Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Amekuwa ni chaguo lisilo chaguo; chaguo lililojichagua na kuchaguliwa. Ilikuwa ni "Urais au nothing". Bilali hakuwa na uamuzi wa kurudi bila ya kitu kinachokaribiana na urais. Uamuzi wa Shein kugombea Zanzibar umekuja baadaye sana baada ya kuona kuwa mtu pekee mwenye nguvu Zanzibar kuweza kumrithi Karume ni Bilal hao kina Nahodha na wenzake walikuwa ni wasindikizaji tu.
Hata hivyo Bilal kwa sababu wanazozijua wao alikuwa tayari anaigawa Zanzibar na kugombea kwake Zanzibar kungempa ushindi mwepesi tu Seif. Lakini hakuwa tayari kujitoa safari hii na alijua kabisa nguvu pekee anayoshindana nayo ni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Lakini alikuwa anajua vile vile kuwa JK ni dhaifu kwenye masuala magumu. Alijua JK hawezi kufanya kazi kukiwepo na dissent ya kweli ndani ya CCM, dissent ambayo kwa mara ya kwanza ingewapa ushindi rahisi zaidi Zanzibar. Lakini kilichoharibu ni wajumbe wa kutoka Zanzibar walioamua kuondoka juzi kwa hasira kurudi Zanzibar wakiwa na dhamira moja tu nayo ni kuhakikisha Shein hashindi visiwani.
Lakini JK ni mwanasiasa ambaye anatumia nafasi zinazojileta kuzuia migogoro, yuko tayari kumuachilia mtu wake wa karibu aanguke (kama linamletea yeye sifa) na kama kumleta karibu mtu ambaye ni tatizo kwake.
Sasa, Bilal ni chaguo lililojichagua; hawakumpa nafasi JK kumchagua mtu mwingine, asingeweza kumchagua mtu mwingine; hakukuwa na uwezekano wa kumchagua mtu mwingine.
Ni jinsi gani hawa wawili watafanya kazi? Ni jinsi gani wataweza kupatana?
Well.... Wamarekani wanasema... "Politics make strange bedfellows"..
Historia itaamua.
MM