumu zitaendelea kukosa walimu na kiwango cha elimu kitaendelea kushuka kwani orodha iliyotolewa ni wachache tu kati ya wengi waliobadilishiwa kinyemela. Nchi yetu haitajengwa kwa uharamia huu, watoto wa masikini wataendelea kukosa haki zao za msingi kwa kunyimwa elimu bora, kama kweli wizara hii iko makini hawa wote waliobadilishiwa vituo wanatakiwa wasipewe ajira kwani wamekiuka agizo la awali kwa kutoripoti katika vituo vyao kwa wakati yaani kabla ya tarehe 14 Februari, La kuumiza zaidi wakati wizara ikiwa busy na kuchakachua vituo vya kazi bado kuna walimu kibao wamekosa ajira na hasa wenye shahada ninao ushahidi wa kutosha kwa hili. Naomba kutoa hoja.


   

  Attached Files:

Loading...