Kwa ufupi haya ndio maendeleo tuliyoyachagua 2015 kupitia Rais John Pombe Magufuli

Leslie Mbena

Verified Member
Nov 24, 2019
70
150
KWA UFUPI HAYA NDIO MAENDELEO TULIYOYACHAGUA 2015 KUPITIA JEMEDARI WETU NDUGU JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 12:30pm 03/06/2020

Chini ya Rais John Pombe Magufuli tunajenga Bwawa la Umeme la Rufiji litakalo zalisha Megawati 2,200 ikiwa sasa Taifa letu linatumia Megawati 1,100 tu kwa hiyo Bwawa la Umeme la Julius Nyerere kule Rufiji litazalisha Umeme tunaotumia Sasa mara mbili,hii ni faida kubwa kwa Taifa na shukrani za dhati ziende kwa Rais wetu,Ndugu John Pombe Magufuli.

Baada ya Kujenga Bwawa la Umeme,chini ya Rais John Pombe Magufuli tunakwenda kujenga Viwanda vitakavyotumia Umeme huo kuviendesha,Viwanda vitatengeneza Taifa linalojitegemea ambalo nguzo kuu ya uchumi wake ni sekta ya viwanda.

Tunataka tufike mahali ambapo Taifa letu litakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kutekeleza mipango yake ya maendeleo bila kutegemea misaada.

Tanzania ni tajiri, na mara zote Rais John Magufuli ametuhakikishia kwa kusema kuwa sisi Tanzania ni Matajiri kwelikweli,hii ameirudia mara nyingi hata mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, NEC Tanzania ni Tajiri, ni Tajiri, walatusiwe na wasiwasi na utajiri wa Tanzania na chini yake yeye Rais Magufuli ameapa utajiri huu wa Maliasili za Tanzania lazima ulete neema nyingi kwa Taifa la Tanzania tuondokane na umasikini,tubadilishe rasilimali hizi ziwe shughuli zitakazoongeza kipato cha kila Mtanzania mmoja mmoja na kwa ujumla tuongeze pato la Taifa letu la Tanzania, sisi Tanzania ni Matajiri kwelikweli.

Katika Awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli,tumegundua Tanzania tuna almasi ila tulikuwa hatufaidiki nayo,Chini ya Rais John Pombe Magufuli makampuni hayo tumefanya nao mazungumzo,namna ya kubadilisha zile hisa zao zilizokuwa zinatunyonya ili kuifaidisha Tanzania hata vizazi vijacho vije kula mema ya nchi kupitia mali asili tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu,

Tanzania tuna kila kitu, ukienda kule Zanzibar kuna mafuta, yale mafuta yakishakuwa Zanziba maana yake hata Bara yapo, tuna gesi ya etheny ipo,

Tuna helium, ukienda kule Mtwara kwa Waziri Mkuu kuna graphite, kule tunakanyaga udongo lakini ndani udongo kuna graphite, ndugu zangu Wamwela hawajui ni kama Wasukuma ambavyo walikuwa hawajui almasi wakawa wanacheza nazo kwenye bao mpaka alipokuja Williamson, Tanzania ni Tajiri ndugu zangu.

Chini ya Rais Magufuli wala tusiogope kuyasemea haya na kusimama imara kulinda rasilimali zetu. Dhababu ipo kila mahali, inawezekana hata hapa ukichimba utakuta dhahabu kwenye jengo hili, dhahabu ipo kila mahali.

1. Ujenzi wa Stiegler's gorge HP Bwawa kubwa la Umeme litalozalisha Megawati 2,300

Mradi huo ambao unafahamika pia kwa jina la Julius Nyerere, unatazamiwa kuzalisha megawati zaidi ya 2,000 za umeme, hatua ambayo inaelezwa kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

2. SGR Treni ya Umeme toka Dar mpaka Moro hadi Dodoma mradi ambao unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa Mwaka huu.

3. Uundwaji wa meli kubwa katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa.

4. Ununuzi wa Ndege kubwa 10 Boeing,Airbus na Bomberdier na upanuzi wa viwanja vya ndege na vya kisasa kabisa.

5. Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa( fly overs ya Mfugale ,Interchange ya Ubunge na Madaraja Makuba mawili yatakayokatiza kwenye maji ya Busisi across lake Victoria na Tanzanite bridge katika Bahari ya Hindi, Ujenzi wa barabara nane ubungo - chalinze ambao ni ujenzi na upanuzi wa barabara wa kisasa kabisa unaoruhusu magari kupishana hata matatu hivyo kupunguza ajali.)

6. Usambazaji wa umeme kuanzia kwenye tarafa, kata hadi vijiji al maarufu kama Umeme wa Rea.

7. Vituo vya afya bwerere zaidi ya 390 Tena vya kisasa na huduma ya oparesheni ili kupunguza vifo vya uzazi ambavyo uzazi uligeuka laana na Sasa Uzazi utakwenda kuwa baraka,

8. Miradi ya maji na usambazaji wa maji maeneo mengi ukiwamo mradi wa maji ya Ziwa Victoria toka Mwanza kuja Singida hadi Dodoma.

9. Uboreshaji wa vyuo na sekondari zilizichoka tangu enzi za Mwalimu Nyerere,Shule zote zimejengwa upya na kurekebishwa vizuri na sasa zina muonekano mzuri kabisa na mazingira bora ya kusoma,

10. Wanafunzi kukaa chini imebaki historia,

11. Ufufuaji na usimamizi wa mazao na kumnufaisha mkulima( pamba, mkonge, chikichiki, korosho, ufuta.) Pamoja na uondoaji wa tozo.

