Kwa Ufupi: Historia ya Padri, Pio wa Pietrelcina

ulimi waupanga

Senior Member
Aug 31, 2014
199
500
Pio wa Pietrelcina (25 Mei 1887 - 23 Septemba 1968) alikuwa Padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa Ndugu Wadogo Wakapuchini

Alipingwa na kudhulumiwa, lakini pia aliheshimiwa na umati wa watu, kutokana na karama na wingi wa miujiza iliyoshuhudiwa.

Alizaliwa na wakulima Grazio Maria Forgione na Maria Giuseppa De Nunzio tarehe 25 Mei 1887 huko Pietrelcina , karibu na Benevento, akabatizwa kesho yake katika kanisa la Mtakatifu Anna na kupewa jina la Francesco kwa heshima ya Fransisko wa Asizi.

Tarehe 27 Septemba 1899 alipokea sakramenti za Kipaimara na Ekaristi. Francesco hakufuata shule kwa utaratibu uliotarajiwa kwa sababu alitakiwa kusaidia familia yake shambani.

Alipofikia umri wa miaka 12 padri Domenico Tizzani, alimsomesha kwa miaka 2 elimu yote ya msingi. Hamu ya kuwa mtawa na padri ilijitokeza mapema, hasa kwa kumuona bradha Camillo wa Sant'Elia a Pianisi akipitia kijijini kuombaomba. Mwaka 1902 alianza utaratibu wa kujiunga na shirika, ambalo baada ya kumkataa mara ya kwanza, lilimkubali.

Alisimulia kuwa tarehe 1 Januari 1903 alianza kujaliwa njozi: moja ilimfunulia wito wake wa kupambana na shetani , nyingine ilimhakikishia upendeleo wa Mungu na Bikira Maria .

Tarehe 22 Januari alianza mwaka wa unovisi kwa jina la ndugu Pio. Kisha kuumaliza na kuweka nadhiri za useja mtakatifu , ufukara na utiifu, alikwenda masomoni na tarehe 27 Januari 1907 aliweka nadhiri za daima. Mnamo Novemba 1908 alihamia Montefusco, kwa masomo ya teolojia . Tarehe 18 Julai 1909 alipewa daraja takatifu ya ushemasi , na tarehe 10 Agosti 1910 ile ya upadri.

Miaka hiyo alianza kuugua sana na kupatwa na mateso yaliyomshirikisha na yale ya Yesu , kama vile madonda mikononi , mapigo ya mijeledi na taji la miba kichwani.

Akiwa San Giovanni Rotondo, katika wilaya ya Foggia, mkoa wa Puglia, mnamo Agosti 1918 Pio alisema ameanza kutokewa na mtu anayemchoma kwa mkuki ubavuni, na hatimaye akaonekana na madonda matano ya Yesu. Viongozi wa Kanisa walianza kutuma mfululizo wa wataalamu kufanya uchunguzi uliomsumbua sana padri Pio, hatimaye tarehe 31 Mei 1923 walitoa hati ya kuangalisha watu wasiamini ni mambo ya Kimungu.

Miaka 8 baadaye ilitolewa hati nyingine iliyomkataza asiadhimishe Misa hadharani wala sakramenti ya kitubio. Padri Pio alitii kwa unyenyekevu wote.

Mwaka 1933 Papa Pius XI alifuta makatazo hayo na Pius XII alihimiza watu kumtembelea. Tarehe 9 Januari 1940 kwa misaada iliyotoka duniani kote alianza ujenzi wa hospitali kubwa Casa Sollievo della Sofferenza ili kutibu na kuliwaza wagonjwa.

Mwaka 1950 idadi ya watu waliotaka kuungama kwake iliongezeka na kuhitaji ufanyike mpango wa kujiandikisha. Papa Yohane XXIII aliagiza ukaguzi mwingine kutokana na mashtaka mapya, lakini Papa Paulo VI alikuwa anamheshimu sana.
Madonda yake yalitoweka wakati wa Misa siku tatu kabla ya kifo chake , kilichotokea tarehe 23 Septemba 1968 padri Pio akiwa na miaka 81.

Kuna ushahidi wa watu mbalimbali kuhusu Padri Pio kuwa na karama ya kusoma moyo wa mtu, kupatikana mahali pawili kwa wakati mmoja (kwa Kiingereza: bilocation ) n.k.

Kesi ya kumtangaza mwenye heri ilianza mapema, lakini ilichukua muda mrefu, kutokana na upinzani wa watu mbalimbali.
Papa Yohane Paulo II , aliyewahi kumtembelea padri Pio miaka 40 ya nyuma, tarehe 21 Januari 1990 alitangaza ushujaa wake katika maadili yote, tarehe 2 Mei 1999 alimtangaza mwenye heri na tarehe 16 Juni 2002 alimtangaza mtakatifu.

Mwenye Miujiza, Matendo na visa vya uyu mtawa anaweza kutujuza ili tujifunze zaidi.

220px-Padre_Pio.jpeg
Padre-Pio-young.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,884
2,000
Kwakweli kisa cha kuonekana sehemu mbili tofauti kwangu ndio muujiza wa ajabu sana kwa huyu Padre. Lakini pia Kanisa Katoliki tunapaswa kujifunza kwa haya yanayotokea.

Ipo mifano ya watakatifu wengi ambao hatua za awali walipingwa sana hadi na maaskofu lakini baada ya uchunguzi wa muda mrefu inagundulika kweli ni kazi ya Mungu.

Mfano ni kwa muanzilishi wa rozali ya huruma (St Faustina), huyu alikuwa anakutana na Yesu na kumuagiza mambo mbalimbali lakini maono yake yalipingwa mno.

Hata aliposema Yesu amemuambia kutatokea nyota mpya kutokea Poland ambayo Itatekeleza aliyosema hakuaminika. Hadi askofu mmoja kutoka Poland alipoanza kufatilia habari za Mtakatifu huyu na kukusanya documents/ushahidi muhimu kwaajili ya kuwakilisha Vatican kama uthibitisho.

Askofu huyo alipokamilisha tu kazi yake ndio akaja kuwa Pope John Paul II ambaye ndiye aliyeipitisha jumapili ya huruma ya Mungu kila baada ya pasaka kama Yesu alivyomuagiza St Faustina na pia kumtangaza mtakatifu.

Kama Kanisa lingekuwa ling'amua mapema maono ya watakatifu pengine tungeweza kuzitumia tunu hizo kwa wakati badala ya uchunguzi ambao mara nyingi unakuja kudhibitishwa hata Mtakatifu mwenyewe ameshafariki. Fatilia hata kisa cha watoto wa Fatima jinsi mwanzo walivyopata upinzani.

Maaskofu wengi ni too rigid pale panapokuwa na miujiza hata kama inatokea kwa Padre achilia mbali mlei (hao ndio shida zaidi).

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
2,031
2,000
Dunia haiko 'fair' kabisa.

Hayo mambo(miujiza) aliyofanya huyo padri, kwa mzungu ni utakatifu ila akifanya mtu mweusi ni uchawi na ushirikina.

Wazungu sio watu wazuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom