Kwa ufisadi huu wa udom ni zaidi ya kiasi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa ufisadi huu wa udom ni zaidi ya kiasi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zema21, May 19, 2012.

 1. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Ikiwa ni miezi sita imepita toka yalipofanyika mahafali ya katika chuo kikuu cha Dodom(Udom) inashangaza sana kuona ni jinsi gani chuo hicho kinaongozwa na genge la mafisadi.
  Wahitimu wa mwaka 2011 walitakiwa kulipia ukodishaji wa josho shilingi 45,000/= za kitanzania kwa kila mhitimu, ahadi ilikuwa fedha shilingi 20,000/= zingerudishwa mara baada ya mhusika kurejesha joho (kwa wahitimu zaidi ya 5000). Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha siku ya urejeshaji wa majoho wahitimu walitakiwa kuandika akaunti namba kwa ahadi kuwa fedha hizo zitalipwa kupitia akaunti namba za wahusika baada ya wiki mbili. Cha ajabu mpaka leo fedha hizo hazijarejeshwa wala haifahamiki ni lini zitarejeshwa. Mwezi wa tatu mwishoni ilitolewa ahadi kuwa fedha hizo zingerejeshwa mwezi wa nne mwanzoni. Lakini hiyo ilikuwa ahadi ya kisiasa kama ilivyo kawaida ya chuo hicho kikuu cha kisiasa cha chama cha magamba.
  Pia hata fedha za taadhari za wahitimu hao walizolipa wakati wakianza mwaka wa kwanza chuoni hapo zilitakiwa kurejeshwa pindi wanapohitimu lakini hilo halikufanyika.
  Pia itakumbukwa jinsi gani fedha za mikopo zinavyocheleweshwa kulipwa kwa wanafunzi ambapo kuna wakati wanafunzi hukaa hata mwezi mmoja wakiwa bado hawajalipwa fedha zao za chakula na malazi. Hata sasa wasomi hawa wa udom wanalia njaa mno.
  Lakini pia sote tunakumbuka jinsi wanataaluma chuoni hapo walivyogoma mwaka 2011 mwanzoni kutokana na mishahara yao kuwa inachakachuliwa na chuo kilikuwa kikianda salary slip zilizochakachuliwa tofauti na zile zilizokuwa zinatoka hazina.
  Hivi mwisho wa haya yote ni nini?
  Lakini kila lenye mwanzo lina mwisho wake pia
   
 2. A

  Adili JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,009
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mtanzania kila kitu ufanyiwe

  Badilka, walalamikaji wote unganeni na kuuburuza uongozi wa UDOM mahakamani mkidai hela zenu na riba. Mkishinda wabebeshwe na gharama za kesi.

  You want something done - diy
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,077
  Trophy Points: 280
  All of the system is corrupt top-down,kama rais naye ni corrupt then kipi cha kushangaza mkuu,pelekeni M4C pale mpaka kieleweke

  ''No body can give you freedom,no body can give you peace or justice or anything else,if you are a man you take it''...

  Malcom X.
   
 4. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ulisoma matangazo yao kwente website yao ukayaelewa? waliongea kuhusu majoho
   
 5. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  tangazo lipi?
  manake tangazo la mwezi march lilisema fedha zingerejeshwa mwanzoni mwa april na vyeti vitatolewa katikati ya mwezi apri

  l
   
 6. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  mzee system ni ile ile ukipeleka mahakamani usitegemee jipya!
  mahakama ya uma sa hv ndo mpango mzima!
  wakifanya ufisadi wao tunawashtaki kwa uma na jamii ya watanzania na ulimwengu mzima
   
 7. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  transcrpt na vyeti mpaka leo ni ndoto kaka, bora hata wangetoa vyeti na kukaa na hizo hela za majoho. Udom kwa kweli kama ni siasa basi zimezid wadau. Unamaliza chuo unakaa mwaka mzima bila cheti hii kweli aibu
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama mmeambiwa mtaingiziwa kwenye akaunti basi mmeliwa. Maana the only way ni kufanya TISS transfer na huwezi kutuma amount ya 5000 na hata kama ukiruhusiwa gharama ya TISS transfer moja ni abt atleast 5000 kwahiyo ni impossible. Labda kama wanafunzi wote wana account kwenye benki moja na UDom ina akaunti kwenye benki hiyo hapo transfer ya kawaida account to account inaweza kufanyika which is cheaper au free kabisa for some banks.
   
Loading...