12. Usimamizi wa mapato ya serikali uliowezesha serikali kuwa na akaunti moja badala ya 2000.

13. Usimamizi mzuri wa vita ya corona. Hapa kila mtanzania alijua tumeisha. JPM alitia ujasiri wa hali ya juu sana na virusi vya kupandikizwa Maabara vikashindwa.

14. Upigaji na upigwaji kwenye ardhi umepungua kwa asilimia 90.
Mengi sana najiandaa kuandika vitabu,

15.Elimu Bure kwa kila Mwanafunzi,

16.Mbuga za Wanyama, mpaka sasa chini ya Rais John Pombe Magufuli Tanzania tunaongoza tuna Hifadhi za Taifa 22 zina Wanyama wote, hata mti mrefu kuliko yote Afrika upo Tanzania, Mlima mrefu kuliko yote Afrika upo Tanzania Mlima Kilimanjaro, Mungu ametupendelea, Tanzania Hoyee

17.Upanuzi wa vituo vya Afya zaidi ya 390 umefanyika na ujenzi wa vituo 7,200 vya kutolea huduma za Afya katika vijiji,

18.Shirika la NDC limeweza kuuza matrekta 684 yenye thamani ya 30 Bilioni sawa na 83.2% ya matrekta 822 yaliyo wasili nchini.

19.Ufufuaji wa mashamba ya kwa sasa uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 86.7 kwa kipindi cha miaka miwili ambapo hapo awali hakuna kumbukumbu zozote kutokana na muwekezaji wa awali aliyekua akisimamia shamba,

Uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 86.7 zenye thamani ya shilingi 210 milioni na kuajiri Watanzania 278,katika Awamu hii ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.

Kupitia mradi huu tumetengeneza ajira zaidi ya 2000 za moja kwa moja,

Kwa kipindi cha takriban miaka miwili, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi 2.6 Bilioni hadi Shilingi 6.9 Bilioni sawa na 164.3% kutoka mwaka 2017 hadi 2019.

#Kama unayo mengine Ongeza hapo chini.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,933
2,000
Kwa kuwa ilani yetu imetekelezwa kwa 100% jpm atashinda kwa %99.999
Tume ya uchaguzi na vyombo vya dola muviongezee nguvu, kuhakikisha vinalinda ushindi wa dhuluma.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,884
2,000
Angeshinda Lowasa mpaka muda huu Wafanyakazi tungekuwa tunaogelea kwenye dimbwi la utajiri wa kipato! Siyo huyo mtu wenu.

1)Elimu
2)Elimu
3)Elimu

Mabadilikooooo!!! Lowasaaaaa!!!
 

Rutorial k

JF-Expert Member
Jun 8, 2014
905
1,000
Yote hayo ni kwa kudhurumu haki za raia na kuwafanya wawe masikini wa kutupwa. Maendeleo lazima yaendane na kuboreka kwa maisha ya watu. Tangu aingie madarakani hakuna nyongeza ya mshahara wala increment,ajira ndio usiseme (eti watu Wajiajiri wakati yeye aliajiriwa),kuanguka kwa mazao ya biashara kwa kujiona anajua kila kitu mfano korosho na pamba hoi. Yani hadi hayo mamiradi yanakamilika atakuwa ameshaua raia wote kwa umaskini uliotopea
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
465
500
Umesahau kitu kimoja: Wanachi ametujaza mapesa mfukoni. Hatuna wasiwasi hata lock-down ya Korona ikiwekwa. Bravo Ccm!
 

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
509
1,000
White elephant projects.

Being stupid is a choice.
Samahani mtoa mada. Sikufurahia mchango wako. Uchangiaji wa aina hii unashusha hadhi ya jukwaa hili. Badala ya kutoa hoja inayoainisha ubovu wa hoja kwenye mchango wa unayempinga, unaishia kumtukana tu na kauli ya kwamba "being stupid is a choice". Mtu kataja uenezaji umeme vijijini, ujenzi wa madaraja (flyovers), wanafunzi kusoma bure, ufuaji wa umeme huko Stiegler's Gorge, ujenzi wa reli ya kisasa, n.k. Wewe unayapuuza yote haya kwa maneno mawili tu "white elephant"! Hivi kweli msongamano wote wa magari hapo Ubungo bado unaliita daraja la hapo "white elephant"? Watanzania kupelekewa umeme vijijini unakuita "white elephant"? Sioni hata kitu kimoja alichokitaja mchangiaji ambacho honestly unaweza kukiita 'white elephant'. Fafanua ni vipi mifano aliyotoa mchangiaji ni "white elephant". Mbaya zaidi ni ile lafudhi ya kumuita mchangiaji mwenzako 'stupid', which is actually what you did with your veiled statement 'being stupid is a choice'! MODS, you may wish to look into this as defeats the objective of the forum of being an arena where great thinkers contribute meaningful discussions, while honoring other people's opinions.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,721
2,000
Ulikuwa ujinga sana
Angeshinda Lowasa mpaka muda huu Wafanyakazi tungekuwa tunaogelea kwenye dimbwi la utajiri wa kipato! Siyo huyo mtu wenu.

1)Elimu
2)Elimu
3)Elimu

Mabadilikooooo!!! Lowasaaaaa!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom